Nimejaribu kuelezea maana ya kuishi na mwanamke kwa akili

Artifact Collector

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
6,539
10,007
Moderator naomba usifute uzi au kuunganisha.

Pia uzi haujajikita kumjua mwanamke bali ni jinsi ya kuishi nae kwa sababu tunaishi na wanawake kama wapenzi wetu na kama wake
Na pia ni mtizamo wangu kwako msomaji unaweza usihafiki


Kwa mda nilioishi hapa dunian huu ndo mtizamo wangu na maon yangu juu ya kauli ya muishi na mwanamke kwa akili

Kuwa Muongo kiasi na sio sana
Hii ndo point namba moja ya kuish na mwanamke kwa akili kuanzia kwenye kumtongoza mpaka kwenye kuish nae kwa asilimia kubwa uongo inabid utumike kwa asilimia kubwa sana ili mahusiano yako na mwanamke/mke yadumu, uongo ninaoungelea ni ule wenye tija usiwe mkweli sana kwa mwanamke/mke wako sababu kubwa kiasili wanawake wanapenda fantasy na ni ngumu kuweza kutoa majibu ya moja kwa moja juu ya fantasy zao

Puuzia baadhi ya mambo anayofanya mwanamke
Kuna mambo mwanamke anaweza kukufanyia as long hayana negative impact kwenye mahusiano yenu au maisha yako achana nayo wala usiangaike nayo

Msikilize mwanamke wako kwa makini hata kama anaongea pumba
Mwanamke anapenda kusikilizwa hata kama anaongea pumba msikilize na mwambie utafanyia kazi usimcrash kabisa tafuta mda akiwa na furaha kile ulichoniambia hakiwezekan kwa sababu hizi na hizi

Usiyataje makosa ya mke wako wazi wazi mbele ya kadamnasi, kuyaropoka mbele za watu, au kwa watoto wako
mfano mke wako anaweza akawa amekupikia chakula kibaya kwa siku usimbwatukie tafuta mda akiwa na furaha mwambie kistaarabu, wanawake hawapendi kupingwa hasa anapokuambia jambo

Kubaliana na udhaifu wa mke wako wala usiangaike nao kuubadilisha
Usijaribu kubadilisha madhaifu ya mke wako/mwanamke wako kubalina nayo na ishi nayo na wala usipende kumwambia au kuyataja mbele za watu au kumtamkia kwa hasira yasitiri
Usimwambie mwanamke jambo flani huwez hata kama kweli huwezi kama mwanaume hautakiwi umwambie mwanamke au mke wako huwez ni kosa kubwa sana

Usimpe mke wako akuhifadhie fedha zako
Epukana na hili kosa kamwe mwanamke asiwe mtunzaji wa fedha zako, hakikisha unazitunza wewe mwemyewe

Usimwambie mwanamke huna hela hata kama kweli huna
Kosa kubwa kwa wanaume wengi ni kuwaambia wanawake zao hawana hela pale wanapohitaji tafuta namna ya kumjibu lakin usimwambie huna hela

Usipende sana kusifia sana mafanikio ya wanaume wengine waliofanikiwa zaid yako mbele ya mwanamke wako/mke wako. Hili ni kosa wanalofanya wanaume wengi hata kama ni rafiki zako wanamafanikio zaid ya mke wako usipende kuwasifia mbele ya mke wako au mwanamke wako hilo ni kosa kubwa sana

Sio kila jambo la kumwambia mke wako
Mfano unataka kusaidia ndugu zako usipende kumwambia mke wako hii ni kwa sababu wanawake wengi hawapendi ndugu wa mwanaume ni wachache sana watakaokua wanapenda ndugu zako kutoka moyoni na kwenye kuwasaidia wengi hawapendi kabisa, kama umepata mtoto nje ya ndoa usimwambie au usimlete mtoto wa nje ya ndoa uishi nae mara nyingi hawa watoto wa nje ya ndoa wanaondoaga aman kwenye ndoa ni bora mchepuko mwenye mtoto wako umpangie chumba/nyumba na umpe matunzo na sio umlete mtoto ndani ya nyumba, biashara zako zote usimwambie, mwambie baadhi au mishe zako za kupata hela hatakiwi kuzijua zote bali azijue baadhi

Mwanamke wako asijue ratiba yako ya kila siku mda mwingine unarudi nyumban saa tano asubuhi mda mwingine saa tano usiku bila kumpa taarifa akikulalamikia msikilize wala usimpe jibu baya au mwambie utalifanyia kazi usibishane nae

