Usaliti: Nusura niue mtu hii weekend

Usaliti: Nusura niue mtu hii weekend

yaani toaka 2011 mtu anakugegeda si mtoto angeshaanza shule?
kweli uzinzi haulipi ebu cheki faida yake
ungetulia zako miaka yote hyo ungekuwa mbali
mlikuwa mnapanga nini miaka yote hyo? yaani mimi sikai na mwanaume hata mwezi kama hasomeki bora nionekane sina maana kuliko kuwa daraja la mtu
Kama kusomea udaktari......
 
Story yako ni nzuri kwakweli.........inaonyesha jinsi gani bongo movie imewaathiri kizazi cha kisasa..........

Okay ngoja na mimi nikomenti kibongo movie......
1.Jambo la kwanza kujua ni je.........huyo mwanaume ana matatizo gani ya akili maana kwanini akae na demu ndani akijua wazi ijumaa ni siku ambayo unakuja na lazima utamtafuta........na upo free kuja kwake.....
2. Imekuwaje mlango akaacha wazi na akijua wazi yupo na mlupo ndani na mtu anaweza ingia kwa bahati mbaya akawakuta....
Hivi kwenye post hujaona hata mimi nimejiuliza hayo maswali? hili jambo sijawahi kulishuhudi, ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa muda wote huo.
 
unaangalia na mahusiano yenyewe deny miaka 6 hata mtu hakuoi? halafu anachepuka live ? mmmh weee
Huyo mwenzio kilichomponza kukaa na mpenzi wake sehemu tofauti sasa katika mahusiano hakuna mwanamume mpumbavu atakae shindwa piga mechi za nje kwa hiyo miaka 6 huku wakiishi sehemu/mitaa tofauti..abiria chunga mzigo wako
 
Kama ndo kwanza umesalitiwa kweli inauma unaweza kuua bila kukusudia!jikaze tu ndio ya dunia sie wanaume tuna udhaifu flani kwamba ukushaona unapendwa masikio yanazidi kichwa isitoshe sie wanaume tuna kasumba moja matata sana yaani hatuna msimamo mmoja thabiti siwezi kusema huo ni udhaifu wetu ila nachohisi ni kudharau hisia za ulienae na kujikuta unamsaliti bila chembe ya kujishtukia!mwanaume kwa mwanamke ni kama mfupa kwa fisi akichekewa anafanya kweli
 
Huyo mwenzio kilichomponza kukaa na mpenzi wake sehemu tofauti sasa katika mahusiano hakuna mwanamume ******** atakae shindwa piga mechi za nje kwa hiyo miaka 6 huku wakiishi sehemu/mitaa tofauti..abiria chunga mzigo wako
sasa angehamiaje bila utaratibu?
 
Kwa sasa utasema hivyo ila hasira zikipungua utabadili msimamo na kuanza kuvutiwa na njemba zitakazokuwa zinakukonyeza huku zikitabasamu.

Labda kama wewe ni KE tunaweza kuwa marafiki...ila siitaji mwanaume tena!
 
Inategemeana ila kuna watu wamekaa miaka 8 ndo harusi imetokea, na tabia za mtu mwenyewe zina husika
kwanini mtu anitongoze kama hana mpango wa kuwa na mimi ?
miaka 6-10? haikubaliki huo ni uchochezi
 
Pole sana omba utampata wakweli, Yawezekaa Mungu hakupanga awe mme bora kwako uchumba gani miaka 6? Nakama alikuwa anakupenda nakukuthamini iweje alete mwingine nyumbani kwake ni afathali wangetoka alifanya makusudi yawezekana kakuchoka hiyo ni gia yakukubwaga fanya yako
 
