Nimesoma michango ya wadau, wengi wameshauri ufanye uchunguzi ujiridhishe. Kwa maoni yangu usifanye hivyo naamini madhara yake kama utakuta ni kweli basi yatakua makubwa sana kwenye nafsi yako na kamwe hayata tibika.
Silaha kuu kwenye mapenzi ni kuaminiana na kamwe si kulindana kwa kuchunguzana.
Kama umehisi imani imepotea kwako basi fanya maamuzi sasa na wala usichunguze. Kama ilikua kweli au si kweli mkeo ataeleza mwenyewe bila kumuuliza ila utakua salama kwenye nafsi yako na hata kama atakudanganya ni bora maana hutakua na kidonda moyoni mwako.
Usithubuti kufanya mipango ya kufumania hata kama utaamua kumuacha mkeo. Kitendo hicho hakitakuja kufutika maishani mwako kamwe na kitaendelea kukuuma milele.
Hatua za kuchukua;
1. Kata mapenzi kwake ila usimnyime matumizi.
2. Ukiona hajali khs hatua hiyo, muache kwa muda. Muondoe au ondoka.
3. Akiendelea kukomaa, Anza kumsahau na tafuta mwingine.
Hakikisha hatua hizo hapo juu unawashirikisha ndugu pia na unapoongea nao usiseme umehisi ila una uhakika anatembea na jirani yako. Kazi ya kuthibitisha na kukanusha waachie wao na mkeo waicheze, wewe usishiriki.
Mpaka hapo utaona mbivu na mbichi ila kama bado unampenda sana mkeo basi usuruhisho utakaopatikana katika hatua yeyote hapo juu utaleta maana na hata kama utadanganywa lakini itakua afya kwako na upendo unaweza kurudi. Naamini kama alikua anafanya au dalili za kutaka kufanya basi hata rudia.
Kumbuka ukielezea hisia zako na ilikuwaje mpaka ukahisi hivyo utakua umeanika mbinu zako na unaweza kuonekana ni dhaifu au hujabaini mipango yao ila unahisi tu.
Kuchukua maamuzi bila kutaja mbinu zako zitakusaidia usijulikane uwezo wako na itamfanya mkeo awe muoga kurudia maana hajui unapataje taarifa. Amini baada ya hapo hata inzi tu akimgusa tako atakwambia kujihami maana labda umeishajua.