USHAURI: CHADEMA msishiriki uchaguzi mdogo ujao iwapo.....

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,341
2,000
KAMA Rais anawaagiza returning officers wa Tume ya Uchaguzi NEC (maDED) kuwa asisikie DED anamtangaza mpinzani kashinda kwa vile anamlipa mshahara, anampa ulinzi na gari juu.

KAMA viongozi wa CCM wakiwemo wabunge wanawaagiza wafuasi wa CCM kuwafuata wapinzani kuwapiga na kuwakata mapanga huku wakisema polisi ni yao na mahakama ni yao tena mbele ya polisi bila kuchukuliwa hatua zozote.

KAMA polisi anatumika kumpiga na kumbruta nje ya chumba cha kuhesabia kura wakala wa Chadema ili abaki wakala wa CCM pekee.

Na KAMA matokeo yanatangazwa kwa kutumia hesabu zao wanazozipanga wenyewe pamoja na dosari zote kuripotiwa bado NEC inabariki.

Kuna haja gani ya kusumbua wanachama na mashabiki wenu kufanya kampeni huku mkijua hata mshinde hamtatangazwa washindi?

Kuna chaguzi ndogo zinakuja za Wabunge majimbo ya Longido, Singida Magharibi na Songea Mjini, najua kabla kutakuwa na mikutano kati yenu na NEC, wapinzani (CHADEMA) waje na RESOLUTION moja ya kuwakataa maDED kuwa returning officers huku mkijenga hoja yenu kutokana na kauli ya rais.

IWAPO NEC itakataa ushauri huo, kuliko kupeleka watu wakavunjwe miguu na polisi, wakadhalilishwe pengine kuuawa. Mimi nashauri huku nikijua kabisa faida na hasara za kususia uchaguzi, tumejifunza kwa CUF ya Maalimu Seif na juzi tumejifunza kwa NASA ya Raila Odinga, bora mjitoe kwenye uchaguzi huu, ili muanze mikakati mipya ya kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na matukio hayo mapema kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019.

Mengi yatasemwa, ila najua watu watawaelewa kuwa mmeepusha maafa kama yaliyotokea kwenye uchaguzi uliopita wa Madiwani, na vile vile mtakuwa mmepeleka 'clear message' kwa watawala na mataifa kuwa kinachofanyika Tanzania sio uchaguzi bali ni mfumo wa kudanganya watu na mataifa yadhani kuwa wako madarakani kihalali na wamechaguliwa na wananchi.
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
51,727
2,000
Hata uchaguzi mkubwa wasishiriki pia maana tushaona Mfano kwenye chaguzi za udiwani kuna watu wamekuwa vilema,wametekwa,wameumizwa n.k
Sasa uchaguzi mkuu si ndiyo itakuwa balaaa

Ova
 
laki si pesa.

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
10,017
2,000
uchaguzi watashiriki na baada ya uchaguzi wataendelea kulalamika kuibiwa kura....Nyalandu ameshatoa fungu kwa CHADEMA hawezi kukubali asigombee ubunge.....CHADEMA wapo kimaslahi zaidi
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,435
2,000
Iwapo cdm wataingia kwenye uchaguzi wowote na mapanga, sime, bunduki nk hapo sawa. Ila eti wao wanauza sera na ushawishi wa kisiasa, ccm wao wanatumia silaha na ukatili wa kutisha achia mbali kulazimisha kutangazwa washindi. Tumeshafahamu na ushahidi upo wazi kwamba ccm haiwezi siasa bali inatumia jeshi kutawala nchi.

Ile kupokea madiwani kwenye hafla ya jeshi ilikuwa ni ushahidi tosha wa hilo. Acha ccm ibaki yenyewe, wananchi wasusie kwa wingi kupiga kura. Hapo wataamua wenyewe washindane kikabila, kikanda na kidini. Halafu huo upuuzi ukishika kasi jeshi nalo litajiingiza kushika madaraka maana nalo litajua taratibu hazifuatwi. Kwenye uamuzi huu tusisikie eti vionngozi wa dini walishauri. Mpaka sasa watu wanauliwa na unyama wote wako kimya.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
26,816
2,000
Ushauri waliompa kenyatta kuwa asijali ODINGA aliyesusa uchaguzi aendelee .Tanzania tutauzingatia.Ushauri waliompa kenyatta na kumtia moyo kuwa aendelee na uchaguzi asimjali raila na uchaguzi ukafanyika akashinda kwa kishindo na wakaenda akina LOwasa kenya kumpongeza.Hakuna tatizo.Wasuse tu no harm precedence ya kenya CCM tutaitumia.Na tutashinda kwa kishindo kama kenyatta alivyoshinda
 
Mnajitekenya wenyewe halafu mnacheka, uchaguzi unakuwa kama vita vya Kagera safari hii nendeni wenyewe vitani.
 
MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,542
2,000
Ushauri waliompa kenyatta kuwa asijali ODINGA aliyesusa uchaguzi aendelee .Tanzania tutauzingatia.Ushauri waliompa kenyatta na kumtia moyo kuwa aendelee na uchaguzi asimjali raila na uchaguzi ukafanyika akashinda kwa kishindo na wakaenda akina LOwasa kenya kumpongeza.Hakuna tatizo.Wasuse tu no harm precedence ya kenya CCM tutaitumia.Na tutashinda kwa kishindo kama kenyatta alivyoshinda
Kuwa na akili kidogo. Raila alipewa ushindi na mahakama lkn bado akakimbia na kutia watu barabarani wakauawa.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,435
2,000
Chadema wakisusa cuf ya lipumba itashiriki

Zitto na timu yake watashiriki hapo ndo utajua wapinzani wana adui ndani ya upinzani

Hata kingeanzishwa chama kingine cha upinzani kikashiriki ni haki yake, ila kushiriki huku wafuasi na viongozi wako wakikatwa mapanga na bado unaporwa ushondi huku umma ukiwa unaogopa kukemea ni kupoteza muda. Huo sio uchaguzi wa kisiasa bali maujai kuhalalisha kupewa misaada na wazungu. Tunaweza kufanya siasa za upinzani bila kupitia vyama vya siasa
 
Mndali ndanyelakakomu

JF-Expert Member
Dec 14, 2016
13,050
2,000
Hata kingeanzishwa chama kingine cha upinzani kikashiriki ni haki yake, ila kushiriki huku wafuasi na viongozi wako wakikatwa mapanga na bado unaporwa ushondi huku umma ukiwa unaogopa kukemea ni kupoteza muda. Huo sio uchaguzi wa kisiasa bali maujai kuhalalisha kupewa misaada na wazungu. Tunaweza kufanya siasa za upinzani bila kupitia vyama vya siasa
Tusubiri ushauri ukipokelewa
 
Tairi bovu

JF-Expert Member
Sep 28, 2017
3,067
2,000
uchaguzi watashiriki na baada ya uchaguzi wataendelea kulalamika kuibiwa kura....Nyalandu ameshatoa fungu kwa CHADEMA hawezi kukubali asigombee ubunge.....CHADEMA wapo kimaslahi zaidi
Akili nyingine bwana yani nyalandu aache ubunge kisha nyalandu atoe pesa/fungu kwa chadema ili agombee tena ubunge!? Kweli tanzania kuna shida kubwa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom