Ushauri: Jinsi ya kuishi na mwanamke mlalamishi

Ushauri: Jinsi ya kuishi na mwanamke mlalamishi

Joined
Oct 26, 2010
Posts
52
Reaction score
29
Ushauri Jamani,

Mke wangu ni mlalamishi sana pia ana wivu uliopindukia.Tulikuwa tukifanya kazi ofisi moja kwa kweli nilikuwa nikipata shida sana yaani nikicheka na msichana yeyote ofisini basi ni kwamba nampenda. Bahati nzuri nikahamishwa kikazi tena nimehama Mkoa kabisa lakini toka nilipohama amekuwa ana lawama za ajabu.

Yaani kila siku ofisini anaonewa yeye kila mtu anamnyanyasa yeye mpaka nakosa amani ukijaribu kufuatilia kiundani unagundua yeye ndio mkorofi. Jambo ni maswala ya urembo wake analalamika eti simpi hela ya saloon mara simnunulii nguo. Nikijaribu kumuuliza hivi wewe katika mshahara unaopata kwanini usitenge hela ya saloon inakua ni ugomvi ndani ukimpa hela kama laki mbili kwamba zitunze basi anaona kesha kuwa kama tajiri.

Ndani ya siku mbili ukiuliza anakwambia katumia elfu hamsini ukiuliza zimefanya nini unaonekana unamnyanyasa kisa anatoka familia ya kimaskini. Napata taabu jinsi ya kuishi na huyu mwanamke. Nimezaa nae mtoto mmoja lakini hatujafunga ndoa. Hawapendi rafiki zangu ilishatokea siku akamsingizia rafiki yangu kuwa amemtongoza.

Ushauri jamani nakosa raha kabisa
 
Mkutanishe na mwanasaikolojia maana hamna namna nyingine.
 
Nimezaa nae mtoto mmoja lkn hatujafunga ndoa... Hawapend rafiki zangu ilishatokea siku akamsingizia rafiki yangu kuwa amemtongoza..... Ushauri jamani nakosa raha kabisaaa

Huyo siku akiacha kulalamika umeumia tayari...
Anyways King Solomon feels you brother.
Proverbs 21:19New King James Version (NKJV)

19 Better to dwell in the wilderness,
Than with a contentious and angry woman


Proverbs 21:9King James Version (KJV)


9 It is better to dwell in a corner of the housetop, than with a brawling woman in a wide house.

Huyo mkeo hata the wisest man kasema ni noma. We anza mazoezi ya kukaa kwenye pembe ya dari tu ama porini, whichever suits you better.



And here is a bonus verse
[h=1]Proverbs 27:15New King James Version (NKJV)[/h]15 A continual dripping on a very rainy day
And a contentious woman are alike;

 
Kuna shida gani ukimpa hela ya saluni? ? Au unataka wenzio wampe????

Anyway vunja ukimya...ila inaonekana hata wewe una tatizo
 
Tatizo la kisaikolojia hilo, tafuta historia ya maisha yake utakuta kuna kipindi inawezekana aliishi katika maisha ya kunyanyasika au kuonewa sana. Anahitaji msaada wa kisaikolojia
 
kuna shida gani ukimpa hela ya saluni? ? Au unataka wenzio wampe????

Anyway vunja ukimya...ila inaonekana hata wewe una tatizo
Samahani mkuu naomba niulize, mke anafanya kazi, ana mshahara wake, mme nae ana kazi ana mshahara wake.

Huwa ni kwa nini mwanamme ampe hela ya saloon mwanamke ili hali nae ana mshahara?

Nauliza kwa nia njema tu, maana huwa sielewi logic yake.
 
Ki ufupi umekutana na Asha ngedere sio mke huyo
 
Unatabu malafyale utafanyaje sasa komaa nae hivo hivyo tunda lako hilo lina mchuzi na miba
 
Mpende saaana na jali hisia zake uwe na kauli nzuri tu kwake na kuwa mvumilivu km unampenda kweli,mambo yatajipa atapoa
 
Nadhani lazima utueleze mtoto ana umri gani,huenda tatizo lako tuko wengi,mimi ikinitokea ile anaanza kuongea in case niko nae go away for some times then she will forget once ukirudi,hebu jitolee kumlinda mtoto wako,other wise mtoto atajenga enough negative.
 
Pole me wangu ni mjamzito sipapendi tena kwangu kulivyo na shida
 
Back
Top Bottom