Ushauri: Anataka nihamie kwake alafu ndoa tufunge baadae

Ushauri: Anataka nihamie kwake alafu ndoa tufunge baadae

Ujinga wakati wa kwenda, now unaporudi tumia akili
Wazungu wana sema

Fool me once, shame on you; fool me twice, shame on me.
Dont be fool again.
Hebu fuatilia mikasa ya huyu bibie kisha ujiulize kama anafaa kushauriwa kumrudia huyo jamaa.
 
Wanaume wanaume... Afu mm najiulzaga iv unafklia nn kumchukua mtoto wa m2 uish nae hata wazaz wake hawajui akiumwa au kufa utafanyaje....
Anakufukia kwenye shimoo
 
Hebu fuatilia mikasa ya huyu bibie kisha ujiulize kama anafaa kushauriwa kumrudia huyo jamaa.
Asante Azarel kwa kutufungua...

Jamaa hampendi asee, halafu mtiririko wa matukio upo vizuri kwahiyo haongopi

Jamani huyu Dada namuonea tuu hurumaa...
 
Asante Azarel kwa kutufungua...

Jamaa hampendi asee, halafu mtiririko was matukio upo vizuri kwahiyo haongopi

Jamani huyu Dada namuonea tuu hurumaa...
Huyu binti sio muongo ila nlichogundua ni kwamba, yeye anampenda sana huyo Mwanaume ila Mwanaume hana Malengo naye.

Iko hivyo.
 
Za muda huu wapendwa poleni na majukumu,
Naomben ushauri wenu,

Nina mzazi mwenzangu tumezaa mtoto 1 kipindi cha uchumba alinitolea mahari ilibaki ndoa tu, badae kumbe nilikuja kugundua katupa mimba wanawake 2 kwa wakati 1, ikazua maneno na kupelekea kutoishi pamoja,

Alinifanyia visa vingi sana ikiwemo kunitukana, dharau in short mengi ya kuumiza moyo. tunaishi mikoa tofauti huwa tunawasiliana kwa ajili ya matumizi ya mtoto na hua anatoa kila mwezi kulingana na kipato chake.

Kinachonifanya niombe ushauri ni kama wiki hivi imepita kaniambia nimechoka kukaa mwenyewe haya maisha ya kutangatanga yamenichosha, nataka tuishi pamoja kwa vile mimi kwanza sikuwa na mahusiano na mtu, pili kuitwa single mother huwa inaniuma sana maana sikupenda ikabidi nikubali na kufuta yote mabaya aliyonifanyia.

Nilimwambia nina plan ya kufungua biashara huku nilipo kaniambia niache twende tukafungue pamoja na yeye huko alipo yaani na yeye aongezee mtaji tufungue kitu kikubwa, mimi nimemwambia tufanye kwanza process za ndoa ndio niende anadai kwa sasa hela haitoshi tukakae kwanza uchumi ukishakaa sawa tutaanza mchakato.

Kinachonipa mawazo namwambia njoo nyumbani uwaambie wazazi kuhusu mimi kuhamia huko anadai nisiwaambie wazazi kama tunaenda kuishi pamoja niage tu nimepata sehemu ya biashara huko,

Nilipoonekana kulipinga hilo akasema basi nipigie simu mama yako nimuombe uje na mtoto huku, baadae uchumi ukikaa sawa tutafunga ndoa. Nipo njiapanda ninapenda kuishi na baba mtoto ila naogopa asije nigeuka kama mwanzo nashindwa niamue nn kwa sasa nipo dilemma
Naombeni mawazo yenu wapendwa.

NB; Hali yake kiuchumi sasa hivi sio nzuri mshahara mdogo, watoto 3 kila mmoja na mama na wote kila mwezi anatuma matumizi, inampa mawazo sana nashindwa kuelewa kweli kaamua kwa moyo 1 au maisha yamemchanganya tu.
Nenda lkn usikubali kubeba mimba nyingine kabla ya ndoa, ukiachia tu umekwisha. Na hakikisha hiyo biashara inaonesha umilki wa wote wawili
 
Mi nawashangaa sana watu wanaoachana halafu baadae wanarudiana,,, unaachanaje na MTU halaf mrudiane?? Ni akil yenu kwel au upofu? Michana kwa kipi na kipi kinawarudisha? Mahusiano kila Mara tunaeleweshana hapa yakishaingiliwa na watu wa pemben hata kuweka vikao tu yameshakufa hayo,,,, na mnaogopa sababu MNA mtoto unadhan mtoto nyie ndio mnampa maisha? Au mnadhan mnaishi kwa niaba yake?mtoto ana maisha yake,wewe una maisha yako na yy ana maisha yake,hakuna MTU anaeeza kuwaynganisha kama lilishatikea tatizo,,, usimrudie,Kata mawasiliano nae,mlee mtoto mwenyewe,,,unaweza maana ulishajiandaa kwa ajili ya mtoto ndio maana ulimtunza miez Tisa... Mteme kabsa hakufai na wala ww humfai
Kuachana na kurudiana inawezekana kabisa. Kinachoweza kuamua mrudiane au msirudiane, ni uzito wa sababu ya kuachana. Trust me, watu wengi wameoa/wameolewa na ma-ex wao. Hata humu JF wapo wengi tu.
 
