Usaliti: Nusura niue mtu hii weekend

Usaliti: Nusura niue mtu hii weekend

we hapo tuu ulikua na fikra, je ungelikua unafanya action ingekuaje?? embu acha kutisha wanaume wewe, ungempiga chapombe alielewa hadi anatembea uchi lakini sio mwanaume alieko fit. sijui hata sura yako ikoje.
hatutishwi na maneno sababu tunatenda haya kwa sababu wanawake mumezidisha usaliti sana, hamuaminiki sasa. ndio maana tunasema ulimwengu wa zaman urudi maana nyie kizaz cha .com mmelaaniwa na wewe ni mmoja wapo umekutwa.
sasa ule uchungu tunaoupata na wewe utaupata.
halafu nasubiria hilo jibu nione likoje, kama ni jipya au vipi. kama waogopa ban njoo hana pm fack
Kama kuna Mungu au Shetani unayemwamini basi akukemee na kukurehemu...sina cha zaidi cha kulumbana na wewe!
 
wewe mleta mada punguza jazba, maisha hayaendi hivyo, inaonekana umepanic sana! kaa chini tula kwanza, mbona mkasa wako ni mbaya lakini si mbaya kiasi hicho? upepanic kupitiliza aisee, come down!
 
Kama kuna Mungu au Shetani unayemwamini basi akukemee na kukurehemu...sina cha zaidi cha kulumbana na wewe!
hakuna cha shetani wala nini, sisi pia wanaume tunaumizwa sana na hata ukiangalia hata lawama zinazolotwa hapa wanaaongoza ni wanaume
 
wewe mleta mada punguza jazba, maisha hayaendi hivyo, inaonekana umepanic sana! kaa chini tula kwanza, mbona mkasa wako ni mbaya lakini si mbaya kiasi hicho? upepanic kupitiliza aisee, come down!
angepigwa ukimwi huyu siangeshakua marehemu kabisa huyu! kitu kidogo ana mind hivyo
 
Guyz kuna watu mnashangaa uchumba wa miaka mitano.Hiyo ni kawaida kabisa, nimeshuhudia uchumba wa miaka 6,7,8, hadi kumi.Inategemeana na malengo na mipango ya wahusika.NAOMBA MKUMBUKE KUWA LENGO LA HUU UZI SIYO KUOMBA USHAURI, MALENGO YAKE YAPO KWENYE AYA YA MWISHO YA UZI...TAFADHALINI SANA NAWAOMBA MSITOKE NJE YA MALENGO YA MADA HUSIKA.
Dada usiwe mkali watu kushangaa uchumba miaka 5 malengo ayo malengo gani au kuchunguzana gani uko uchumba mwaka au mwaka na nusu watu mnaoana hapana aisee angekua mumeo miaka yote hyo unafkili angeleta mwanamke ndani kwenu angefanya nae uchafu wake nje halaf kingine unatakiwa ujue wanaume wote tabia zao moja lazma wacheat hakuna mwanaume wa peke ako labda umuumbe mwenywe
 
Dada usiwe mkali watu kushangaa uchumba miaka 5 malengo ayo malengo gani au kuchunguzana gani uko uchumba mwaka au mwaka na nusu watu mnaoana hapana aisee angekua mumeo miaka yote hyo unafkili angeleta mwanamke ndani kwenu angefanya nae uchafu wake nje halaf kingine unatakiwa ujue wanaume wote tabia zao moja lazma wacheat hakuna mwanaume wa peke ako labda umuumbe mwenywe
pia hakuna mwanamke wa peka yako
 
Pole sanaeeee mama. Kwa kweli huyo hakuwa ridhiki
 
hivi bata mweusi ana tabia gani nataka nimtukane mtu hapa yaweza kuwa tusi jipya la kumuumiza yule aliyekutenda na yeye akaaumia the same
 
Id yako nzuri bibie@ mjumbe wa amani uliposema bata mweusi nimejisikia kucheka balaa. nilitaka kukushauri lkn umesema hutaki ushauri wowote, ngoja nikupe pole tu kwa kuangukia kwa bata mweusi lakini ukitaka ushauri zaidi milango iko wazi unakaribishwa.
 
