Ushamba: Siasa ndani ya ndege ya kibiashara (Dreamliner)

Ushamba: Siasa ndani ya ndege ya kibiashara (Dreamliner)

Hizi siasa wanazopiga sasa majibu yao yatakuja kwenye business
 
Ndege ya Serikali aina ya Boeing 787-8 Dreamliner imeanza safari ya kwanza leo Julai 29, 2018 tangu ilipowasili nchini Julai 8.

Ndege hiyo inayoelekea Mwanza kupitia Kilimanjaro (Kia) iliondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam saa 12:35 asubuhi badala ya saa kumi na mbili asubuhi.

Kabla ya ndege kuondoka abiria walihesabiwa na baadaye wahudumu walitoa matangazo ya usalama.

Tofauti na ndege nyingine za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier, matangazo ya usalama katika ndege ya Dreamliner yanatolewa kwa njia ya video kupitia skrini iliyo mbele ya kila kiti.

Ukaguzi wa abiria

Awali, eneo la ukaguzi wa abiria wa safari za ndani lilijaa hivyo mtu alitakiwa kusubiri kwa takriban dakika 20 ili kukaguliwa jambo lililosababisha muda wa abiria kuingia kwenye ndege kuchelewa.

Idadi ya abiria kwenye chumba cha kusubiri kupanda ndege kilikuwa na watu wengi.

Awali, ilipangwa muda wa abiria kuingia kwenye ndege uwe saa 11:20 asubuhi lakini kutokana na wingi wa watu, walianza kuingia saa 11:35 asubuhi wakitangulia viongozi kadhaa waliokuwapo na waandishi wa habari.

Ndani ya ndege kulikuwa na wahudumu takriban 10 waliotoa huduma kwa abiria kwa ukarimu.

Miongoni mwa abiria waliokuwapo ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi.

Abiria aliyeingia na bendera ndogo tatu za CCM, alimkabidhi moja Polepole aliyekuwa amevaa sare za chama hicho.
Polepole aliyekuwa akipiga picha na baadhi ya abiria alisema, “Magufuli hoyee.”

Baadhi ya abiria aliokuwa amekaa nao karibu waliitikia, “Hoyee.”

Rais John Magufuli aliahidi kuifufua ATCL kwa kuipatia ndege mpya, Dreamliner ikiwa ni utekelezaji wa ahadi hiyo.

Abiria mwingine alisema ndege hiyo inatokana na kodi za wananchi.

Polepole aliijibu kwa kusema, "Ni kweli kabisa hizi ni kodi za wananchi lakini matumizi mazuri yanapangwa na Serikali."

Ilivyokuwa KIA

Ndege hiyo ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) saa 1:17 asubuhi.
Baada ya kutua Kia ikiwa ni mara ya kwanza, ndege hiyo ilipokewa kwa kumwagiwa maji.

Baadhi ya wananchi waliokuwapo uwanjani na wafanyakazi wa Kia walitumia simu zao za mkononi kupiga picha tukio hilo.

Abiria walioshuka uwanjani hapo walikabidhiwa maua.

Katika uwanja wa ndege wa Kia ndege ilikaa kwa dakika 40 kabla ya kuruka kuelekea Mwanza

Sasa wakiingiza siasa ndio wataanza kuchanganya na kuharibu hii biashara!!!.
Sasa itaonekana kama ndege ya chama!!!!
 
wakuu nimeshangazwa na hiki kitendo mno ivi kulikua na umuhimu gani polepole kuvaa nguo za chama na kupeperusha bendera wakati ndege ya Ikiwasili mwanza na kilimanjaro maana yake ndege ni ya wanaccm au watanzania kwa ujumla hivi hawaoni wanagawa matabaka nchini?
ndege ile ni mali ya chama cha mapinduzi au mali ya watanzania wote?

ni fedha za chama cha mapinduz zimenunua au ni fedha za walipakodi wa tanzania?

tujitafakari,,,,,,,,,,,
....siasa ya ndege inaenda mbali saana
IMG-20180708-WA0004.jpg
IMG-20180708-WA0005.jpg
 
Tuache porojo.Kuna changamoto mbili tatu zinazopelekea mengi ya yaliyolalamikiwa humu.
1) Ndege ni mpya na hatuna marubani ambao walikuwa na masaa ya kurusha hizi ndege.Inabidi kufanya route na line trainings .Waweza fanya line katika airline nyingine wakikuruhusu au unaweza kama tulivyofanya tunafanya kwa supervision ya marubani wa boeing.
2) Viwanja vina changamoto karibu vyote.Kupakia abiria kwa wakati kwa ndege kama 787 kungekuwa na ufanisi kama uwanja unakuwa na jet bridges zaidi ya moja au abiria wapande kwa ngazi za magari mbele na nyuma.Kwa ile case ya A380 iliyotua tulihitaji jet briges tatu mpaka nne.Pia lounge ya mwanza haitoshi kwa maana ya uwepo wa abiria zaidi ya 150.Ila naamini ujenzi wa jengo jipya la abiria uko njiani.Pia runway category ni changamoto.787 inashindwa kwenda Mbeya kwa sababu runway ni moja na ndege haiwezi kugeuza kutokana na urefu wake (Ili pia lipo Arusha kwa ndege za Q400).Ndege fupi kama A320 , B737 na ndogo zake zinageuza.Hiyo pia wahusika wanajua solutions zake.
Hivyo hata ndege za airbus A220-300 (Zamani ziliitwa Bombardier CS300) zitakavyofika mwezi Novemba ,kutahitajika kufanya route training na this time zitafika Mpaka Songwe ,Kigoma na Mtwara kama wakubwa wataona inafaa.
 
Back
Top Bottom