Usaliti: Nusura niue mtu hii weekend

Usaliti: Nusura niue mtu hii weekend

Tuliza munkari mama, Ila ulifanya mambo jema kwa kutumia kila aina ya njia kupunguza stress kama kulia, kulala, na kushare hayo matatizo kwa mtandao ili ufarijike, cha kufanya hapo msamehe huyo jamaa we songa na maisha kivyako
Nimesha msamehe Mkuu ndio maana ata anaishi...ila akijaribu kunifuatilia tu,...He will face my real satanic version.
 
Kwanza, pole sana kwa yaliyokupa, unachotakiwa kujua ni kwamba hata kwenye mahusiano kuna ajali kama hizi.
Akili uliiaminisha kumwamini na hukuipata nafasi ya kupokea matokeo hasi kama haya ya kusalitiwa.
Pili, kama kweli ulimpenda kama unavyojinasibu naamini utamsamehe baada ya hasira kukuisha.
Tatu, kufuga chuki moyoni ni hatari sana kwa afya yako (hususani ukimuona unayemchukia anakula raha na wengine) na kumchukia mtu asiyekukosea kwa sababu ya mtu mwingine ni kosa pia.
All in all asante kwa ushauri na kila la heri katika maisha yako mapya.
 
Ulivyowaona Alafu Ukaondoka Kwenda Kupanga Jinsi Ya Kuwaua. Basi Hapo Mwanasheria Labda Akusaidie Ufungwe Maisha Badala Ya Kunyongwa. Kama Ulivyoingia Ukaenda Moja Kwa Moja Chumbani Ukachukua Kama Chupa Ya Soda Umeikuta Ndani Ukawaua Bas Labda Mwanasheria Angekusaidia Toka Murder To Manslaughter Under Provocation. Ila Ukaenda Hone Alafu Urudi. Ile Passion Yako Ilicool Ungerudi Tena Iyo Ni Kuua Kwa Kukusudia My Dear. Shukuru Mungu Sana. Alafu Hakua Mumewako So Ungeenda Jela Kwa Sababu Ya Kijinga Sana Tbh.
 
Never make a decision when you are angry. Pole sana kwa shurba hiyo
Had I made a decision when I was angry,perhaps by now I would have a murder case at hand to answer....nimetulia sana Mkuu ndio nikafikia hayo maamuzi.
 
Changamoto kwakweli..
Daah ndo maana mie nafikiria sana nitamuoa nani hasa kwa kizazi hiki, ukiwaona njiani wanavyong'aa mwenyewe utakubali lakini kumbe kuna jitu limegegeda zaidi ya miaka mitano bila ndoa, yaani daah acha waumizwe tuu maana hawajiongezi kabisa hawa dada zetu. kama wewe mvulana unajitunza kusubiri ndoa halafu unakutana nalo la hivi duuh Mwenye-Ezi Mungu aniepushie MBALI KABISA.
 
Ulivyowaona Alafu Ukaondoka Kwenda Kupanga Jinsi Ya Kuwaua. Basi Hapo Mwanasheria Labda Akusaidie Ufungwe Maisha Badala Ya Kunyongwa. Kama Ulivyoingia Ukaenda Moja Kwa Moja Chumbani Ukachukua Kama Chupa Ya Soda Umeikuta Ndani Ukawaua Bas Labda Mwanasheria Angekusaidia Toka Murder To Manslaughter Under Provocation. Ila Ukaenda Hone Alafu Urudi. Ile Passion Yako Ilicool Ungerudi Tena Iyo Ni Kuua Kwa Kukusudia My Dear. Shukuru Mungu Sana. Alafu Hakua Mumewako So Ungeenda Jela Kwa Sababu Ya Kijinga Sana Tbh.
Mkuu naona Mungu aliniepusha na hilo, ingawa nilipanga kuwaterminate kimafia...siyo ile ya kumdelete ni ikiwa na real identity.
 
Kama mchumba tu anataka kuua kisa fumanizi ungekua umeolewa je?
 