Usipende ligi/mabishano na mke wako au mwanamke wako
Mwanaume huwa anaongea mara chache usipende sana ligi na mke au mwanamke wako ukishaongea msimamo wako we endelea na mambo yako mwache aendelee kulalamika au kuongea
 
Kuna hiki kitabu MEN ARE FROM MARS WOMEN ARE FROM VENUS nikijaribu kukiweka kinagoma.....Hakika mwanaume na mwanamke ni watu wawili ambao wametoka katika sayari tofauti, wapo tofautiiii kabisa maisha ya Mars na Venus tofauti kabisa, sasa ndio tumekuja kwenye Earth kuishi pamoja. Unadhani ni rahisi?? Sio rahisi any way kitabu ni kizuri kuna miongozo mizuri sana ya mahusiano, ukikisoma kuna mambo utapata kuyaelewa kwanini mwanamke yupo hivyo alivyo na kwanini mwanaume yupo hivo.

Moja kati ya concepts nilizozipenda na kuzielewa na zimenichekesha "MEN ARE LIKE RUBBER BANDS" "and " WOMEN ARE LIKE WAVES" Unazijua tabia za rubber band?? Unajua tabia za waves?? Kuna mambo ukiyaelewa basi hata kukusumbua inakua ni kidogo mnooo
 
Kuishi na mwanamke hakuna formula inayofanana kwa sababu na wao wanatabia zisizofanana. Kuna wapole, wakorofi, wenye gubu la asili na wapo wale wife material. Cha muhimu omba Mungu akupe anae fanana nawe.

Wanawake wa kizazi hiki cha hali ngumu, jambo kubwa kwa mwanaume ni uwe na kazi inayokuingizia kipato tu. Mwanamke akiwa na uhakika wa mahitaji muhimu wala hutapata shida kuishi nae. Mambo mengine ya kitabia utayoyaona kwake yanatokana na aina ya malezi toka kwa wazazi wake.

Ni muhimu sana Mwanaume kabla ya kuoa, jitahidi upate ABC za maisha ya watu waliomlea huyo binti (Je wazazi wake wanaishi pamoja au waliachana?, Je huyo binti ni mtoto wa mwisho kuzaliwa? huyu utajua alilelewa kwa kudekezwa, Je kwao wamezaliwa kila mtoto ana Baba yake? ni inshu ya muda tu nawe yatakukuta mbele ya safari) Asillimia sabini za tabia mbaya au nzuri za watu waliotulea huwa zinakuja kujirudia kwenye maisha yetu.
 
Hata me nimeona Mkuu embu atuambie jibu lingine la kumpa kama hauna hela 🤨
Wanawake wa sahiv waambie huna hela mara kadhaa kuna mwanaume flani huwa anampa vizawadi na anamtongoza kuwa na uhakika atamkubali

Faida za kutokumpa jibu la moja moja kwa moja ni kushindwa kukosa mfano mim ninaweza nikawa nina hela mwanamke akaniomba hela namwambia kuna kazi nimefanya bado sinapewa hela au wadeni wangu bado hawajanilipa maksudi alafu baada ya mda namtimizia lile hitaji lake by suprise mwisho wa siku anakua hanielewi
Mwanamke ili akupende anatakiwa asipredict your next move ndo wanawake wengi sio wote wanapenda bad boys sababu hawako predictable
 
Kuna hiki kitabu MEN ARE FROM MARS WOMEN ARE FROM VENUS nikijaribu kukiweka kinagoma.....Hakika mwanaume na mwanamke ni watu wawili ambao wametoka katika sayari tofauti, wapo tofautiiii kabisa maisha ya Mars na Venus tofauti kabisa, sasa ndio tumekuja kwenye Earth kuishi pamoja. Unadhani ni rahisi?? Sio rahisi any way kitabu ni kizuri kuna miongozo mizuri sana ya mahusiano, ukikisoma kuna mambo utapata kuyaelewa kwanini mwanamke yupo hivyo alivyo na kwanini mwanaume yupo hivo.

Moja kati ya concepts nilizozipenda na kuzielewa na zimenichekesha "MEN ARE LIKE RUBBER BANDS" "and " WOMEN ARE LIKE WAVES" Unazijua tabia za rubber band?? Unajua tabia za waves?? Kuna mambo ukiyaelewa basi hata kukusumbua inakua ni kidogo mnooo
Ni Kweli kipenz mm pia Huwa nakupenda ninacho ngoja nikiweke hapa
 
Back
Top Bottom