Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.

Godbless J Lema

Arusha MP
Joined
Sep 28, 2013
Posts
92
Reaction score
2,205
Safari yetu ya kubadilisha utawala inaonekana kufika ukingoni na nifuraha ya kila Mtu mwenye hisia ya ukweli katika maisha na ninapotazama mbali sana ninaona jinsi ambavyo Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa ni bahati mbaya sana uwezi kuwaepuka katika harakati hizi lakini tukiwa makini tunaweza kuwathibiti .

Kama Chadema leo itashindwa kuwachukulia hatua wasaliti wa wazi wa kazi hii njema ni vipi Chadema itaweza kuitaka Serikali na Rais iwajibishe Viongozi wake katika ufisadi na wizi wa mamilioni ? Na Wananchi lazima wajue lengo kubwa na muhimu la Chadema kwanza liwe kubadilisha fikra na mitazamo na kuupa UMMA elimu na mamlaka na nguvu ya kusimamia Taifa lao katika kuhoji ,kudadisi na kukemea , kwani UMMA usipojua wajibu wake katika kusimamia rasilimali na Taifa lao , ukweli utabaki kuwa Nchi itabadilishwa na kufanikishwa na Jamii iliyoamua kuishi matendo dhahiri ya ukweli na haki na sio unafiki na usaliti .

Viongozi wote wa Siasa wanatokana na Jamii kwa hiyo jamii Thabiti inayo furahia UTU ni Nchi bora tutakayoijenga lakini Jamii yenye woga na hofu na Sifa itazaa Taifa lenye usaliti na Wanafiki . Usaliti na Unafiki unaliangamiza Taifa sana . Maombi na Dua za Watu wengi kuelekea 2015ni kutaka kuona Chadema inachukua Nchi , lakini Dua na Sala hizi zina Imani kubwa na Viongozi wa Chadema na sio rangi ya Chadema , hivyo ni muhimu Chadema kuchukua hatua sasa ya kusafisha Chama na kama hatua hiyo muhimu ya kuondoa Watu wenye rangi mbili italeta madhara katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwamba tunaweza tusishinde dola basi madhara hayo ni muhimu kwani lengo letu lisiwe tu kwenda Ikulu bali kubadilisha fikra ya utawala katika kutenda na kuamua .

" Ni bora Simba wakali mia moja walioko Nje kuliko nyoka mdogo mmoja aliye ndani " Chadema lazima ifanye maamuzi sasa ya kusafisha Nyumba yake la sivyo itakuja kujuta katika siku za mwisho , wasaliti wote waondolewe hasa yule Kiongozi wao kwani hakuna genge la usaliti lisilokuwa na Kiongozi , kuna Watu wengi Vijana wamekuwa wahanga na ndoto zao kupotea katika Siasa kwa sababu waliongozwa vibaya na Kiongozi mkubwa anayeratibu usaliti ndani ya Chama .

Mtu huyu wote tunamjua ni matumaini yangu Usaliti wake sasa utafika kikomo kama Chama kitaamua kuwa na busara za kutosha katika kujenga siku njema zinazokuja . Mtu huyu amefanya mambo mengi mabaya katika Chama yanayohusu usaliti na amewaponza Vijana wengi na kuangamiza ndoto zao kwa sababu ya mambo yake binafsi .

" To me, the thing that is worse than death is betrayal. You see, I could conceive death, but I could not conceive betrayal." Malcolm X



Lema Godbless - Mp
Nimefuatilia mjadala sana leo ukizingatia ilikuwa ni Jumamosi kwamba hatukuwa na kazi nyingi sana za Kibunge hasa baada ya kuanzisha mjadala unaosema " Usaliti na Unafiki unavyoliangamiza Taifa " na nimeona mjadala na nimejifunza mambo mengi sana sikumtaja Mtu ila Watu wengi wametaja majina ya Watu , sijui kwanini ? ila naendelea kutafakari , kesho nitaandika kuhusu mada inasema " UNAFIKI WA ZITTO KUHUSU POSHO " na mpaka saa nane mchana nitakuwa nimewasilisha na jambo hili halina mgogoro na kanuni za Chama kwani ni jambo liko wazi kwenye vyombo vya habari .

Asanteni

 
Godbless J Lema, na taifa wanaelewa unamlenga nani (ni msaliti yoyote ndani ya chama) najaribu kujiuliza ni msimamo wako binafsi kupambana na wasaliti katika chama ama wewe unakuja tu kuwasilisha ajenda.

However siku za karibuni nimenote ukweli kuwa CHADEMA ina kamati kubwa kabisa ambayo ni makada na watumishi wa CCM.

Je umeshindwa kulijadili hili katika vikao vya chama??? Ikiwezekana mtajane?

Chadema bila kuchora mstari, tutafika 2015 vipande vipande
 
Karibu sana JF Kamanda.