Kwanza, pole sana kwa yaliyokupa, unachotakiwa kujua ni kwamba hata kwenye mahusiano kuna ajali kama hizi.
Akili uliiaminisha kumwamini na hukuipata nafasi ya kupokea matokeo hasi kama haya ya kusalitiwa.
Pili, kama kweli ulimpenda kama unavyojinasibu naamini utamsamehe baada ya hasira kukuisha.
Tatu, kufuga chuki moyoni ni hatari sana kwa afya yako (hususani ukimuona unayemchukia anakula raha na wengine) na kumchukia mtu asiyekukosea kwa sababu ya mtu mwingine ni kosa pia.
All in all asante kwa ushauri na kila la heri katika maisha yako mapya.
Asante Mkuu...nimesha samehee na sina chuki, hata nikimuona na mtu mwingine wakiwa pepona wanapata raha nitawabariki pia.
 
Had I made a decision when I was angry,perhaps by now I would have a murder case at hand to answer....nimetulia sana Mkuu ndio nikafikia hayo maamuzi.
Yes mjumbe wa amani, saying huhitaji tena mwanaume hayo ni maamuzi ya hasira, in reality utasahau alichokufanyia na kuingia kwenye mahusiano mapya
 
Mkuu naona Mungu aliniepusha na hilo, ingawa nilipanga kuwaterminate kimafia...siyo ile ya kumdelete ni ikiwa na real identity.
Roho Ya Mtu Sio Kitu Cha Rahisi. You Never Know. Hilo Kosa Sidhani.La Kuwish Mtu Afe. Just Move On. Then Ushajifunza Usipende 100%....
 
Na Mimi Nina stress hapa nione pm tu nyutralaizi atress zetu
 
Mabibi na Mabwana wa JF salam!
Ni imani yangu kwamba mmekuwa na weekend njema na yenye utulivu nawapongeza sana na poleni kwa mliokumbwa na dhoruba za maisha kama mimi.Binafsi hii weekend haijawa nzuri kwangu kwani ilibaki chembe kabla sijampeleka mtu kuzimu. Mungu wangu! pengine mida hii ningekuwa nahaha kutafuta mawakili wa kunitetea kwenye murder case.
NDUGU ZANGU IPO HIVI:
Nilikuwa kwenye mahusiano na mwanaume mmoja kwanzia jun.12 2011 hadi Ijumaa iliyopita tar.2 sep 2016. Kwakweli tulipendana mno tena sana, tulijaliana na kushirikiana kwa kila jambo, Mimi nilipenda sana, nilimjali na kumheshimu kwenye kila kitu.Hakuwa mkamilifu kwa 100% ila nilitambua hakuna haja ya yeye kuwa mkamilifu hivyo nilimpenda kwa moyo wote, nilimwona ni sehemu ya mwili na maisha yangu mimi, kwahiyo nilimjali kama ninavyojali mwili na maisha yangu mwenyewe.Mapungu ya kibinadamu aliyokuwa nayo nilijisi kama vile ni ya kwangu so nilimuweka wazi kabisa ni jinsi gani nilivyompenda.
Kuhusu yeye siwezi kueleza yote, alinipenda hadi nikajihisi kwamba nina deni kwake...He was more than a generous lover.Alinijali kwanzia nje hadi chumbani nakote huko niliridhika na kujiona nimepewa kuliko nilivyostahili.
Kwa ufupi tulikuwa na mapenzi ya dhati sana.Kwa hicho kipindi cha miaka mitano na zaidi, tulipata furaha iliyosaidia kupooza changamoto za maisha tulizo kabiliana nazo, It was like a single soul living within the two separate bodies.Wote tulikuwa na imani moja, yaani kuishi pomaja milele panapo majaaliwa ya Mungu.

