Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,869
Leo ndio ilikuwa iwe siku ya mkutano/kongamano la kwanza kati ya matatu kabla ya maandamano yasiyo na kikomo kwa ufadhii wa SAUTI YA WATANZANIA chini ya uratibu wa Wakili Msomi Mwabukusi, Balozi mstaafu Dr. Slaa, mwanaharakati Mdude CHADEMA na timu yao yote
Habari zilizopatikana kutoka Mwanza ni kwamba kongamano hakijafanyika mpaka sasa, polisi wametanda hoteli waliyofikia waratibu na wengine wanarandaranda mitaani
Kwa dalili hizi za leo ni kwamba kuna nguvu kubwa sana inatumika kuzima hayo makongamano na hatimaye maandamano tarajiwa..!
Timu ya waratibu iliyopo pamoja na uthubutu mkubwa waliyo nayo lakini wanahitaji nguvu nyingine kubwa zaidi iliyoko well organized ili kuweza kutimiza lengo ama azma yao inayosubiriwa kwa hamu kubwa na Watanganyika wanaojitambua
Tayari CHADEMA wana platform kubwa, mtandao na vibali vya mikutano mikubwa ya hadhara.. Pamoja na timu kubwa zenye kila kitu
Ushauri wangu: Waratibu hawa waasitishe kwa muda wafanye mawasiliano na CHADEMA wayajenge kisha wakaribishwe kwenye mikutano ya CHADEMA popote itakapokuwa.. Kwakuwa watakuwepo kama wageni basi watapangiwa utaratibu mzuri wa kuweza kufanikisha yale maono yao ambayo hayatofautiani na ya CHADEMA
Ni katika kukaribishwa huko ndio kunaweza kutengenezwa mkakati wa pamoja wa kuliamsha dude maeneo matatu ama matano kwa pamoja kwa ajili ya maandamano yasiyokoma..
Kwa uzoefu na mtandao na mbinu za CHADEMA hili jambo litakuwa kama kumsukuma mlevi! Wakitaka kukomaa wenyewe watachoka na kuishiwa pumzi mapema sana wakati tunawahitaji sana kwenye hii vita