Aliacha kazi ya ualimu saizi ana maduka ya hardware na supermarket kibao

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
14,304
29,842
Anitwa Abdallah Idd kutoka songea, alikuwa mwalimu Kwa miaka kumi mkoani dodoma wilaya ya BAHI halmashauri ya BAHI DC. Familia yake ilikuwa ikiishi songea mjini kwakua huko ndo alikuwa na duka lake moja la kuuza nafaka na mtu pekee wa kusimamia hiyo biashara ni mke wake

Alihangaika kuomba uhamisho lakini juhudi zake hazikuzaa matunda akaamua kuchukua maamuzi magumu ya kuacha kazi, alimwambia mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bahi kuwa "Hii kazi ya ualimu haiwezi kunitenganisha na Familia yangu Kwa miaka kumi, Naomba nikuachie kazi Yako mheshimiwa"

Alivyosema hivyo akabeba begi lake kwenda kwao songea, mwanzo alikutana na changamoto baada ya kuacha kazi lakini baada ya miaka mitano mbele mambo yalibadirika biashara yake ya duka la nafaka likawa kubwa kuliko duka lolote pale songea mjini,

Hakuridhika na sehemu hiyo tu, akabid ajiongeze kufungua biashara zingine saizi anamaduka mengi sana ya hardware, ukitaka nondo, mabati mbao, misumari na vipuri vyote vya pikipiki na magari basi utaenda hapo, supermarket anazo za kumwaga. Kipato chake Kwa mwaka mwamba anatengeneza zaidi ya million sabini

Haya wewe mwalimu tuambie, ukijumlisha na kamshahara ka kufungia mwaka 2023 umetengeneza kiasi gani zaidi ya kunuka jasho tu
 
Kwanza kabisa niwashukuru sana walim wote kwa juhudi na maarifa mnazotumia kutuondolea Ujinga vichwani mwetu..

Walimu kokote mliko mzidi kubarikiwa na muishi maisha yasiyo mkwaza Mungu.

Cha pili niwaombe sana walimu kokote mliko msitishwe wala kurudishwa nyuma na hizi kelele za wanafunzi wenu hawajui walitendalo

mambo ya kuwa tajiri ni suala tambuka sana
 
Anitwa Abdallah Idd kutoka songea, alikuwa mwalimu Kwa miaka kumi mkoani dodoma wilaya ya BAHI halmashauri ya BAHI DC. Familia yake ilikuwa ikiishi songea mjini kwakua huko ndo alikuwa na duka lake moja la kuuza nafaka na mtu pekee wa kusimamia hiyo biashara ni mke wake

Alihangaika kuomba uhamisho lakini juhudi zake hazikuzaa matunda akaamua kuchukua maamuzi magumu ya kuacha kazi, alimwambia mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bahi kuwa "Hii kazi ya ualimu haiwezi kunitenganisha na Familia yangu Kwa miaka kumi, Naomba nikuachie kazi Yako mheshimiwa"

Alivyosema hivyo akabeba begi lake kwenda kwao songea, mwanzo alikutana na changamoto baada ya kuacha kazi lakini baada ya miaka mitano mbele mambo yalibadirika biashara yake ya duka la nafaka likawa kubwa kuliko duka lolote pale songea mjini,

Hakuridhika na sehemu hiyo tu, akabid ajiongeze kufungua biashara zingine saizi anamaduka mengi sana ya hardware, ukitaka nondo, mabati mbao, misumari na vipuri vyote vya pikipiki na magari basi utaenda hapo, supermarket anazo za kumwaga. Kipato chake Kwa mwaka mwamba anatengeneza zaidi ya million sabini

Haya wewe mwalimu tuambie, ukijumlisha na kamshahara ka kufungia mwaka 2023 umetengeneza kiasi gani zaidi ya kunuka jasho tu
Thubutu uache kazi bila mpango ndo utajua jiji
 
Aina nyingine ya UMASKINI na UJINGA wa WATANZANIA kuendelea kuwa Maskini ni kila mmoja hasa Walimu na Manesi kutaka kufanyakazi Maeneo/Wilaya waliyozaliwa.
Shiiiiit.... Mchina kavuka mabara na mabara kaja mpaka Kijijini kwenu kutafuta, Mnigeria kavuka Nchi kibaoooo yuko Sinza hapo analisongesha, Wewe punguani kutoka Tunduru ukipangwa kazi Rorya ukoo mzima wanalalamika ndugu yetu anaenda kupotea.
Hii mentality ni ya kimaskini sana sana sana na ndiyo inafanya tusiende Nje ya Nchi kutafuta fursa, sembuse ndani kwa ndani tumeshindwa tutaweza kwenda Sudani kusini au Commoro kutafuta?
 
Back
Top Bottom