MKASA WENYEWE:
Kwenye mahusiano yetu tulikuwa na mazoea ya kutoka pamoja kila ijumaa ama jumamosi kwenda sehemu nzuri ya utulivu na kuongea mawili matatu juu ya maisha yetu.Juzi ijumaa nilimpigia simu mida ya saa nane hadi tisa lakini simu yake haikupatikana.Basi nikachukua uamuzi wa kwenda kwake kumjulia hali na kama mambo yangekuwa poa basi tutoke kama kawaida yetu(kila tulipotoka tulichangia gharama, kwa jinsi nilivyompenda sikukubali kabisa abebe mzigo wote wa ghara, wakati mwingine nililipa mimi au yeye.Ulikuwa ni utamaduni wetu). Nilipita sehemu nikanunua matunda mbali mbali na ya kutosha, nilipenda sana kubeba chochote pindi niendapo kwake.
Baada ya kufika nilipatwa na mshangao pale nilipoona viatu vya kike mlangoni,nikajiuliza vitakuwa vya nani? moja ya jibu lililonijia pengine ni ndugu yake wakike kamtembelea.Nikaingia ndani nikazidi kushangaa zaidi, sebuleni hakuna mtu na mlango upo wazi.Ghafla nikasikia kicheko cha Mwanamke chumbani, Oh my God! sikuhitaji genus aniambie nini kinaendelea ndani.Nilipatwa na kizungu zungu lakini niliweza kujimudu, nikaweka mikoba yangu chini nikatoka nje kuchungulia kwa dirishani...nilichokiona sikuamini! yani mwanaume niliyempenda kwa moyo wangu wote leo kamkumbatia mwanamke mwingine? office mate wake wa kike?.Anyway iliniuma ila sikupatwa na mshituko sababu nilishajua kilichokuwa kinaendelea...jamani yasikie tu, lakini maumivu niliyohisi Mungu ndiye ajuaye.
Nilichokiamua ni kuwadelete hao wasaliti wangu kwenye uso wa dunia, Kweli niliamua kuwauwa wote! potelea mbali, liwalo na liwe.Nikaingia ndani nikachukua mikoba yangu nakuondoka ili kupanga namna nitakavyotekeleza hukumu yangu.Ile nakatiza kona mara nikasikia mtu ananiita jina, alikuwa ni huyo mwanaume akiwa kavalia pensi.Sikutaka kumsikiliza, nilichapa mwendo hadi kwenye gari na kwenda zangu hadi nyumbani.
Baada ya kufika nyumbani nilikwenda moja kwa moja hadi chumbani na kulia sana, nililia kama mtoto mdogo.Hadi saa tano usiku mashavu yaliniuma, macho yalivimba na muda wote mate yalikuwa machungu mdomoni...nikapitiwa na usingizi hadi asubuhi.

Sasa jana katuma watu waje kumwobea msamaha, kwamba eti amekosa nimsamehe, niliwarudisha mbio bila kujali ni kina nani...alimtuma hadi mama yake mzazi ila nilimwambia, mama huyo mwanao zamani alikuwa mpenzi wangu na pengine mume mtarajiwa ila kwa sasa namwona kama bata mweusi tu.Nimemwambia Mama yake amwambie atafute mwanamke mwingine wa kuchezea siyo mimi...siwezi kuwa kwenye mahusihano na bata asiye na utu, yaani kumbe alikuwa ni michepuko ila aliigiza maisha pindi alipokuwa na mimi?.Anywa kwa kuwa aliniona pindi naondoka kwake, nionda adhabu ya kifo.Akifa ili hali inaeleweka kwamba tupo kwenye mgogoro sintakuwa salama, laiti kama asingeniona lazima ningepanga mipango ya kwaondoa wote!!! wacha waishi ila sintarudiana naye ata kama Mbingu zitashuka kuja kutupatanisha.

MWISHO:
Nimekuja hapa jukwaani;
1.Kuwaomba radi niliowakwaza jana jioni na leo asubuhi, jamani niwieni radhi, nilikuwa na hasira juu yenu pasipo sababu.
2.Kuwaasa wanawake wenzangu kuwa makini na hawa wanaume, wachache ni wanaume ila wengi wao ni wavulana walioishi miaka mingi
3.Enyi wanaume kuweni makini mnapopewa moyo wa mtu, inauma sana kusalitiwa jama.Wanawake tu dhaifu ila siyo sababu ya kutokuwa wakatili pindi unapopita kwenye 18 zetu vibaya.

Maamuzi nimeshafanya mwenyewe KAMWE SINTOMRUDIA HUYO BATA MWEUSI, kwa hiyo siitaji kushauriwa juu ya hilo.Nimeshagombana na rafiki zangu wawili kisa shauri zisizo na umuhimu.NIMEKUJA KUWAASA TU JAMANI ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI.

Ukiua mtu kwa sababu ya mwanamme au mwanamke wewe ni mnyama na hujafikia kiwango cha kujitenga na mnyama kama binadamu mwenye kutumia fikra zaidi ya kuhemuka.
 
Dunia imeisha na imefika mwisho,kwa nini ulikubali kuwa na uchumba sugu(miaka mitano)???.......Sasa hivi utaanzisha tena mahusiano na utakaa tena na uchumba sugu kwa miaka mitano jumla inakuwa kumi!!!,na huenda ukaachika tena!!.....what next???.....uzinzi umekuwa fasion siku hizi???
 
Back
Top Bottom