Usanii wamponza Mnyika - Uhuru

Umeita tetesi halafu umetoa hitimisho kama vile ni ukweli, hizi sasa ni siasa chafu. Ni vizuri ukaeleza nilipigwa mayai viza lini na wapi? Vyombo vya habari unavyovisema ni vipi na weka hapa habari kamili ijadiliwe. Niko tayari kupokea ushauri, lakini si vyema kuleta uzushi na propaganda nyeusi.
JJ
John,

you dont need to answer these lunatics... they are paid to smear people and some are cheap and have nothing to lose because CCM has taken everything away from them

STAND UP TALL, IGNORE THESE MUPPETS!!!!
 
Umeita tetesi halafu umetoa hitimisho kama vile ni ukweli, hizi sasa ni siasa chafu. Ni vizuri ukaeleza nilipigwa mayai viza lini na wapi? Vyombo vya habari unavyovisema ni vipi na weka hapa habari kamili ijadiliwe. Niko tayari kupokea ushauri, lakini si vyema kuleta uzushi na propaganda nyeusi.
JJ

Kwa namna gharama za maisha zilivyo juu, sidhani kama kuna anayeweza kutupa mayai hata kama ni viza!
 
Mbunge wangu Mnyika,i have no doubt with you nor your perfomance.
Najua unafahamu tataizo kubwa la maji kimara,naomba unisaidie kuwadharau wabunge wote waliopita bila kulitatua tatizo hili. Nimezaliwa kimara,nimekulia kimara,nimepata degree yangu nikiwa kimara,nimeanza kazi nikiwa kimara,na mpaka sasa nishafanya kazi kampuni tatu tofauti bado ni mkazi wa kimara ila tatizo la maji halijawahi kuisha kwa kipindi chote hicho.
Naamini utakua shujaa wa kulimaliza tatizo hilo
 
Safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Mheshimiwa Mnyika I am proud of you na kwa kweli kila napoona unatoa majibu kwa hoja unafanya nisijutie nauli niliyolipa toka Shinyanga kuja Dar kupiga kura jimbo la Ubungo kwa sababu niliamini unaweza na naendelea kuamini hivyo

Asante, ingia tu hapa: JOHN MNYIKA, utapata update ya hatua kwa hatua. Kwa sasa niko katikati ya kazi, nitarejea kujibu swali kwa swali kwa yoyote atayependa kufahamu zaidi, mimi naamini zaidi kwamba matendo yanapaswa kuzungumza yenyewe kuliko maneno. Hivyo, wananchi wenyewe ndio wanapaswa kulinganisha kati ya mbunge wa sasa wa Ubungo na wabunge waliopita wa Jimbo hili, katika kipindi cha mwaka mmoja ambao nimekuwa kwenye utumishi. Aliyekuwepo kwenye Mkutano huo unaotajwa wa Mburahati aje hapa aeleze, siku hiyo nilieleza wazi wananchi kwamba sitahutubia, bali ni kuelezana tu hatua iliyofikiwa katika kila jambo walilonituma, na nilieleza na wananchi walieleza wazi kwenye mkutano huo wa hadhara kuridhika na utumishi wangu kwao katika kipindi cha mwaka mmoja tofauti na miaka mingi ya waliotangulia. Wakanipa kazi nyingine zaidi za kufuatilia, ikiwa CCM wana hamu sana nirudi Mburahati kwa mara nyingine tena kufanya mkutano mwingine ili idhihirike mimi na wao ni nani wa kupigwa mayai viza, waseme tu nirudi. Lakini, ishara ya wananchi kuridhika ni kwamba walikaa kwenye mkutano huo wa hadhara kuanzia jioni mpaka usiku saa moja giza likiingia. Na pia tulitembea pamoja wa miguu toka Mburahati Barafu, Darajani mpaka Mpakani kwenye mabonde mbalimbali. Na ishara nyingine ya kuridhika ni kwamba badala ya kupungua kwa bendera za CHADEMA siku hiyo wananchi wakaamua kufungua matawi na misingi zaidi ya CHADEMA mbele yangu. Pia, kwenye suala la maji baada ya kueleza hatua ambazo tumechukua niliwaomba waonyooshe mikono wote wanaunga mkono na walifanya hivyo mkutanoni, mkutano wenye mayai viza ungevunjika mara baada ya kuanza badala yake kwa mwamko wa wananchi siku hiyo nilihutubia mpaka usiku kinyume cha sheria.

JJ
 
gazeti la uhuru linamilikiwa na serikali mhariri wafanya kazi wote wanalipwa na serikali ni mara chache kuhoji utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya ccm ila ni wepesi kukurupuka na kuandika habari ya kuuza gazeti ila wasiwasi wangu ni kuwa
wamepoteza uwezo au .ni kitu gani kimewasibu
 
Umeita tetesi halafu umetoa hitimisho kama vile ni ukweli, hizi sasa ni siasa chafu. Ni vizuri ukaeleza nilipigwa mayai viza lini na wapi? Vyombo vya habari unavyovisema ni vipi na weka hapa habari kamili ijadiliwe. Niko tayari kupokea ushauri, lakini si vyema kuleta uzushi na propaganda nyeusi.
JJ
Pole sn mkuu kwa usumbufu unaoupata. Sisi kama wapiga kura wako tuna imani sana na wewe. Achana na hizo propaganda bali piga kazi jembe letu. Tayari tumeona juhudi zako ktk kazi yako ya ubunge.