Mabibi na Mabwana wa JF salam!
Ni imani yangu kwamba mmekuwa na weekend njema na yenye utulivu nawapongeza sana na poleni kwa mliokumbwa na dhoruba za maisha kama mimi.Binafsi hii weekend haijawa nzuri kwangu kwani ilibaki chembe kabla sijampeleka mtu kuzimu. Mungu wangu! pengine mida hii ningekuwa nahaha kutafuta mawakili wa kunitetea kwenye murder case.
NDUGU ZANGU IPO HIVI:
Nilikuwa kwenye mahusiano na mwanaume mmoja kwanzia jun.12 2011 hadi Ijumaa iliyopita tar.2 sep 2016. Kwakweli tulipendana mno tena sana, tulijaliana na kushirikiana kwa kila jambo, Mimi nilipenda sana, nilimjali na kumheshimu kwenye kila kitu.Hakuwa mkamilifu kwa 100% ila nilitambua hakuna haja ya yeye kuwa mkamilifu hivyo nilimpenda kwa moyo wote, nilimwona ni sehemu ya mwili na maisha yangu mimi, kwahiyo nilimjali kama ninavyojali mwili na maisha yangu mwenyewe.Mapungu ya kibinadamu aliyokuwa nayo nilijisi kama vile ni ya kwangu so nilimuweka wazi kabisa ni jinsi gani nilivyompenda.
Kuhusu yeye siwezi kueleza yote, alinipenda hadi nikajihisi kwamba nina deni kwake...He was more than a generous lover.Alinijali kwanzia nje hadi chumbani nakote huko niliridhika na kujiona nimepewa kuliko nilivyostahili.
Kwa ufupi tulikuwa na mapenzi ya dhati sana.Kwa hicho kipindi cha miaka mitano na zaidi, tulipata furaha iliyosaidia kupooza changamoto za maisha tulizo kabiliana nazo, It was like a single soul living within the two separate bodies.Wote tulikuwa na imani moja, yaani kuishi pomaja milele panapo majaaliwa ya Mungu.

MKASA WENYEWE:
Kwenye mahusiano yetu tulikuwa na mazoea ya kutoka pamoja kila ijumaa ama jumamosi kwenda sehemu nzuri ya utulivu na kuongea mawili matatu juu ya maisha yetu.Juzi ijumaa nilimpigia simu mida ya saa nane hadi tisa lakini simu yake haikupatikana.Basi nikachukua uamuzi wa kwenda kwake kumjulia hali na kama mambo yangekuwa poa basi tutoke kama kawaida yetu(kila tulipotoka tulichangia gharama, kwa jinsi nilivyompenda sikukubali kabisa abebe mzigo wote wa ghara, wakati mwingine nililipa mimi au yeye.Ulikuwa ni utamaduni wetu). Nilipita sehemu nikanunua matunda mbali mbali na ya kutosha, nilipenda sana kubeba chochote pindi niendapo kwake.
Baada ya kufika nilipatwa na mshangao pale nilipoona viatu vya kike mlangoni,nikajiuliza vitakuwa vya nani? moja ya jibu lililonijia pengine ni ndugu yake wakike kamtembelea.Nikaingia ndani nikazidi kushangaa zaidi, sebuleni hakuna mtu na mlango upo wazi.Ghafla nikasikia kicheko cha Mwanamke chumbani, Oh my God! sikuhitaji genus aniambie nini kinaendelea ndani.Nilipatwa na kizungu zungu lakini niliweza kujimudu, nikaweka mikoba yangu chini nikatoka nje kuchungulia kwa dirishani...nilichokiona sikuamini! yani mwanaume niliyempenda kwa moyo wangu wote leo kamkumbatia mwanamke mwingine? office mate wake wa kike?.Anyway iliniuma ila sikupatwa na mshituko sababu nilishajua kilichokuwa kinaendelea...jamani yasikie tu, lakini maumivu niliyohisi Mungu ndiye ajuaye.
Nilichokiamua ni kuwadelete hao wasaliti wangu kwenye uso wa dunia, Kweli niliamua kuwauwa wote! potelea mbali, liwalo na liwe.Nikaingia ndani nikachukua mikoba yangu nakuondoka ili kupanga namna nitakavyotekeleza hukumu yangu.Ile nakatiza kona mara nikasikia mtu ananiita jina, alikuwa ni huyo mwanaume akiwa kavalia pensi.Sikutaka kumsikiliza, nilichapa mwendo hadi kwenye gari na kwenda zangu hadi nyumbani.
Baada ya kufika nyumbani nilikwenda moja kwa moja hadi chumbani na kulia sana, nililia kama mtoto mdogo.Hadi saa tano usiku mashavu yaliniuma, macho yalivimba na muda wote mate yalikuwa machungu mdomoni...nikapitiwa na usingizi hadi asubuhi.

