Ushauri: Anataka nihamie kwake alafu ndoa tufunge baadae

jack 1

Member
Oct 28, 2012
61
63
Za muda huu wapendwa poleni na majukumu,
Naomben ushauri wenu,

Nina mzazi mwenzangu tumezaa mtoto 1 kipindi cha uchumba alinitolea mahari ilibaki ndoa tu, badae kumbe nilikuja kugundua katupa mimba wanawake 2 kwa wakati 1, ikazua maneno na kupelekea kutoishi pamoja,

Alinifanyia visa vingi sana ikiwemo kunitukana, dharau in short mengi ya kuumiza moyo. tunaishi mikoa tofauti huwa tunawasiliana kwa ajili ya matumizi ya mtoto na hua anatoa kila mwezi kulingana na kipato chake.

Kinachonifanya niombe ushauri ni kama wiki hivi imepita kaniambia nimechoka kukaa mwenyewe haya maisha ya kutangatanga yamenichosha, nataka tuishi pamoja kwa vile mimi kwanza sikuwa na mahusiano na mtu, pili kuitwa single mother huwa inaniuma sana maana sikupenda ikabidi nikubali na kufuta yote mabaya aliyonifanyia.

Nilimwambia nina plan ya kufungua biashara huku nilipo kaniambia niache twende tukafungue pamoja na yeye huko alipo yaani na yeye aongezee mtaji tufungue kitu kikubwa, mimi nimemwambia tufanye kwanza process za ndoa ndio niende anadai kwa sasa hela haitoshi tukakae kwanza uchumi ukishakaa sawa tutaanza mchakato.

Kinachonipa mawazo namwambia njoo nyumbani uwaambie wazazi kuhusu mimi kuhamia huko anadai nisiwaambie wazazi kama tunaenda kuishi pamoja niage tu nimepata sehemu ya biashara huko,

Nilipoonekana kulipinga hilo akasema basi nipigie simu mama yako nimuombe uje na mtoto huku, baadae uchumi ukikaa sawa tutafunga ndoa. Nipo njiapanda ninapenda kuishi na baba mtoto ila naogopa asije nigeuka kama mwanzo nashindwa niamue nn kwa sasa nipo dilemma
Naombeni mawazo yenu wapendwa.

NB; Hali yake kiuchumi sasa hivi sio nzuri mshahara mdogo, watoto 3 kila mmoja na mama na wote kila mwezi anatuma matumizi, inampa mawazo sana nashindwa kuelewa kweli kaamua kwa moyo 1 au maisha yamemchanganya tu.
 
Kinachonipa mawazo namwambia njoo nyumban uwaambie wazazi kuhusu Mimi kuhamia huko,,anadai nisiwaambie wazazi kama tunaenda kuishi pamoja niage tu nimepata sehem ya biashara huko

Mdogo wangu usikubali kwenda bila taarifa husika, alishatoa mahari, hivyo anafahamika.

Kama ana nia nzuri aje ajieleze kwa wazee aombe hilo analokuomba wewe, na wakikubali nenda, usikubali mawasiliano yafanyike kwa njia ya simu.

BTW, yule mzazi mwenzake yuko wapi?

Naziona dalili za kutaka kukabeba kamtaji kako atokomee nako.
 
Mdogo wangu usikubali kwenda bila taarifa husika, alishatoa mahari, hivyo anafahamika.

Kama ana nia nzuri aje ajieleze kwa wazee aombe hilo analokuomba wewe, na wakikubali nenda, usikubali mawasiliano yafanyike kwa njia ya simu.

BTW, yule mzazi mwenzake yuko wapi?

Naziona dalili za kutaka kukabeba kamtaji kako atokomee nako.
Kubeba sizani maana biashara ni dispensary na nilishaona Nyumba tukaongea na mama mwenyewe Nyumba yeye ni muajiriwa serikalin kwa hiyo muda mwingi nitakua nakaa mimi
 
Kubeba sizani maana biashara ni dispensary na nilishaona Nyumba tukaongea na mama mwenyewe Nyumba yeye ni muajiriwa serikalin kwa hiyo muda mwingi nitakua nakaa mimi

Basi kuwa makini sana, maswala ya mapenzi ni ngumu sana sisi wa pembeni kushauri tukasikilizwa, maana mlivyopeana mnajua wenyewe, ila kwa kifupi huyo mwanaume atakuumiza tena.