Hakuna jambo baya katika mapambano kama usaliti.CHADEMA kiliposhambuliwa katika kesi fake za Ugaidi kuna waliosimama na chama kidete katika kushinda vita ile lakini ilikua ni mpango wa Mungu kuwafichua wasaliti.Tukiendeleza harakati hizi za kupambana na CCM basi hata wale wasaliti miongoni mwetu tuwapimie kwa vipimo vile vile tunavyowapimia CCM na watawala dhalimu maana adui aliyejipenyeza ndani ya kambi ya mapambano ni hatari kuliko adui aliyeko nje

Siku hizi kuna silly excuse ya uhuru wa kutoa maoni katika kutimiza matakwa ya usalaiti.Mstari radical kabisa ndio utakaotenganisha wapambanaji na wasaliti kwa Doctrine radical.It's either you are with us or against us.No middle ground.Hata kama Dunia ni three dimension

Vijana tuungane na tusimame kidete.Anayepoteza na kuua ndoto za vijana wengi katika safari ya mapambano ni adui mkubwa wa vijana. Tumaini kubwa ni kuwa katika mapambano yoyote ukiona usaliti unazidi kuibuka ujue ukombozi unakaribia.Mitume na Manabii walisalitiwa katika harakati za ukombozi

"A nation can survive its fools and and even the ambitious but it cannot survive treason from within. An enemy at the gates is less formidable... The traitor moves amongst those within the gate freely, his sly whispers rustling through all the alleys, heard in the very halls of government itself... He rots the soul of a nation, he works secretly and unknown in the night to undermine the pillars of the city, he infects the body politic so that it can no longer resist." (Cicero)
 
Kama ni mshangao mkubwa nilio nao, ni jinsi mnavyolea mnafiki mkubwa ambaye anjidhihirisha wazi na kukichezea chama kama mwanasesere jinsi anavyotaka Shibuda.

Hakuna sababu zozote za msingi za kuendelea kuwa na Shibuda kwenye chama... Kama ni kweli alishiriki katika njama za kusingizi ugaidi ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA huyu anafaida gani kwenye chama, bora ata angekuwa akifanya hayo mambo kwa kificho lakini anafany awzi wazi na mnazidi kumchekea!
 
Huyo msaliti ni nani? Vp umeshndwa kuongea hayo kwenye vikao vya chama unakuja hapa hadharani.

Huwa naamini mijadala ktk vikao vya chama. Post ya Lema inatoa clues kwa maadui wa chama.
 
Mkuu Lema, pengine utusaidie kutupatia maana halisi ya 'Usaliti', 'Unafiki' na 'utu' kwa namna uelewavyo wewe.

Maneno haya kutoka kwako yananishangaza kidogo, kwa vigezo kuwa kwa yale unayofanya nawewe unaweza fuzu kuitewa Mnafiki na Msaliti asie na utu. Labda kama unatumia hii njia kujikosha baada ya wewe pia kutambua kuwa umeonyesha Usaliti mkubwa kwa Watanzania unaowawakilisha.

Lema inatakiwa uelewe haya;

Unatakiwa kujua kuwa hata kina KUBENEA wameshakuchoka, yeye si mmoja wa hao unaowasema? (Au woga ambao siku zote unashabikia ni sumu leo si sumu tena?), pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/547535-mh-lema-anaivuruga-chadema.html

Watanzania wengi washakushtukia, unakiruvuga chama kwa siasa zako za kishabiki na kitoto wenzetu wanaita 'armature' (an insult ukiichukulia undani wake) pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...gwe-gavana-rahisi-kusababisha-mitafaruku.html

Inawezekana unawashambulia Shibuda na Zitto kwenye bandiko hili, vipi ni kwakuwa wewe Lema unapenda sana Posho hivyo umeamua liwalo na liwe? pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...bungeni-zitto-lema-katika-vita-ya-maneno.html

Au unataka kusema hizi posho zinamaanisha Uzalendo na Utu kwa Taifa? (Are you serious??). Zitto alisha litabiri hili na kueleza wazi (hakutumia unafiki) kuwa Siasa za Posho zitasababisha mjenge chuki na mmwite majina yote mabaya! www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/299635-zitto-sijahongwa-ni-siasa-za-urais-na-hasira-za-posho.html

Au hii ndiyo step ya kwanza ya kufanya Zitto aondoke Chadema? Maana inajulikana wazi kuwa kuna mkakati wa kumkatisha tamaa Zitto aondoke CHADEMA mapema kabla mwaka haujaisha ili mpumue ndani ya chama cha watu wa Kaskazini (viongozi wa juu). Inaturudisha kule kule mnako kukataa siku zote (Udini/Ukabila).

Pole zako Lema, watanzania wa leo si mabwege!
 
