Ushauri: Iundwe Kamati huru kubaini chanzo cha nyufa JNHP maana kuna harufu ya uhujumu uchumi

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,163
22,672
Tumeona Naibu waziri mkuu, Mh Dotto Biteko akifanya ziara katika Bwawa la Mwalimu Nyerere na Kutoa ushauri jinsi ya kuziba nyufa zilizoanza kuonekana kwenye ukuta wa Bwawa.

Haiwezekani kuacha jambo hili lipite hivi hivi bila kufanyika uchunguzi na kuchukua hatua Kali dhidi ya wahusika wote.

Nashauri kamati huru ya Bunge iundwe kuchunguza sakata hili huku wahusika wote wakiwa nje ya ofisi za umma.

Ikiwezekana kamati hiyo huru ihusishe wataalamu Kutoka nje ya Serikali na nje ya nchi kupata UKWELI Ili kupendekeza solution sahihi.

Mkopo hata nusu ya robo haujalipika, na Mwekezaji aliongeza gharama zaidi ya Trilioni 1.5 zaidi ya Gharama halisi alizosaini mkataba na Bado tunaona mapungufu haya hata kabla ya uzalishaji kuanza.

Tusipokuwa serious katika masuala muhimu ya nchi, tukiruhusu kuoneana Aibu, kamwe hatutafanikiwa lolote .

NB: Tunapojadili Mada hii inayogusa maslah mapana ya nchi, tuepuke udini, ubinafsi, uchama nk nk, Uzalendo uwe Dira yetu.

Nawasilisha.🙏

Amen.
 
Wakulaumiwa n I mwendazake, tayaribkylikuwa na dizaini nanilikuwa Wabrazil waanze kulijenga, yeye alivyoingia akabadili mambo kwa kukurupuka na kujimwambafai.

Ni hayo hayo kwa SGR, ilikuwa tayari Wachina waanze kazi.

Lakini kiufundi inarekebIshika vizuro tu, sema gharama na muda wa kumalizika vinaongezeka.

Cheap is expensive.
 
Hakifanyiki chochote kwa vile wanatuona nyani tuh

1694939460086.png
 
Wakulaumiwa n I mwendazake, tayaribkylikuwa na dizaini nanilikuwa Wabrazil waanze kulijenga, yeye alivyoingia akabadili mambo kwa kukurupuka na kujimwambafai.

Ni hayo hayo kwa SGR, ilikuwa tayari Wachina waanze kazi.

Lakini kiufundi inarekebIshika vizuro tu, sema gharama na muda wa kumalizika vinaongezeka.

Cheap is expensive.
Mada inashauri uchunguzi ufanyike kubaini tatizo, haisemi nani alaumiwe Kwa nyufa zilizojitokeza.
 
Back
Top Bottom