Mkuu nimependa mchango wako. Mimi binafsi namkubali sana John Mnyika. Ni kweli anafanya siasa tena za kistaarabu na za kihoja. Amejipambanua kwa hilo na kwake maslahi ya Taifa na watu wake huwa mbele. Hufikia hata wakati akasema twende kwenye win win situation badala ya kuvutana bila sababu. Hilo bila shaka limemjengea maadui wa NDANI na NJE ndani ya Tanzania.katika viongozi wa kisiasa wote hapa tz (na pengine East Africa yote).. ni John Mnyika pekee yake ambae anafanya kazi zake kisasa.. anaweka taarifa ya kazi zake katika mtandao.. akiorodhesha kero na jinsi ya utatuzi wa matatizo yanayolikabili jimbo lake na tz kwa jumla..! najua hili linawakera wengi ambao kwao uongozi umepotea njia.. so watajaribu kila wawezalo kum-discredit John.. Naomba wale wote wenye mapenzi mema na nchi hii waendelee kumlinda John dhidi ya hawa wasio na vision.. Peke yake hataweza bila ya msaada toka kwe2 maana hawa ni watu ambao wako tayari kuwaua hata wazazi wao..
Gazeti la Uhuru si kulisoma tu hata kufungia maandazi halifai.
Hi thread imeshajibiwa na mnyika mwenyewe humu jamvini mchana,naona umeamua kuirudisha tena na chanzo chake cha gazeti la chama cha CCM uhuru,habari hizo ni uongo mtupu na Mh mnyika ameshakanusha humu jamvini! Haya nenda ofisi za CCM ukachukue posho baada ya kumaliza kazi uliyotumwa na masaburi wako Nape.
Anastahili kupopolewa, bora wangemnyuka kisawasawa, amekalia kupiga domo tu huyu.
Hicho chanzo, mh!!!!!!!
Umeita tetesi halafu umetoa hitimisho kama vile ni ukweli, hizi sasa ni siasa chafu. Ni vizuri ukaeleza nilipigwa mayai viza lini na wapi? Vyombo vya habari unavyovisema ni vipi na weka hapa habari kamili ijadiliwe. Niko tayari kupokea ushauri, lakini si vyema kuleta uzushi na propaganda nyeusi.
JJ
Hawaruhusu maneno mabovu ningekutukana ila we ni hamnazo.
Ni uzushi tu.
kuna baadhi ya mijitu humu ni mapu...kabisa, yaani yanakuja na post za ajabu ajabu sijui yamelipwa shilingi ngapi na napee yawachafue watu!
Umesema mkuu. Ni kweli Mnyika asitegemee tu kujenga hoja ndani ya Bunge. Kwa kujenga hoja namkubali ila akumbuke wanaubungo huwa hawasilizi hoja wanataka matendo hivyo basi aendelee kutenda. Nakumbuka Mwaka 2010 kabla ya kura za maoni ndani ya CCM nilikuwa Kyela. Katika pitapita yangu nikagundua kulikuwa na watu wanamwaga bia na soda kwenye vijiwe, wakati watu wanaendelea kunywa jamaa wakawa wanatumbukiza hoja na kusema: Jamani huyu mbunge wetu sisi tunataka atuletee maendeleo jimboni kwetu lakini yeye amekuwa akiongelea mambo ya kitaifa kuhusu ufisadi, hatufai huyu! Mnyika nawe usije ukajengewa hilo zengwe!Uwe uongo ama uzushi kazi yetu ni kuchukulia hiyo kama changamoto KWANI ni kweli kuna negative response kutoka kwa public kwa mtazamo wa poor performance ya wabunge wetu vijana kote, mfano mbeya ukuacha mh. silinde kule mbozi anaonyesha uhai. siwezi sema sana kwa myika ingawa nimepita maeneo ya mbezi lwis na kwa msuguri nk sijaona malalamiko yoyote. lakini hata hivyo asije na kukataa bali afanyie kazi
Mkuu wa chuo, chanzo cha Habari kama ni Uhuru hapa huwa hakiheshimiki kwasababu ni gazeti la magamba.
nilikuwa sijaona kama alikwisha ijibu lakini mi ndio nimeiona mida hii kwenye gazeti la uhuru! Hizo posho kwa Nape hapo mi sijui, labda we unaweza ukawa unafahamu sana kuliko unaemsadikisha anachukua posho!
Duh!!!!!
Gazeti la uhuru lipo mtaani?