Shiriki maandamo ya amani kwa kufanya yafuatayo

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,929
Tumeshaburuzwa kwa miaka 60, imetosha sasa! Hakuna dalili za kukitoa madarakani chama chawala kupitia sanduku la kura bila shinikizo la maandamo ya amani ambayo yako halali kikatiba CCM wanajiandaa kubaka tena uchaguzi ujao.

Suala la bandari limetupa mwamko na ari mpya kama atanganyika.. Umuhimu wa katiba mpya unaonekana sasa kuliko wakati mwingine wowote. Kilichotokea Ngorongoro tumekiona.

- TEC wamekuja na mwongozo mzuri sana kupitia waraka wao uliosomwa kwa waumini wao wiki sita mfululizo.

- Wakili msomi Mwambukusi na timu yake wameshatoa elimu na ufafanuzi mzuri sana.

- CHADEMA kupitia viongozi wake kwenye mikutano ya hadhara nao wamefanya sehemu yao.

- Mitandao inayojitambua imeruhusu mijadala chanya juu ya hayo mambo mtambuka yaliyotuunganisha watanganyika wote wenye akili timamu.

- Kuna wasemaji mmojammoja na wahamasishaji pia. Kila mmoja kwa nafasi yake ametimiza jukumu lake.

Serikali imepewa muda wa kutosha kujitafakari na kuweza kufanya kile wananchi watakacho. Kuna kila dalili itashupaza shingo
Siku 30 za serikali kusema jambo zinaelekea ukingoni. Maandalizi ya maandamano ya amani kwa mujibu wa katiba yanaendelea vema.

Kwakuwa si kila mmoja wetu ataweza kushiriki maandamano kwa sababu zozote zile kwa kuingia barabarani, bado kuna njia nyingine nyingi tu za kuwa pamoja na watakaoingia barabarani.

1. Kususia usafiri wa umma
Hapa ni muhimu kufanya manunuzi muhimu ili siku hiyo kusiwe na pilika za kutoka na hata wenye magari binafsi kusitisha safari zote.

2. Kususia vinywaji laini na vinywaji yabisi, shurubati, soda, vileo nk.. Siku hiyo sio siku ya kwenda bar

3. Kwa siku husika kutokwenda kwenye ofisi yoyote ya umma kupata huduma yoyote ile

Haya na mengine mengi yakifanyika kwa ufanisi kwa siku 3 tuu hata kama mamalaka zitatumia nguvu kubwa kuyavunja maandamo ya amani. Ujumbe maridhawa utakuwa umefika kunakohusika!

Shiriki mjadala huu kwa kupendekeza njia nyingine zozote zitakazowezesha kufanikiwa kwa maandamano tarajiwa.

Tunaitazamia Tanganyika mpya

014ab9329eb5b0ecf142dcdf7b743548.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumeshaburuzwa kwa miaka 60! Imetosha sasa! Hakuna dalili za kukitoa madarakani chama chawala kupitia sanduku la kura..! Bila shinikizo la maandamo ya amani ambayo yako halali kikatiba ccm wanajiandaa kubaka tena uchaguzi ujao

Suala la bandari limetupa mwamko na ari mpya kama watanganyika.. Umuhimu wa katiba mpya unaonekana sasa kuliko wakati mwingine wowote.. Kilichotokea Ngorongoro tumekiona..

TEC wamekuja na mwongozo mzuri sana kupitia waraka wao uliosomwa kwa waumini wao wiki sita mfululizo
Wakili msomi Mwambukusi na timu yake wameshatoa elimu na ufafanuzi mzuri sana
CHADEMA kupitia viongozi wake kwenye mikutano ya hadhara nao wamefanya sehemu yao
Mitandao inayojitambua imeruhusu mijadala chanya juu ya hayo mambo mtambuka yaliyotuunganisha watanganyika wote wenye akili timamu
Kuna wasemaji mmojammoja na wahamasishaji pia. Kila mmoja kwa nafasi yake ametimiza jukumu lake

Serikali imepewa muda wa kutosha kujitafakari na kuweza kufanya kile wananchi watakacho.. Kuna kila dalili itashupaza shingo
Siku 30 za serikali kusema jambo zinaelekea ukingoni.. Maandalizi ya maandamano ya amani kwa mujibu wa katiba yanaendelea vema

Kwakuwa si kila mmoja wetu ataweza kushiriki maandamano kwa sababu zozote zile kwa kuingia barabarani.. Bado kuna njia nyingine nyingi tu za kuwa pamoja na watakaoingia barabarani
Njia ya kwanza
Kususia usafiri wa umma.. Hapa ni muhimu kufanya manunuzi muhimu ili siku hiyo kusiwe na pilika za kutoka.. Na hata wenye magari binafsi kusitisha safari zote

2.njia y pili
Kususia vinywaji laini na vinywaji yabisi, shurubati, soda, vileo nk.. Siku hiyo sio siku ya kwenda bar

3. Kwa siku husika kutokwenda kwenye ofisi yoyote ya umma kupata huduma yoyote ile
Haya na mengine mengi yakifanyika kwa ufanisi kwa siku 3 tuu hata kama mamalaka zitatumia nguvu kubwa kuyavunja maandamo ya amani.. Ujumbe maridhawa utakuwa umefika kunakohusika!

Shiriki mjadala huu kwa kupendekeza njia nyingine zozote zitakazowezesha kufanikiwa kwa maandamano tarajiwa...!

Tunaitazamia Tanganyika mpyaView attachment 2765060

Sent using Jamii Forums mobile app

Azimio la Umoja style haijawahi kushindwa kuyaleta hata mawe mezani ..
 
Naunga mkono hoja na mawazo yote yaliyotolewa ila sio la kususia safari za baridi kwa siku tatu, hii hapana.
 
Back
Top Bottom