Sidhani kama anahitaji ushauri. Sababu anayemjua ni yeye na tayari anajua changamoto zilizoko hata kabla haya hajaileta hapa. Na pia yeye ndiye muamuazi wa mwisho.kama anapinga hapa maoni ya watu sasa ni msaada gani anaoutaka?
 
Kwanini hataki kwenda kwa wazazi wako kuweka mambo sawa?,hapo ni kwa kutilia mashaka..
 
Ukweli mchungu huu


Walai ukienda kwa huyo mwanaume nitakushangaa sana!

Ni kweli kuna exceptions kama ya iryn lakini hii ya kwako ni wazi huyo mtu hana mpango na wewe!

Aisee my dear, ni kweli kuwa single mother kama hukupanga iwe hivyo inauma na inakera, lakini ni mara mia afadhali kuliko huko unakotaka kwenda!
 
Single mother wewe hujifunzi kabisa. Mwanaume aliyekutapeli na kuzalisha mwanamke mwingine. Halafu anakwambia usifungue biashara yako ukakae naye tena bila ndoa. Mtaji wako umpe. Kesho si atakufukuza na malboro yako. Huu ni ujinga wa kiwango cha PhD. Chembilecho huko shuleni huwa mwaenda kusomea ujinga?

Nilimwambia ninaplan ya kufungua biashara huku nilipokaniambia niache twende tukafungue pamoja na yeye huko alipo yaani na yeye aongezee mtaji tufungue kitu kikubwa, mimi nimemwambia tufanye kwanza process za ndoa ndio niende anadai kwa sasa hela haitoshi tukakae kwanza uchumi ukishakaa sawa tutaanza mchakato.
 
Mdogo wangu usikubali kwenda bila taarifa husika, alishatoa mahari, hivyo anafahamika.

Kama ana nia nzuri aje ajieleze kwa wazee aombe hilo analokuomba wewe, na wakikubali nenda, usikubali mawasiliano yafanyike kwa njia ya simu.

BTW, yule mzazi mwenzake yuko wapi?

Naziona dalili za kutaka kukabeba kamtaji kako atokomee nako.

Sijaelewa kwa wazazi akafuate nini tena. Alishatuma mshenga, akaposa, akatajiwa mahari na akalipa...kimila hapo keshakabidhiwa binti, zimebaki taratibu tu za kidini na kisheria ambazo ni maamuzi ya ninyi wawili, sio wazazi...maana alishamalizana nao!

Cha muhimu ni mhusika kuamua, kama bado anampenda mchumba/baba watoto wake na amekubaliana na hali yake (kiuchumi and the fact that ana watoto wengine wa2 kwa mama wa2 tofauti) aende wakaishi wajenge maisha. Kama hajakubaliana na hiyo hali awe muwazi kwa mzazi mwenzie, na sio kujificha kwenye kivuli cha wazazi.
 
Hilo hapana namfaham ni mtu wa aina gani?
Ungekuwa wamfahamu ni mtu wa namna gani basi usingeshangaa kujua kuwa wenye mimba mko wawili.
Ungekuwa wamfahamu mtu wa namna gani usingekuja kuomba ushauri maana majibu yote ungekuwa nayo maana unamfahamu ni mtu wa namna gani
 
Single mother wewe hujifunzi kabisa. Mwanaume aliyekutapeli na kuzalisha mwanamke mwingine. Halafu anakwambia usifungue biashara yako ukakae naye tena bila ndoa. Mtaji wako umpe. Kesho si atakufukuza na malboro yako. Huu ni ujinga wa kiwango cha PhD. Chembilecho huko shuleni huwa mwaenda kusomea ujinga?
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] mbona chombilecho
 
Kuachana na kurudiana inawezekana kabisa. Kinachoweza kuamua mrudiane au msirudiane, ni uzito wa sababu ya kuachana. Trust me, watu wengi wameoa/wameolewa na ma-ex wao. Hata humu JF wapo wengi tu.
Hamuwez kua sawa mkirudiana,mtaishi kwa mashaka kila wakati,hakuna sababu inayowafanya muachane then kuwe na sababu nyingine za kurudiana... Kwan nn mwanzo na kwann sasa? Kiufupi siwapangii watu Ila mi siwez maana haina maana nya kuachana kama mtakuja kurudiana
 
Angalia vizuri motive ya huyo jamaa kabla hujaenda,maana unasema ana watoto watatu na kila mtoto na mama yake,sasa hao akina mama wengine wako wapi?Na kwanini alilipa mahari na akakubali kuachana na wewe?Je kiafya sasa hivi yuko sawa?
 
Back
Top Bottom