Ushauri: Anataka nihamie kwake alafu ndoa tufunge baadae

Ushauri: Anataka nihamie kwake alafu ndoa tufunge baadae

Usijaribu kwenda biashara yako inaenda kuwatunza matoto anaozaa zao ovyo. Na vile amina ana mimba yake? Hata kwa ndoa sikushauri huyo ni indirect mariooooooo utajutraaaaaa

uking'atwa na nyoka ogopa mijusi
 
Ogopa sana mtu anakwambia usimwambie fulani (hasa wazazi) maana likitokea baya (kupigwa, kudhurumiwa) lawama zitakuja kwako.
kama uchumi hauko vizuri hakikisha unapo enda wazazi wanafahamu
 
Sipendi sherehe ndugu Mimi nimepita huo umri wa kupenda sherehe mi nilimwambia hata kwenda tu kanisani kubariki inatosha,,,bt dharau alinifanyia kubwa mpaka kuongea na wanawake zake mbele yangu
Sasa kinachokufanya utake kurud kwake nini? Au ni hyo biashara ya dispensary? Fanya yako lea mwanao ili mradi anatuma pesa ya matumiz ya mtoto
 
unapewa ushauri ila bado unabishia mawazo ya watoa ushauri haya nenda kwa huyo bwana wako ila usisahau kutupa mrejesho
Anaomba ushauri akiwa tayar na jibu lake huyu hakua na serious kuhitaji ushauri
 
wewe hapa unatafuta cover tuuu.....una habari kuhusu wale wenzio waliodunguliwa kama wewe???? je uko tayari kuwa mke mwenza?? uko tayari kulea mwana wa mwenzio???? eti kuitwa sigle mama kunakuumiza!!!! wewe kuna kitu unatafuta....mfuate tu.........kwani akiwaambia wazazi wako ndo kigezo cha kutokukutesa???? cheza karata vizuri dada...
Karubunika na dispensary
 
Za muda huu wapendwa polen na majukum
Naomben ushaur wenu,,,
Nina mzazi mwenzangu tumezaa mtoto 1.. Kipindi cha uchumba alinitolea mahari ilibaki ndoa tu,, badae kumbe nilikuja kugundua katupa mimba wanawake 2 kwa wakati 1,,,, ikazua maneno na kupelekea kutoishi pamoja,,,alinifanyia visa vingi sana ikiwemo kunitukana,,,,dharau in short mengi ya kuumiza moyo
Tunaishi mikoa tofauti huwa tunawasiliana kwa ajir ya matumizi ya mtoto na hua anatoa kila mwezi kulingana na kipato chake
Kinachonifanya niombe ushauri
Kama wiki hv imepita kaniambia jack nimechoka kukaa mwenyewe haya maisha ya kutangatanga yamenichosha nataka tuishi pamoja kwa vile Mimi kwanza sikua na mahusiano na mtu,,, pili kuitwa single mother hua inaniuma sana maana sikupenda ikabidi nikubali nakufuta yote mabaya alonifanyia....
Nilimwambia ninaplan ya kufungua biashara huku nilipo kaniambia niache twende tukafungue pamoja na yeye huko alipo yaan na yeye aongezee mtaji tufungue kitu kikubwa,, ,
Mimi nimemwambia tufanye kwanza process za ndoa ndio niende anadai kwa sasa hela haitoshi tukakae kwanza uchumi ukishakaa sawa tutaanza mchakato
Kinachonipa mawazo namwambia njoo nyumban uwaambie wazazi kuhusu Mimi kuhamia huko,,anadai nisiwaambie wazazi kama tunaenda kuishi pamoja niage tu nimepata sehem ya biashara huko,, nilipoonekana kulipinga hilo akasema basi Nipigie cm mama yako nimuombe uje na mtoto huku ,,badae uchum ukikaa sawa tutafunga ndoa
Nipo njia panda ninapenda kuishi na baba mtoto ila naogopa asije nigeuka kama mwanzo nashindwa niamue nn kwa sasa nipo dilemma
Naomben mawazo yenu wapendwa

NB,,hali yake kiuchumi sasa hv sio nzuri mshahara mdogo,,watoto 3 kila mmoja na mama na wote kila mwezi anatuma matumizi ,,,inampa mawazo sana nashindwa kuelewa kweli kaamua kwa moyo 1 au maisha yamemchanganya tu
Acha ubwege ndoa ulisha liwa mpaka chalii juu unajidai ndoa[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]

Nyie nani aliwaloga hapo unataka akuongezee mtaji wa biashara huku unataka aingie gharama za ndoa (harusi) ukimchosha mzazi mwenzio anachukua chance unaishia kulalama.
 