Sasa jana katuma watu waje kumwobea msamaha, kwamba eti amekosa nimsamehe, niliwarudisha mbio bila kujali ni kina nani...alimtuma hadi mama yake mzazi ila nilimwambia, mama huyo mwanao zamani alikuwa mpenzi wangu na pengine mume mtarajiwa ila kwa sasa namwona kama bata mweusi tu.Nimemwambia Mama yake amwambie atafute mwanamke mwingine wa kuchezea siyo mimi...siwezi kuwa kwenye mahusihano na bata asiye na utu, yaani kumbe alikuwa ni michepuko ila aliigiza maisha pindi alipokuwa na mimi?.Anywa kwa kuwa aliniona pindi naondoka kwake, nionda adhabu ya kifo.Akifa ili hali inaeleweka kwamba tupo kwenye mgogoro sintakuwa salama, laiti kama asingeniona lazima ningepanga mipango ya kwaondoa wote!!! wacha waishi ila sintarudiana naye ata kama Mbingu zitashuka kuja kutupatanisha.

MWISHO:
Nimekuja hapa jukwaani;
1.Kuwaomba radi niliowakwaza jana jioni na leo asubuhi, jamani niwieni radhi, nilikuwa na hasira juu yenu pasipo sababu.
2.Kuwaasa wanawake wenzangu kuwa makini na hawa wanaume, wachache ni wanaume ila wengi wao ni wavulana walioishi miaka mingi
3.Enyi wanaume kuweni makini mnapopewa moyo wa mtu, inauma sana kusalitiwa jama.Wanawake tu dhaifu ila siyo sababu ya kutokuwa wakatili pindi unapopita kwenye 18 zetu vibaya.

Maamuzi nimeshafanya mwenyewe KAMWE SINTOMRUDIA HUYO BATA MWEUSI, kwa hiyo siitaji kushauriwa juu ya hilo.Nimeshagombana na rafiki zangu wawili kisa shauri zisizo na umuhimu.NIMEKUJA KUWAASA TU JAMANI ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI.

Hongera, umemaliza vizuri, haka kasafari kanaweza kuwa kagumu on the way maana ulimzoea, ila jipe moyo maana ni maamuzi ya busara! sio mianaume mingine inakuja hapa kuomba ushauri wa kuacha au kutokuacha
 
Kama ndo kwanza umesalitiwa kweli inauma unaweza kuua bila kukusudia!jikaze tu ndio ya dunia sie wanaume tuna udhaifu flani kwamba ukushaona unapendwa masikio yanazidi kichwa isitoshe sie wanaume tuna kasumba moja matata sana yaani hatuna msimamo mmoja thabiti siwezi kusema huo ni udhaifu wetu ila nachohisi ni kudharau hisia za ulienae na kujikuta unamsaliti bila chembe ya kujishtukia!mwanaume kwa mwanamke ni kama mfupa kwa fisi akichekewa anafanya kweli
Word! Mkuu afadhali unajua jinsi hali halisi ilivyo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
sasa angehamiaje bila utaratibu?
Hapo katika maelezo yake kakiri hadi mama wa huyo mchumba ake anamfahamu na alienda kumwombea msamaha mwanae hivyo hawa watu walishatambulishana hadi kwa wazazi sasa walishindwa vipi kuishi pamoja huku taratibu zingine zikiendelea
 
Back
Top Bottom