Nani amekuambia nahitaji mahusiano tena? hivi ni wanawake wangapi walioishi bila wanaume maisha yao yote?
Sasa hivi una hasira i know. Hakuna mtu asiyehitaji kuwa kwenye mahusiano. Itatokea tu kipindi lazima utayahitaji tena itakuwa very much maana tayari una experience ya kutosha so kuna wakati utahisi kabisa unakosa vitu fulani. Hao wanawake wengine unaowazungumzia ni kweli wapo wengi tu hawana waume ila from the bottom of their hearts wanamiss sana sema wana pretend kwamba wana furaha ili kuwavutia watu kama nyie muende kwenye life style yao, si unajua kifo cha wengi harusi.
 
NiPo bata mweupe usijal huyo bata mweus au jina maarufu huwa tunawaita bata mavi achana nae
 
Mabibi na mabwana wa JF salam!

Ni imani yangu kwamba mmekuwa na weekend njema na yenye utulivu nawapongeza sana na poleni kwa mliokumbwa na dhoruba za maisha kama mimi.Binafsi hii weekend haijawa nzuri kwangu kwani ilibaki chembe kabla sijampeleka mtu kuzimu. Mungu wangu! Pengine mida hii ningekuwa nahaha kutafuta mawakili wa kunitetea kwenye murder case.

NDUGU ZANGU IPO HIVI:
Nilikuwa kwenye mahusiano na mwanaume mmoja kwanzia jun.12 2011 hadi Ijumaa iliyopita tar.2 sep 2016. Kwakweli tulipendana mno tena sana, tulijaliana na kushirikiana kwa kila jambo, Mimi nilipenda sana, nilimjali na kumheshimu kwenye kila kitu.Hakuwa mkamilifu kwa 100% ila nilitambua hakuna haja ya yeye kuwa mkamilifu hivyo nilimpenda kwa moyo wote, nilimwona ni sehemu ya mwili na maisha yangu mimi, kwahiyo nilimjali kama ninavyojali mwili na maisha yangu mwenyewe. Mapungu ya kibinadamu aliyokuwa nayo nilijisi kama vile ni ya kwangu so nilimuweka wazi kabisa ni jinsi gani nilivyompenda.

Kuhusu yeye siwezi kueleza yote, alinipenda hadi nikajihisi kwamba nina deni kwake. He was more than a generous lover. Alinijali kwanzia nje hadi chumbani nakote huko niliridhika na kujiona nimepewa kuliko nilivyostahili.
Kwa ufupi tulikuwa na mapenzi ya dhati sana. Kwa hicho kipindi cha miaka mitano na zaidi, tulipata furaha iliyosaidia kupooza changamoto za maisha tulizo kabiliana nazo, It was like a single soul living within the two separate bodies.Wote tulikuwa na imani moja, yaani kuishi pomaja milele panapo majaaliwa ya Mungu.

MKASA WENYEWE:
Kwenye mahusiano yetu tulikuwa na mazoea ya kutoka pamoja kila ijumaa ama jumamosi kwenda sehemu nzuri ya utulivu na kuongea mawili matatu juu ya maisha yetu. Juzi ijumaa nilimpigia simu mida ya saa nane hadi tisa lakini simu yake haikupatikana. Basi nikachukua uamuzi wa kwenda kwake kumjulia hali na kama mambo yangekuwa poa basi tutoke kama kawaida yetu (kila tulipotoka tulichangia gharama, kwa jinsi nilivyompenda sikukubali kabisa abebe mzigo wote wa ghara, wakati mwingine nililipa mimi au yeye. Ulikuwa ni utamaduni wetu). Nilipita sehemu nikanunua matunda mbali mbali na ya kutosha, nilipenda sana kubeba chochote pindi niendapo kwake.