Huyo aliyeleta hiyo mada ni ama ametumwa kukuchafua au an ajenda yake binafsi kwa manufaa yake au kikundi cha watu fulani.

HITIMISHO
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Hapa namaanisha kuwa aliyoyafanya mh mnyika kama ni mazuri basi tumpe haki yake. Na pale anapohitaji kupewa ushauri basi apewe. My comrade mnyika watch out bro!
 
Umeita tetesi halafu umetoa hitimisho kama vile ni ukweli, hizi sasa ni siasa chafu. Ni vizuri ukaeleza nilipigwa mayai viza lini na wapi? Vyombo vya habari unavyovisema ni vipi na weka hapa habari kamili ijadiliwe. Niko tayari kupokea ushauri, lakini si vyema kuleta uzushi na propaganda nyeusi.
JJ

Nakumbuka magazeti yalifanya kazi kubwa sana kwa Sumaye (negatively) na kwa Kikwete (positively) around 2005. Ni vyema Mh

Mnyika ukachukua hatua gazeti hilo maana ni defamation per se! Otherwise watanzania wengi wanaosikiliza clouds na vituo vituo

vingine vinavyotangaza magazeti wataamini. Kukanusha hapa JF ambapo si watanzania wengi wana access compared to Radio

Stations haitoshi. If you didnt know CCM are determined to take back Ubungo 2015 at any costs legal or illegal! watch out! Play

smart.
 
Kwa namna gharama za maisha zilivyo juu, sidhani kama kuna anayeweza kutupa mayai hata kama ni viza!
Siku hizi uswahilini miguu na vichwa vya kuku ndio mboga ya weekend, yaani familia hapo ndio inahesabu imekula kuku.
Back to the topic, hizi siasa za gazeti la CCM ndio zile zinazoitwa Gutter politics ( siasa uchwara )
 
Mkuu unaweza lishtaki hilo gazeti la Uhuru kwa kukuchafulia jina?
 
Jambo la msingi mheshimiwa Mnyika sio kusema umepigwa mayai viza au la, wabaya wako wanaweza kusema/kufanya lolote ili kukuharibia. Sisi kwa nje tunaona uimara na uhodari katika uchapakazi wako ndani ya Chadema, na kwa ajili ya taifa letu. Lakini ndani ya jimbo lako la ubungo ni wewe na wanajimbo wako mnaweza kusema kwa undani. Gazeti liandike/lisiandike la msingi ni kile kinachojulikana kwako na wanajimbo lako. Kama kuna kilio cha wanajimbo wako ufuatilie kama ni kweli au la. Ni wazi hata kama kuna ahadi zilitolewa zote haziwezi kutekelezwa ndani ya mwaka 1. Lakini pia inategemea ni ahadi ya namna gani, inayotekelezeka au la. Kama uliahidi kugeuza ubungo kuwa "Dubai", labda hutaepuka lawama, kwani hiyo ni vigumu kutekeleza. Mungu akubariki. Mungu aibariki Chadema, Ubungo na Tanzania kwa ujumla.
 
Hongera sana mnyika hakuna kulala brazaa hadi kieleweke! Mungu azidi kukupigania tunahitaji wabunge zaidi aina yako!
 
Nyoka hazai mjusi, watoto wa nyoka nao ni nyoka ni lini mtamkana baba yenu wa uongo? Badilikeni leteni hoja zenye mashiko na si kuchafua watu ovyo.
 
Mkuu unaweza lishtaki hilo gazeti la Uhuru kwa kukuchafulia jina?
Hili ndilo nilikuwa nalitaka. Kumbe kuna wakati unakuwa muungwana? Kama gazeti limezusha alipeleke tu kwa pilato yaani baraza la habari ili likemewe na kutakiwa kumuomba radhi.
 
Jimbo la Ubungo Nepi bado analihitaji na analitolea udenda sana. Magazeti ya uhuru na mzalendo lipo chini ya idara ya uenezi ya CCM inayoongozwa na Nepi.
Just connect the dots utaelewa maana yake..
Hapo umesema vyema. Nadhani umemsaidia pia Mkuu Hugo Chaves. Nadhani pia kama alivyosema Fidel80 ni vyema Mnyika akalishitaki hili gazeti ili iwe fundisho kwake na magazeti mengine yenye tabia kama hiyo! Hiki ni chombo cha habari pamoja na kwamba kinamilikiwa na CCM hivyo hiyo jabari kuna kundi kubwa litaiamini kama haitakanushwa na gazeti lenyewe.
 
Umeita tetesi halafu umetoa hitimisho kama vile ni ukweli, hizi sasa ni siasa chafu. Ni vizuri ukaeleza nilipigwa mayai viza lini na wapi? Vyombo vya habari unavyovisema ni vipi na weka hapa habari kamili ijadiliwe. Niko tayari kupokea ushauri, lakini si vyema kuleta uzushi na propaganda nyeusi.
JJ

kweli kamanda wetu huyu jamaa katumwa na mag.amba kuja kukuchafua ila laiti tungemjua tungemkata sikio moja
 
Back
Top Bottom