Ushabiki wa Simba na Yanga ndiyo tumefikia huku????

Ushabiki wa Simba na Yanga ndiyo tumefikia huku????

The introvert

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2023
Posts
1,118
Reaction score
2,228
Habari za muda huu wana jamvi

Je ni sahihi kwa hiki kilichofanyika uwanjani?

Ule utani wa jadi uko wapi?

Ushabiki utaenda kutugawa muda si mrefu tutaanza kuona watu wakipigana mapanga na kuuwana kisa ushabiki wa timu hizi mbili.

Wasemaji wa hizi timu kuna namna wanasababisha haya mambo kutokea , nimesikitika juzi kuona video ya CEO wa Simba Sc akitoa kauli za vitisho kwa watani zao kuhusu kuja uwanjani mbele ya press conference kabisa.

Hii si sawa kabisa mamlaka za aoka fumbueni macho., hali inaenda kuwa mbaya.
 
Mchana huu mashabiki wa Simba wamewajeruhi mashabiki wa Yanga waliofika kiwanjani kutazama Burudani ya final ya CAFCC

Tukumbuke viongozi wa Simba walihimiza mashabiki wao kuwadhuru na kuwavamia, Sasa Leo wametekeleza walivoambiwa na viongozi wao

Huu mpira wa miguu ni watu wote, viongozi wa Simba waelimishe mashabiki wao kuwa watu wote kiwanjani hawawezi kuwa upande wako, Kuna watakaokushangilia na kukuzomea

TFF oneni aibu japo mna urafiki wenu na Simba ila toeni adhabu kali Kwa viongozi wa Simba walihamasisha fujo hadi kutaka wapinzani wao wauwawe

SMZ kamateni hao vibaka na kuwafikisha mahakamani Kwa kuvunja amani na utulivu
 
Kibu D kibu Denga aka mkandaji yuko benchi
 
Si sawa
 
Attachments

  • Mashabiki_wa_Simba_SC_hawataki_utani_😀Mashabiki_wa_Simba_SC_hawataki_utani_😀(360p).mp4
    2 MB
Hao nao walipaswa watumie akili. Leo watu wapo kwenye mihemko inatakiwa watumie common sense watabakwa waje walalamike. Wavae nguo za kawaida. Simba leo wanafungwa so wana hasira na kila mtu. Itumike busara wasije lalamikiwa.
 
Back
Top Bottom