Ushamba: Siasa ndani ya ndege ya kibiashara (Dreamliner)

Ushamba: Siasa ndani ya ndege ya kibiashara (Dreamliner)

Dua la kuku halimpati mwewe,aliyeshinda ni yule aliyenunua ndege mpya ya kisasa na kuwakabidhi wananchi waitumie na kuiendesha,na hicho ndio kinachoendelea.Hakuna anayelia kuwa imenunuliwa ndege hewa au abiria wapewa tiketi hewa.Kitu muhimu ndege imebeba abiria na mizigo yao,imeruka na kutua katika anga ya Tanzania kama ilivyopangwa.We need to give a credit when is due.Hongera Magu you have proved the imposibles to be possibles but more kites are required to fulfil catpure and command aerospace business.
 
wakuu nimeshangazwa na hiki kitendo mno ivi kulikua na umuhimu gani polepole kuvaa nguo za chama na kupeperusha bendera wakati ndege ya Ikiwasili mwanza na kilimanjaro maana yake ndege ni ya wanaccm au watanzania kwa ujumla hivi hawaoni wanagawa matabaka nchini?
ndege ile ni mali ya chama cha mapinduzi au mali ya watanzania wote?

ni fedha za chama cha mapinduz zimenunua au ni fedha za walipakodi wa tanzania?

tujitafakari,,,,,,,,,,,
 
Ndege ya Serikali aina ya Boeing 787-8 Dreamliner imeanza safari ya kwanza leo Julai 29, 2018 tangu ilipowasili nchini Julai 8.

Ndege hiyo inayoelekea Mwanza kupitia Kilimanjaro (Kia) iliondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam saa 12:35 asubuhi badala ya saa kumi na mbili asubuhi.

Kabla ya ndege kuondoka abiria walihesabiwa na baadaye wahudumu walitoa matangazo ya usalama.

Tofauti na ndege nyingine za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier, matangazo ya usalama katika ndege ya Dreamliner yanatolewa kwa njia ya video kupitia skrini iliyo mbele ya kila kiti.

Ukaguzi wa abiria

Awali, eneo la ukaguzi wa abiria wa safari za ndani lilijaa hivyo mtu alitakiwa kusubiri kwa takriban dakika 20 ili kukaguliwa jambo lililosababisha muda wa abiria kuingia kwenye ndege kuchelewa.

Idadi ya abiria kwenye chumba cha kusubiri kupanda ndege kilikuwa na watu wengi.

Awali, ilipangwa muda wa abiria kuingia kwenye ndege uwe saa 11:20 asubuhi lakini kutokana na wingi wa watu, walianza kuingia saa 11:35 asubuhi wakitangulia viongozi kadhaa waliokuwapo na waandishi wa habari.

Ndani ya ndege kulikuwa na wahudumu takriban 10 waliotoa huduma kwa abiria kwa ukarimu.

Miongoni mwa abiria waliokuwapo ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi.

Abiria aliyeingia na bendera ndogo tatu za CCM, alimkabidhi moja Polepole aliyekuwa amevaa sare za chama hicho.
Polepole aliyekuwa akipiga picha na baadhi ya abiria alisema, “Magufuli hoyee.”

Baadhi ya abiria aliokuwa amekaa nao karibu waliitikia, “Hoyee.”

Rais John Magufuli aliahidi kuifufua ATCL kwa kuipatia ndege mpya, Dreamliner ikiwa ni utekelezaji wa ahadi hiyo.

Abiria mwingine alisema ndege hiyo inatokana na kodi za wananchi.

Polepole aliijibu kwa kusema, "Ni kweli kabisa hizi ni kodi za wananchi lakini matumizi mazuri yanapangwa na Serikali."

Ilivyokuwa Kia

Ndege hiyo ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) saa 1:17 asubuhi.
Baada ya kutua Kia ikiwa ni mara ya kwanza, ndege hiyo ilipokewa kwa kumwagiwa maji.

Baadhi ya wananchi waliokuwapo uwanjani na wafanyakazi wa Kia walitumia simu zao za mkononi kupiga picha tukio hilo.

Abiria walioshuka uwanjani hapo walikabidhiwa maua.

Katika uwanja wa ndege wa Kia ndege ilikaa kwa dakika 40 kabla ya kuruka kuelekea Mwanza
Ukimpata Polepole, muulize: Kule kwao Katumba (iliyokuwa kambi ya wakimbizi) Dreamliner itasaidiaje kubeba akina Mama wajawazito kwenda hospital ya wilaya/mkoa?
 
Yaani bado mnahangaika na mtu huyu?
mkuu inashangaza sema picha zinakataa kuapload yani badala ya kupepurusha bndera ya tanzania inapeperushwa ya. ccm bc waipake rangi zao ndege ionekane ya kwao kila inapopepuruka angani
 
Upumbavu na aina hii ya wapumbavu inapatikana Tanzania tu. Yaani ni kama vyura wa Kihansi huwezi kuwakuta pengine duniani. Ukikuta mpumbavu wa aina hiyo India jua ni ndugu yako!
unamaana gani mkuu
 
wakuu nimeshangazwa na hiki kitendo mno ivi kulikua na umuhimu gani polepole kuvaa nguo za chama na kupeperusha bendera wakati ndege ya Ikiwasili mwanza na kilimanjaro maana yake ndege ni ya wanaccm au watanzania kwa ujumla hivi hawaoni wanagawa matabaka nchini?
ndege ile ni mali ya chama cha mapinduzi au mali ya watanzania wote?

ni fedha za chama cha mapinduz zimenunua au ni fedha za walipakodi wa tanzania?

tujitafakari,,,,,,,,,,,
Kwani Chedema mlikatazwa kubeba kabendera kenu?
 
Nilikuwa airport asubuhi nikashangaa,nilijua CCM ndio wametengeneza hiyo ndege kumbe tumenunua . Seriously tunaacha kazi za msingi tunaenda kuishabikia ndege kuanza safari yake ya kwanza .Watanzania tulikofikia siko wenzetu wanatengeneza nasisitiza wanazitengeneza nyingi tu sisi kamoja utafikiria tumetua mass tusibweteke Watanzania safari bado Ni ndefu Sana Kama ndege tu tunaacha shughulike zote na kupokea . Anyway hongera Raisi wetu tunashukuru tungeshangilia Nini kwa mfano Maine Seema Nina wivu jamani Ni mawazo yangu ya kishamba
 
inashangaza kwa kweli
 
Shauri yako, watu wanasonga mbele wewe umekalia umbea tu.
Itajaa siku za mwanzo tu baadae itakuwa inaenda na watu 10 tu, hao wa leo makada ni comp tu hizo, nitapanda hiyo kama ndege nyngine haziendi hiyo sehemu kama vile tabora, au nikishaona maji yako shingoni na nyingine zimejaa,
 
Back
Top Bottom