Ushauri: Anataka nihamie kwake alafu ndoa tufunge baadae

Ushauri: Anataka nihamie kwake alafu ndoa tufunge baadae

Za muda huu wapendwa polen na majukum
Naomben ushaur wenu,,,
Nina mzazi mwenzangu tumezaa mtoto 1.. Kipindi cha uchumba alinitolea mahari ilibaki ndoa tu,, badae kumbe nilikuja kugundua katupa mimba wanawake 2 kwa wakati 1,,,, ikazua maneno na kupelekea kutoishi pamoja,,,alinifanyia visa vingi sana ikiwemo kunitukana,,,,dharau in short mengi ya kuumiza moyo
Tunaishi mikoa tofauti huwa tunawasiliana kwa ajir ya matumizi ya mtoto na hua anatoa kila mwezi kulingana na kipato chake
Kinachonifanya niombe ushauri
Kama wiki hv imepita kaniambia jack nimechoka kukaa mwenyewe haya maisha ya kutangatanga yamenichosha nataka tuishi pamoja kwa vile Mimi kwanza sikua na mahusiano na mtu,,, pili kuitwa single mother hua inaniuma sana maana sikupenda ikabidi nikubali nakufuta yote mabaya alonifanyia....
Nilimwambia ninaplan ya kufungua biashara huku nilipo kaniambia niache twende tukafungue pamoja na yeye huko alipo yaan na yeye aongezee mtaji tufungue kitu kikubwa,, ,
Mimi nimemwambia tufanye kwanza process za ndoa ndio niende anadai kwa sasa hela haitoshi tukakae kwanza uchumi ukishakaa sawa tutaanza mchakato
Kinachonipa mawazo namwambia njoo nyumban uwaambie wazazi kuhusu Mimi kuhamia huko,,anadai nisiwaambie wazazi kama tunaenda kuishi pamoja niage tu nimepata sehem ya biashara huko,, nilipoonekana kulipinga hilo akasema basi Nipigie cm mama yako nimuombe uje na mtoto huku ,,badae uchum ukikaa sawa tutafunga ndoa
Nipo njia panda ninapenda kuishi na baba mtoto ila naogopa asije nigeuka kama mwanzo nashindwa niamue nn kwa sasa nipo dilemma
Naomben mawazo yenu wapendwa

NB,,hali yake kiuchumi sasa hv sio nzuri mshahara mdogo,,watoto 3 kila mmoja na mama na wote kila mwezi anatuma matumizi ,,,inampa mawazo sana nashindwa kuelewa kweli kaamua kwa moyo 1 au maisha yamemchanganya tu

Pole dada. Kuna maneno ya kwamba hata nyumba umeiona. Na biashara utaendesha wewe. Naona kama una majibu tayari. Lakini umesahau kuwa umesema mwenyewe alikutukana na dharau juu. So pamoja na upendo wako mkubwa na pamoja na kisingizio hupendi kuishi peke yako ,je unadhani alipokutukana na kukufharau alikuwa amelewa --je wewe unakubali kuingia kwenye maisha ya dhambi bila ndoa kisa yeye amechoka. UPENDO NDO IWE SABABU YA KUINGIA KWENU TENA KWENYE MAHUSIANO---sio kingine. Na nyie wanawake mnapenda sana sherehe mwambie mfunge ndoa. Hata bila sherehe kwa kuwa hana hela. DADA USISAHAU KABISA MATUSI NA DHARAU ALIZOKUAGA NAZO UTAJUTA
 
Pole dada. Kuna maneno ya kwamba hata nyumba umeiona. Na biashara utaendesha wewe. Naona kama una majibu tayari. Lakini umesahau kuwa umesema mwenyewe alikutukana na dharau juu. So pamoja na upendo wako mkubwa na pamoja na kisingizio hupendi kuishi peke yako ,je unadhani alipokutukana na kukufharau alikuwa amelewa --je wewe unakubali kuingia kwenye maisha ya dhambi bila ndoa kisa yeye amechoka. UPENDO NDO IWE SABABU YA KUINGIA KWENU TENA KWENYE MAHUSIANO---sio kingine. Na nyie wanawake mnapenda sana sherehe mwambie mfunge ndoa. Hata bila sherehe kwa kuwa hana hela. DADA USISAHAU KABISA MATUSI NA DHARAU ALIZOKUAGA NAZO UTAJUTA
Sipendi sherehe ndugu Mimi nimepita huo umri wa kupenda sherehe mi nilimwambia hata kwenda tu kanisani kubariki inatosha,,,bt dharau alinifanyia kubwa mpaka kuongea na wanawake zake mbele yangu
 
Mimi nisingerudi bila ndoa. Si lazima sherehe ila kuishi kienyeji tena after matusi na mimba kwa watu wengine, no way. You can't trust such a person as easy as that anymore.
Na hata hio ndoa aise hapana nahisi atamnyanyasa sana tena sana. Halaafu pia jamaa lengo la kumpigia kuomba waishi wote sio kwamba anampenda lakin just ameona kua yuko single, and blah blah lakin sijasikia nataka urudi sabaabu nakupenda bado na natakaa tufunge ndoa ..sijasikia hio statement, kama hamna hio statement hapo hamna kitu.
 
