Unajua inabidi kuwaheshimu viongozi wetu? Assuming angekuwa baba yakob ungeweza kuandika maneno ya namna hii juu yake? Kama sivyo, kwa nini uandike juu ya hawa watu heading ya kuwakashfu hivyo, hata kama wasingekuwa viongozi wa Taifa? Heshimuni mamlaka iliyopo madarakani hata kama hamuipendi, ni Mungu ameiruhusu kuwepo pale vinginevyo isingekuwepo. T
uachaneni na kashfa na kudharauliana, mimi huwa ninaamini mtu ambaye anaonyesha dharau kwa mtu mwingine bila sababu ya Msingi, ni yeye mwenyewe huwa amejidharau kwanza, au huwa an-feel kudharauliwa sometimes, hivyo na yeye anajaribu kulazimisha kudharau hata wale ambao hawezi kuwadharau ili afidie gap la majeraha yake. Kuonyesha dharau kwa wenzako bila sababu za Msingi ni utumwa!