Ebu tulia kabisa Huko huko ulipo maana ukisha changanya hiyo pesa ya biashara ndo kwisha habari yako ndoa sio kigezo cha yeye kutokugeuka akaenda zake

"Wanasema the devil is on the details" fikiria kwa makini ni bora uendelee kuwa single mom utapata mme mtaoana ila ukishajichanganya hahahahahaha ur dead
 
Usikubali kufanya mambo kichwa kichwa na bvihuruma visivyo na tija... Fanya yako unayofanya kama ana nia afate taratibu zote uwe mke halali then mtafute vyenu.... Halafu eti muanzishe kitu cha pamoja, thubuuuuutu!!!! Utaishia kulia tu uje ukose pa kuanzia wewe na mwanao. Wanaume waone kama walivo shogaangu, kama kuoa ni gharama basi aende kwa wazazi na wewe uende kwao mjuane then muishi. Ila atafute mtaji wake afanye yake, huwez jua ya kesho, kikinuka unasepa unaenda kuendelea n maisha yko k wa kua kaz yko unafanya. Sasa wewe logwa mfate bila taratibu, kamoe hela zote funguen biashara utakuja kulia apa
 
wewe hapa unatafuta cover tuuu.....una habari kuhusu wale wenzio waliodunguliwa kama wewe???? je uko tayari kuwa mke mwenza?? uko tayari kulea mwana wa mwenzio???? eti kuitwa sigle mama kunakuumiza!!!! wewe kuna kitu unatafuta....mfuate tu.........kwani akiwaambia wazazi wako ndo kigezo cha kutokukutesa???? cheza karata vizuri dada...
[emoji7] [emoji7] [emoji7] [emoji7]
 
Mimi nimemwambia tufanye kwanza process za ndoa ndio niende anadai kwa sasa hela haitoshi tukakae kwanza uchumi ukishakaa sawa tutaanza mchakato
Mwambie siku hizi kufunga ndoa ni 10,000 inatosha, refer yule kijana wa Kenya.
 
Wakati mwingine masuala ya mahusiano hayahitaji ushauri.. Inafika wakati MTU anaamua kulingana na jinsi moyo moyo wake unavyomuelekeza.
Wapo wanaofanikiwa na wapo wanaoharibikiwa kabisa..

Speaking from my personal experience, Nina kesi kama yako.. Nilizaa na mwanaume ambaye wakati wa ujauzito alini mistreat kweli kiasi kwamba nikajipa moyo na kuamua kulea mimba na mtoto peke yangu. Watu walioijua story yangu hakuna hata mmoja aliyetamani kuona kwamba itatokea siku yule baba anisalimie wala ashike mwanangu.

We stayed apart for four good years lakini baada ya muda huo alirudi kwa style hiyo hiyo. Mama yangu akasema usithubutu kumchekea.. (But I loved him..) Kwa kuwa nilikuwa mbali na nyumbani nilirudiana naye kwa siri na Ni miaka mitatu sasa since tumerudiana.

Alipoona wakati unamfaa alikwenda mwenyewe kwa wazazi wangu kujieleza na kuomba radhi na tuna mtoto wa pili sasa .. Hatujawahi tena kugombana..
Sometimes mambo haya hayako uniform I hope. Dada wewe ndyo unamjua vizuri MTU wako zaidi ya sisi wachangiaji. Usikilize moyo wako lile linalokupa Amani lifanye
Wako alikuwa na familia zingine? Huyu ana familia zingine mbili(watoto), hapo ndo pagumu,atamvuruga tu dada wa watu!
 
"ushaambiwa uaiwaage wazazi, hataki ushahidi baadae akikuacha na mtoto wa pili" Tumia akili huyo mwanaume hakupendi na hatokaa akuoe. Mtu mezaa anashindwa kuja home? jiongeze.
 
Kama kakutoea mahali ina maana huyo ni mmeo. Lililopo fanya uchunguzi kama kweli ana nia ya dhati kuishi na wewe!
 
Wako alikuwa na familia zingine? Huyu ana familia zingine mbili(watoto), hapo ndo pagumu,atamvuruga tu dada wa watu!
Labda kwa hilo la familia zingine maana hapo kila mama anahitaji haki ya kuwa mke.. Wa kwangu nashukuru sikuwahi hadi leo kusikia tetesi ya kwamba alikuwa na familia nyingine.
 
Akili za wanawake Mungu anazijua
Jamani Ni kweli ni a kili za wanawake. Lakini habari pia ya kumwambia mtu.. Tulia utapata mwingine.. Sio wote tunatamani kuhesabiwa majumba mengi .. Leo umetoka kwa huyu kesho uko hapa.. Mtoto mmoja ana ubini wa Peter mwingine wa Juma
 
Wanaume wa siku hizi waongo huyo hana mapenzi atakua na mambo yake anayategea kutoka kwako. Jiulize kwa mini anataka mfanye siri kuishi nae wakati hadi mtoto mnae kuwa makini nae
 
Back
Top Bottom