Kufunga ndoa haina gharama kabisa. Sana sana ni gharama ya kile cheti cha ndoa tu.
 
unapewa ushauri ila bado unabishia mawazo ya watoa ushauri haya nenda kwa huyo bwana wako ila usisahau kutupa mrejesho
 
I'll

Ilo hapana namfaham ni mtu wa aina gani?

Kama unamfahamu na tayari unaonekana uko interested kwenda kuishi nae unaomba ushauri wa nini? Unadhani wenzio waliozaa nae hawataki watoto waishi na baba yao km wewe,?
NEVER EVER speak for someone, unaeza sema Hapana, akaku surprise na Ndio. Hata akikuoa chances ni, atacheat kwa sana tu.
 
Cha muhimu dada hapo ni kujiongeza kimawazo,lazima ujue uwezo wako wa kipato wa wakati mpo wote na sasa upoje,kama umeongezeka na jamaa hali imemzidi bas jua hyo ni janga la njaa limemfika na cyo mapenz,ila icho cyo kipimo cha mwisho mwambie aje nyumbani hawaombe wakwe zake msamaha than ikiwezekana mkaanzishe maisha pengine tofaut na alipokua yy.
 
Mi nawashangaa sana watu wanaoachana halafu baadae wanarudiana,,, unaachanaje na MTU halaf mrudiane?? Ni akil yenu kwel au upofu? Michana kwa kipi na kipi kinawarudisha? Mahusiano kila Mara tunaeleweshana hapa yakishaingiliwa na watu wa pemben hata kuweka vikao tu yameshakufa hayo,,,, na mnaogopa sababu MNA mtoto unadhan mtoto nyie ndio mnampa maisha? Au mnadhan mnaishi kwa niaba yake?mtoto ana maisha yake,wewe una maisha yako na yy ana maisha yake,hakuna MTU anaeeza kuwaynganisha kama lilishatikea tatizo,,, usimrudie,Kata mawasiliano nae,mlee mtoto mwenyewe,,,unaweza maana ulishajiandaa kwa ajili ya mtoto ndio maana ulimtunza miez Tisa... Mteme kabsa hakufai na wala ww humfai
 
wewe hapa unatafuta cover tuuu.....una habari kuhusu wale wenzio waliodunguliwa kama wewe???? je uko tayari kuwa mke mwenza?? uko tayari kulea mwana wa mwenzio???? eti kuitwa sigle mama kunakuumiza!!!! wewe kuna kitu unatafuta....mfuate tu.........kwani akiwaambia wazazi wako ndo kigezo cha kutokukutesa???? cheza karata vizuri dada...
 
"anadai nisiwaambie wazazi kama tunaenda kuishi pamoja niage tu nimepata sehem ya biashara huko,, nilipoonekana kulipinga hilo akasema basi Nipigie cm mama yako nimuombe uje na mtoto huku"

VITU VINGINE MNAJITAKIAGA NA VYA WAZIWAZI TU
 
Wakati mwingine masuala ya mahusiano hayahitaji ushauri.. Inafika wakati MTU anaamua kulingana na jinsi moyo moyo wake unavyomuelekeza.
Wapo wanaofanikiwa na wapo wanaoharibikiwa kabisa..

Speaking from my personal experience, Nina kesi kama yako.. Nilizaa na mwanaume ambaye wakati wa ujauzito alini mistreat kweli kiasi kwamba nikajipa moyo na kuamua kulea mimba na mtoto peke yangu. Watu walioijua story yangu hakuna hata mmoja aliyetamani kuona kwamba itatokea siku yule baba anisalimie wala ashike mwanangu.

We stayed apart for four good years lakini baada ya muda huo alirudi kwa style hiyo hiyo. Mama yangu akasema usithubutu kumchekea.. (But I loved him..) Kwa kuwa nilikuwa mbali na nyumbani nilirudiana naye kwa siri na Ni miaka mitatu sasa since tumerudiana.

Alipoona wakati unamfaa alikwenda mwenyewe kwa wazazi wangu kujieleza na kuomba radhi na tuna mtoto wa pili sasa .. Hatujawahi tena kugombana..
Sometimes mambo haya hayako uniform I hope. Dada wewe ndyo unamjua vizuri MTU wako zaidi ya sisi wachangiaji. Usikilize moyo wako lile linalokupa Amani lifanye
 
Back
Top Bottom