Ushairi: Baridi ya Morogoro haina adabu

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
23,914
23,077
BARIDI YA MOROGORO HAINA ADABU

1. Ya moyoni ninayo, mengi kujaza kapu
Yaani tena yahusuyo, baridi iumizayo pafu
Baridi adabu hamnayo, nawapa yake makavu
Baridi ya Morogoro, kweli haina adabu.

2. Mimi sasa nipo, Uluguru kwa pembeni
Haihitaji hata malipo, milima hii angalieni
Kipupwe hasa kijapo, hakukaliki hasa milimani
Baridi ya Morogoro, kweli haina adabu.

3. Baridi mwaka huu, imefika kwetu pembeni
Tupia jinsi juu, haijari atupia nani
Yapenye hata fuvu, mzungu kapitia dirishani
Baridi ya Morogoro, kweli haina adabu.

4. Mshono yangu sweta, juzi kati nkatupia
Nkatokeza hasa matata, wadhani ninao rupia
Asubuhi baridi kanikamata, sweta yangu kashambulia
Baridi ya Morogoro, kweli haina adabu.

5. Baridi hii haijafunzwa, hasa huko itokako
Wakubwa wadogo wakunjwa, mpaka waone mchoko
Baridi haijui mgonjwa, wote ni viboko
Baridi ya Morogoro, kweli haina adabu.

6. Wanywa chai mwawindwa, baridi iko mafichoni
Wanywa supu hamjapitwa, baridi hii kutibueni
Midomo yenu kuunguzwa, na mchemsho asubuhini
Baridi ya Morogoro, kweli haina adabu.

7. Jana nikajitupa gurioni, baridi dawa mtafutia
Nikajipanga hata mfukoni, muuza dawa asijenkatalia
Kwa mapatano makini, mkoti sufi nkajitwalia
Baridi ya Morogoro, kweli haina adabu.

8. Dawa nyingine nimepata, kufanya kazi kinguvu
Shamba mboga nimepata, baridi timua kimabavu
Kulima dawa matata, baridi haileti uvivu
Baridi ya Morogoro, kweli haina adabu.

9. Mazao mboga nikipata, pesa mshibo uhakika
Reli kasi tutapata, haraka sokoni kufika
Bombadia nayo kupita, Kihonda kubeba karotika
Baridi ya Morogoro, kweli haina adabu.

10.Baridi ishikishwe adabu, sisi tufanyapo kazi
Rais kafuta sababu, sisi kutofanya kazi
Baridi siyo sababu, kaweka furusa wazi
Baridi ya Morogoro, sasa imefunzwa adabu.

===
Mtunzi TUJITEGEMEE wa JF.
-----
Ushairi wangu wa kwanza wenye beti kumi kuwahi kuutunga na kuuandika ndani ya masaa manne. Naomba Maksi juu ya uwezo wangu wa kiswahili na utunzi. Pia unipapo maksi naomba unipe na mapungufu yangu endapo sitapata maksi zako za 100 kwa 100.

Karibuni.
 
Last edited:
Nakupa alama 50%
Umefanikiwa kuzingatia urari wa vina na mizani lakini hujatumia lugha ya kisanaa, mathalani ungetumia misemo/nahau/methali/sitiari/ taswira n.k
Pia hujatumia misamiati ya Kiswahili bali umetumia maneno ya kawaida sana.
 
Asante sana mkuu, yaani uliyoeleza yote sikujua kama ni masharti muhimu katika utunzi wa shairi.
Hongera sana ni mwanzo mzuri!
Ugumu wa kuandika mashairi uko kwenye fani sio maudhui. Ukitaka kuwa jagina katika ulingo huu jitahidi sana kuzingatia fani. Japo hawa watunzi wa kisasa hata maudhui ni shida kwao mfano mzuri ni baadhi ya mashairi ya bongo fleva.
 
Hamsini yako chukua,ndo maksi ulizokwapua!
ushairi unahitaji fikiria,umaridadi na uinjinia.

lugha adhimu umepewa,kiswahili kukitumia
fanya kuchagua vyema,mwali kumchukua.
kwa kiasi umekosha,japo halima umemkosa!

wasome kina malenga,kuna vitu utapata
baridi hutoona tena,wazimu kutapatapa.
 
kwa kiasi umekosha,japo halima umemkosa!

wasome kina malenga,kuna vitu utapata
baridi hutoona tena,wazimu kutapatapa.
ASANTE SANA, USHAURI NIMECHUKUA

Vyanzo bayana, sioni ushairi.
Nimewatafuta sana, Malenga wanishauri
Magazeti mapana, yamewaweka lakiri
Asante sana, ushauri nimechukua
 
Last edited:
Back
Top Bottom