Ushauri: Badala ya tozo kuelekezwa kusikojulikana, tozo hizo zielekezwe kwenye matibabu bure kwa kila Mtanzania

Paulsylvester

JF-Expert Member
Oct 15, 2021
1,467
3,381
Tanzania Salaam,

Nchi yetu sio masikini, Bali wananchi mmojammoja ndio masikini! Na umasikini huo unaweza kuchangiwa na vitu vingi, ni pamoja na kutokuwa na viongozi wenye maono! Viongozi waliodumaa kiakili, huduma mbovu wazipatazo wananchi licha kwamba kodi wanatozwa kila wakilala na kuamka!

Tunaposema kwamba nchi yetu ni tajiri, tunamaana ya Rasilimali watu wapo, resources nyingi katika aridhi yetu, shida tu ni kukosa viongozi wenye uchungu na wivu wa nchi yao, badala yake tunapata viongozi wenye umimi kwanza! Na ndiyo maana ukifuatilia, koo za viongozi wetu, wote wana utajiri Mkubwa na ukiangalia utakuta ni watu wawili au watatu tuu ndio wamewahi kushika nyadhifa za juu huko serikalini katika ukoo huo, cha ajabu, watu hao wachache wamekuwa sababu ya utajiri wa ukoo wenye idadi ya watu zaidi ya mia moja

Tukuje kwenye mantiki ya lengo langu,

Katika taqwim za serikali zinasema, wananchi wa nchi hii, wengi wanakipato cha chini ya dollar 1 Kwa siku, maana yake mwananchi kama Huyo, hawezi kujimudu linapokuja suala la matibabu, Kwa bili zinazokuwa zinatolewa pale mhimbili na hospital zingine nchini, thubutuu, na matokea yake, wananchi kama hawa, hulazimika kurudi kwenye umasikini uliopitiliza baada ya Kutoka kwenye matibabu hayo yenye ghali, na si hivyo tuu, Bali pia tumepoteza wananchi wengi Kwa kukosa tu pesa ya matibabu!

Lakini Kwa nini tuendelee kuwa nchi isiyojali wananchi wake?

Serikali kupitia wizara ya Afya, na Kwa wananchi wote Tanzania, mambo ya Tozo, ni bora sasa ndo iwe ni pesa inayoingia moja Kwa moja kwenye kumwezesha mwananchi kupata matibabu bule popote pale alipo!

Kama kwenye mafuta kuliongezwa tozo ya mia, wafanye hivyo hata kwenye manunuzi ya Luku, kila mwananchi akinunua Luku, 50 iwe tozo Kwa ajili ya matibabu, vivyo hivyo kwenye ving'amzi, kwenye mabank, kwenye mitandao n.k

Hapo hatutauliza tozo zetu huwa zinakwenda wapi na zimefanya kazi gani! Katika hili, Nani atalalamika!?

Matibabu imekuwa ni sehemu ya mwananchi kwenda, akirudi tayari keshakuwa masikini wa kutupwa!

Lakini pia, Kwa niini gharama za matibabu ni ghali kiasi hiko na wakati kila mwaka kunatengwa bajeti ya kuingizwa huko, ununuzi wa dawa na vifaa Tiba?

Huu ughali wa huduma, hizo fedha zinazotokana na makusanyo Kwa wagonjwa, huwa zinakwenda wapi?

Paulsylvester, Niko shamba naendeleza mapambano ya maisha, maisha ya mjini yalinishinda toka mwaka Jana!

Mungu akipenda niwe Rais wa nchi hii, mpaka sasa kunawanaostahili kunyongwa peupe pee,

JPM atakuwa cha mtoto!

Muwe na siku njema
 
Ila hii nchi! Yaani kusanyo la kwanza likatangazwa kabisa na mbwembwe nyingi baada ya hapo kimyaaa. Ila wanajua akili zetu acha watupige tu
 
Huwenda Watanzania tuko imara sana kwenye umbea na majungu kuliko kwenye mambo mhimu na ya maendeleo
 
Back
Top Bottom