Kama unaweza kufanya biashara zako vizuri na ukalea mtoto bila shida ungeachana naye ukaendelea na maisha yako, utapata mwanaume atakaye kuthamini, ila huyo anacheza na fursa za kusikia una mtaji.
 
Mdogo wangu usikubali kwenda bila taarifa husika, alishatoa mahari, hivyo anafahamika.

Kama ana nia nzuri aje ajieleze kwa wazee aombe hilo analokuomba wewe, na wakikubali nenda, usikubali mawasiliano yafanyike kwa njia ya simu.

BTW, yule mzazi mwenzake yuko wapi?

Naziona dalili za kutaka kukabeba kamtaji kako atokomee nako.
Nafikiri hiyo ndio point ya msingi, kwanini aogope kuja kwenu na mahari kaishatoa. There's something behind the scene
 
Ujinga wakati wa kwenda, now unaporudi tumia akili
Wazungu wana sema

Fool me once, shame on you; fool me twice, shame on me.
Dont be fool again.
 
Za muda huu wapendwa polen na majukum
Naomben ushaur wenu,,,
Nina mzazi mwenzangu tumezaa mtoto 1.. Kipindi cha uchumba alinitolea mahari ilibaki ndoa tu,, badae kumbe nilikuja kugundua katupa mimba wanawake 2 kwa wakati 1,,,, ikazua maneno na kupelekea kutoishi pamoja,,,alinifanyia visa vingi sana ikiwemo kunitukana,,,,dharau in short mengi ya kuumiza moyo
Tunaishi mikoa tofauti huwa tunawasiliana kwa ajir ya matumizi ya mtoto na hua anatoa kila mwezi kulingana na kipato chake
Kinachonifanya niombe ushauri
Kama wiki hv imepita kaniambia jack nimechoka kukaa mwenyewe haya maisha ya kutangatanga yamenichosha nataka tuishi pamoja kwa vile Mimi kwanza sikua na mahusiano na mtu,,, pili kuitwa single mother hua inaniuma sana maana sikupenda ikabidi nikubali nakufuta yote mabaya alonifanyia....
Nilimwambia ninaplan ya kufungua biashara huku nilipo kaniambia niache twende tukafungue pamoja na yeye huko alipo yaan na yeye aongezee mtaji tufungue kitu kikubwa,, ,
Mimi nimemwambia tufanye kwanza process za ndoa ndio niende anadai kwa sasa hela haitoshi tukakae kwanza uchumi ukishakaa sawa tutaanza mchakato
Kinachonipa mawazo namwambia njoo nyumban uwaambie wazazi kuhusu Mimi kuhamia huko,,anadai nisiwaambie wazazi kama tunaenda kuishi pamoja niage tu nimepata sehem ya biashara huko,, nilipoonekana kulipinga hilo akasema basi Nipigie cm mama yako nimuombe uje na mtoto huku ,,badae uchum ukikaa sawa tutafunga ndoa
Nipo njia panda ninapenda kuishi na baba mtoto ila naogopa asije nigeuka kama mwanzo nashindwa niamue nn kwa sasa nipo dilemma
Naomben mawazo yenu wapendwa

NB,,hali yake kiuchumi sasa hv sio nzuri mshahara mdogo,,watoto 3 kila mmoja na mama na wote kila mwezi anatuma matumizi ,,,inampa mawazo sana nashindwa kuelewa kweli kaamua kwa moyo 1 au maisha yamemchanganya tu
Naona kamtaji kako kanaviziwa hapo...

Asipige simu mwambie apeleke miguu mpaka home na awaombe msamaha wazazi
 
Magufuli kamnyoosha huyo.. Jeuri ya pesa imemfanya akukumbuke, wengine sio wavumilivu, wamemkimbia. Kaokoe Jahazi linazama
 
kweli nimeamini roho y huruma mnayo kina mama jamani,na kwa nini hataki kuskia mipango ya ndoa?, then vipi amekusisitiza kuhusu mtoto, kuwa makini naye kila step unayopiga lazima umshirikiShe mzazi wako
 
Back
Top Bottom