Baada ya kufika nilipatwa na mshangao pale nilipoona viatu vya kike mlangoni,nikajiuliza vitakuwa vya nani? Moja ya jibu lililonijia pengine ni ndugu yake wakike kamtembelea. Nikaingia ndani nikazidi kushangaa zaidi, sebuleni hakuna mtu na mlango upo wazi. Ghafla nikasikia kicheko cha Mwanamke chumbani, Oh my God! sikuhitaji genus aniambie nini kinaendelea ndani.Nilipatwa na kizungu zungu lakini niliweza kujimudu, nikaweka mikoba yangu chini nikatoka nje kuchungulia kwa dirishani nilichokiona sikuamini! Yani mwanaume niliyempenda kwa moyo wangu wote leo kamkumbatia mwanamke mwingine? Office mate wake wa kike? Anyway iliniuma ila sikupatwa na mshituko sababu nilishajua kilichokuwa kinaendelea jamani yasikie tu, lakini maumivu niliyohisi Mungu ndiye ajuaye.

Nilichokiamua ni kuwadelete hao wasaliti wangu kwenye uso wa dunia, kweli niliamua kuwauwa wote! Potelea mbali, liwalo na liwe. Nikaingia ndani nikachukua mikoba yangu nakuondoka ili kupanga namna nitakavyotekeleza hukumu yangu. Ile nakatiza kona mara nikasikia mtu ananiita jina, alikuwa ni huyo mwanaume akiwa kavalia pensi. Sikutaka kumsikiliza, nilichapa mwendo hadi kwenye gari na kwenda zangu hadi nyumbani. Baada ya kufika nyumbani nilikwenda moja kwa moja hadi chumbani na kulia sana, nililia kama mtoto mdogo. Hadi saa tano usiku mashavu yaliniuma, macho yalivimba na muda wote mate yalikuwa machungu mdomoni nikapitiwa na usingizi hadi asubuhi.

Sasa jana katuma watu waje kumwobea msamaha, kwamba eti amekosa nimsamehe, niliwarudisha mbio bila kujali ni kina nani alimtuma hadi mama yake mzazi ila nilimwambia, mama huyo mwanao zamani alikuwa mpenzi wangu na pengine mume mtarajiwa ila kwa sasa namwona kama bata mweusi tu. Nimemwambia mama yake amwambie atafute mwanamke mwingine wa kuchezea siyo mimi siwezi kuwa kwenye mahusihano na bata asiye na utu, yaani kumbe alikuwa ni michepuko ila aliigiza maisha pindi alipokuwa na mimi?. Anywa kwa kuwa aliniona pindi naondoka kwake, nionda adhabu ya kifo. Akifa ili hali inaeleweka kwamba tupo kwenye mgogoro sintakuwa salama, laiti kama asingeniona lazima ningepanga mipango ya kwaondoa wote, wacha waishi ila sitarudiana naye hata kama Mbingu zitashuka kuja kutupatanisha.

MWISHO:
Nimekuja hapa jukwaani;
1.Kuwaomba radhi niliowakwaza jana jioni na leo asubuhi, jamani niwieni radhi, nilikuwa na hasira juu yenu pasipo sababu.
2.Kuwaasa wanawake wenzangu kuwa makini na hawa wanaume, wachache ni wanaume ila wengi wao ni wavulana walioishi miaka mingi
3.Enyi wanaume kuweni makini mnapopewa moyo wa mtu, inauma sana kusalitiwa jama. Wanawake tu dhaifu ila siyo sababu ya kutokuwa wakatili pindi unapopita kwenye 18 zetu vibaya.

Maamuzi nimeshafanya mwenyewe KAMWE SITOMRUDIA HUYO BATA MWEUSI, kwa hiyo siitaji kushauriwa juu ya hilo. Nimeshagombana na rafiki zangu wawili kisa shauri zisizo na umuhimu.

NIMEKUJA KUWAASA TU JAMANI, ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI.

Will u marry me ??
 
Back
Top Bottom