Njia iliyotumika huko nyuma kudharau harakati zake lakini wakati huo tunafuatilia nyendo zake ilikuwa sahihi kabisa! Najua vikosi vyetu vya usalama vinafanya kazi yake sawa sawa sawa kabisa.

Hii ni comment yangu ya mwisho hadharani kama kiongozi! Nakushauri sana kamanda Lema, ebu haya mambo yashughulikiwe ndani ya vikao. Chonde chonde kamanda!!!
 
vikao vipo ila bado tuamini kuwa na misimamo tofauti ndani ya chamasi mbaya
ila USALITI NI DHAMBI KUBWA
 
unamawazo sahihi, mtizamo sahihi na nakuelewa vyema ILA Sidhani wewe kama kiongozi wa chama chako na mwenyekupenda maendeleo yake upo sehemu sahihi.
 
Zitto??? Shibuda??? Au Mwenyekiti wetu???? Halafu kuna mada mbili tatu zimo humu zinakuhusu mkuu.. Uwe unatutembelea na kujibu kama katibu mkuu anavyofanya bssi
 
Kwa vile hata wewe as kiongozi hujataka kumweka wazi huyo msaliti hata sisi tutabaki kumkisia tu ila kwa vile umetupa mwanga na wengi wetu tuko kwenye mkumbo kama wako wa kuhisi hisi kuwa ndiye sie, huna budi kuja na mpango mkakati wa kujitoa kimasomaso na mkumtaja huyo nyoka moja kwa moja.

Tunajua lema huogopi kitu, ukiamua kusema kitu daima dhamira yako ya ukweli hukoongoza na kusema utakacho, mimi, wewe na wengine ndani ya cdm huyu msaliti tunamjua au tunabahatisha?

Kama lengo letu na kuchukua dolla kwa nini tusifocus kwenye lengo kwanza kuliko kuanza kuboa lengo?

Kuna mda itafikia hiki chama tutakiua sisi wenye kwa unafiki wetu na wala ccm haitalaumiwa kwa hili, kama dhamira yetu ni moja bs tutimize tulichokusudia huyo nyoka tutamwajibishia kulingana na taratibu na kanuni za katiba ya chama.

Lema cc tuko nyuma yako, ukimtaja utakosha roho zetu ila si kwa lengo la kuboa bali tuendelee kujenga chama kwanza kuelekea ulikokusema wewe othewise tutaua ndoto za vijana wengi na watanzia kwa ujumla, sprit yako haiongozwi kwa kujikomba bali kwa kujitoa kupigania masilahi ya taifa.

Tukilinde chama kwa kushirikiana, hatuko ladhi kuona watu wachache wanataka kukichafua chama kwa vile tu wameahidiwa uongozi wakati wanajua hata huku waliko wananafasi kubwa ya kuwa vuongozi.
 
Mtu huyu wote tunamjua ni matumaini yangu Usaliti wake sasa utafika kikomo kama Chama kitaamua kuwa na busara za kutosha katika kujenga siku njema zinazokuja . Mtu huyu amefanya mambo mengi mabaya katika Chama yanayohusu usaliti na amewaponza Vijana wengi na kuangamiza ndoto zao kwa sababu ya mambo yake binafsi
Na watakaoibomoa CDM si wengine bali hawa ambao wamekuwa wakipima upepo tangu mwanzo. Leo nccr, kesho tlp, keshokutwa cdm...
Kila siku unatuhubiria ujasiri, unashindwa nini kumtaja huyo msaliti? Mwigamba alichukuliwa hatua kwa uzushi kwa viongozi wake. Lema is doing the same, CDM chukueni hatua before it's too late.
 
Godbless J Lema,
Mimi nakukubali katika harakati za ukombozi wa taifa hili. Lakini naomba kukushauri kitu kimoja: Katika siasa kubali kutofautiana na watu fikra. Na sio kila mara unaotofautiana nao fikra basi ni maadui zako. Ni wazi kabisa kwamba Mwenyekiti wetu Mbowe angesema nawachukulia kama maadui wale wote anaotofautiana nao kifikra, CHADEMA isingekuwa hapo ilipo.

Kila shilingi ina pande mbili. Sio sahihi kumjudge mtu kwa kuangalia weakness zake peke yake. Naamini CHADEMA imefika hapo ilipo kwa juhudi kubwa za viongozi wake WOTE na wanachama wake. Na ninaposema wote nina maana ya WOTE. Sio vyema mtu mmoja au kikundi cha watu kujiona kuwa wao ni bora zaidi ya wengine. Kila mtu anayo madhaifu yake kama alivyo na mazuri yake. Hakuna mtu aliyekamilika, sio CDM, sio CCM na sio popote.

Wanasema mbwa ukishamjua jina hakusumbui Lema.... Tafakari braza...
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom