Usalama wa ndege za Precision ukoje?

mtoa hoja ana chuki binafsi au anatumiwa na washindani wa hii biashara kuichafua precision air. Mimi ni mtumiaji mkubwa wa huduma zao, ndege zao ziko katika hali nzuri sana. Nyingi ni bado mpya na hata huduma zao ndani ni za kuridhisha. Tatizo lao ni ucheleweshaji (si mara zaote) na pia ukizidisha hata kilo moja wanakulipisha.....ie hawana uhusiano mzuri na wateja ktk mzani.

watake radhi wana jf

uliza ile mpya iliokuja juzi imepelekwa nairobi kufanya nini wiki sasa niisje zaidi??
 
hawa ndio waliokuwa nyuma ya kifo cha air tanzania na sisi tukashangilia sasa tunalalamika ndivyo sivyo!

Tulalamike air tanzania tunaitaka au tulalamike precision air inavuja? Labda tuna tatizo la kutokujuwa nini tunatakiwa kudai kwa nguvu zetu na sauti zetu zote, au wakati watu wanadai vitu vya msingi tunawaona ni wapiga kelele na wanachodai hakina uhusiano na mambo yetu kabisa.

Haya ni watunda ya ujinga wetu kuachia air tanzania ikatokomea bila kuhoji na bado tutagonga glass na kunywa whisky, wine na bia kwa kuwa hayakuwa yanatuhusu.

ndugu zanguni binafsi nina ka idea sio kidogo cha airline
kwa ukweli ulio wazi wakija inspector kutoka nje ya nchi akuna ndege itakayoruka tanzaniaa else hizi mpya zilizokuja
anyway sitaki kulalalia kwa precision maana sio tatizo lao tatizo ni tcaa..kumekuwa na kuhongana na kuandika wrong report kufurahisha airline bila kujali afya za watu...nakupa mfano tu nenda kaulize ile meli iliodondoka miezi minne iliopita imefanyiwa chks na sumatra na wamesema iko sawa leo wanadai ilikuwa na matatzo kibao so mpaka ndege zianguke ndio utasikia tcaa .....,,kama mnakumbuka kuna aliejua soln ya tatizo liliotokea ile ndege ya mwanza kuanguka nothing wamekaa kimya....na hiki ndicho kilichofanyika mv bukoba leo imehamia bahari ya zanzibar wameunda kamati ambayo tunatumia kod za wanchi tunaishia kupata laana....,,

labda nikusaidie kuna vitu vingi vinachangia kuharibika kwa ndege ikiwemo matengenezo..sasa kinachofanyika ma engineer wengi wa tanzania wamekuwa na dharau hasa wakishajua wakicancel ndege mkubwa wao atawauliza mlikuwa wapi...hili linafanya kumtia majaribuni ruban wa ndege huku sheria zikiwa wazi kuna matatizo haya inabidi ndege isiruke...m nakumbuka kuna siku rubani wa precision alishuka alipoangalia ndege ikiwa na matatizo na ma engineer wakadai inaweza kuruka ikirudi inarekebishwa ...akashuka akaondoka ceo akapigiwa akasema apelekwe ruban mwingine akaingia mkenge akairusha abiria walipofika mwanza wakarusha malalamiko ikiwemo na jf,,,ile ndege iliondoka baada ya siku 3...so unaweza jua nani wanaoua watu.....kama umesikia leo kuna ruban alishuka alipokataa kuendesha meli akaitwa mwingine akamwambia bosi wake anaileta pemba ...leo anachezea jela akisubiri kuhukumiwa kwa mauwaji

vitu vingine ni spareparts,,tumekuwa tukiwa tumia used mara kwa mara na vinapochakaa vinapelekwa mjini vinachongwa..ndugu ni shida hapa hili sio precission tu atc, na kampuni nyingi..sasa vinapochoka vikiwa juu lazima rais aende kutoa pole hapo...na afadhali meli unapatikana ndege uonekani ngo,,ndege ya precission mpya imeletwa hapa dar aikurukaa wiki iko sasa nairobi zaidi ya wikimbili ...ni aibu kusema loh!!!huko nairobi wanabadilisha spare wakirusha vinaamka vingine wamebaki management wanajiuliza ...sasa hapa ni story ndefu kuna ten percent unakuta mnaleta ndege ili mradi watukadhaa wakokwenye payroll za malipo ya ndege...sitaki kusem kaulize vituko vya atcl airbus ilipo na imekuwaje iko huko

upya wowote msidanganyike jamani..kuna watu wako huko nje kusubiri watwaahadaa vipi waafrika...ndege ya
 
Nimeguswa na hii mada. Nilipanda Precision air nikitokea Mwanza kuja Dar majira ya saa moja jioni, ilikuwa ni ATR, baada ya kusafiri kwa dakika 45 au saa moja hivi tukiwa anga la singida, nilianza kushindwa kupumua na ghafla nikaona taa za hatari zimewashwa nikajua tayari soo. rubani akatangaza kwamba ndege imepata hitilafu kwahiyo tunarejea mwanza. Baada ya kufika mwanza rubani akasema mfumo wa hewa haufanyi kazi kwahiyo angeendelea na safari basi nusu ya abiria wangepoteza maisha angani kwa kukosa hewa.

Nakumbuka sana safari hii na sitaisahau. Rubani alinikera aliposema option rahisi kwake ilikuwa ni kwenda KIA au Arusha kuliko Mwanza lakini aliogopa shirika lingetakiwa kuingia gharama kubwa kutupeleka hoteli zenye hadhi kuliko Mwanza na ndio sababu aliamua kurudi mwanza ingawa ilikuwa hatari pia. nilimuona rubani kama muuaji, shirika likatupeleka kutulaza Mwanza hoteli majira ya saa tano usiku na kesho yake asubuhi ndege ikkatengenezwa na tukaondoka kama saa tatu au nne hivi.

TCAA inabidi waifanyie ukaguzi precision na ndege zake maana ipo siku watu watapoteza maisha na hapo itaundwa TUME kuchunguza wakati tahadhari inapaswa kuchukuliwa mapema. Ni kweli Precision inaelekea kubaya now.
 
Names calling kwenye mambo ya msingi will never make a great thinker hata siku moja .Heshima mbele na angalia mie sikurupuki na jamvi hili wengine si wasema hovyo tunaweza lakini umri na heshima zetu mbele .So ukiwa hujui acha kuchangia badala ya kuwaudhi watu .
Mimi Lunyungu sina lolote la kuweza kunifanya niwe na beef na shirika hili ndege .Shirika hili nilianza kupiga kelele nalo miaka 5 nyuma .Hawasikii maana wanajua pesa yaweza kuongea na wakaendelea .Niliwahi kum face Kioko baada ya air hostess ku missbehave ndiyo siku joto ndani ya ndege ilikuwa issue kubwa mno na we were sweating kama kawaida ya watanzania hakuna aliye fungua mdomo kasoro mimi pekee .

Ndege ambazo nimepata kuna shida ya ubovu na uchakavu wa viti na hata ukiingia chooni hakifugi wala haki flash .Hakuna toilet papers na maji hayatoki kabisa .Kweli waweza kusema hii ni ndege ?

Ushahidi nakupa .Ndege ya jana PW 423 nilikuwa natoka KIA kupitia ZNZ naomba yeyote aingie ataona ninalosema kuna shimo liko wazo na choo hakina maji .Eneo linaonyesha kama kulikuwa na handle but it is no longer there na pako wazi .Nilishangaa sana sana .

Tarehe 22 August nilipanda PW 407 toka Dar kwenda Musoma then Mwanza ilikuwa inacheza bodi kwa ndani upepo unajaa na kutoka unaona kwa macho ikicheza na ukigusa iko kama uko nje bati linachezewa na upepo nilimwita crew nikamweleza akaona na akasema samahani atafikisha taarifa lakini akasema kila mara wanaeleza yote lakini wakubwa hawajali .

Ndege ya ajabu kabisa kuliko zote ilikuwa na ref hii 0031 PW 549250 hii ilikuwa sawa na daladala na sikuamini nilicho kiona hata vit nimechanika achilia mbali makelele na landing na taking off ya ajabu .

I am a frequent flier wa ndege za hapa nchini na ndege zote za Kimataifa .Ninajua ninalo sema hapa .Ukianza matusi ukaanza tuhuma nakushangaa sana sana lakini kuna siku mtakumbuka hii thread .Precision na usalama wa Watanzania tukae macho sana .Pesa kwao mbele na maisha yetu .Serikali inajua yote haya lakini kama kawaida hawajali wanangoja tume baada ya tukio .You wait and see .

Tuache matusi na tuhuma hizi ndege zina shida sana let alone ujinga wao wa huduma na dharau kwa wateja .Mie naongelea ubovu wa ndege zao so gear wala engine zao bali kitu kama choo, nk hazifai .

Ndege hizi hizi huwa zinashindwa kutua kila mara na kurudi ama KIA au Dar kwa sababu nyingi za ufundi leo mnatetea ujinga huu ?
Asilimia kubwa hapa hatujuani kwa hiyo tuna kupa heshima kutoka na maandiko yako...Ni kweli ndege za precision zina "matundu kama dala dala?"
 
Kwa wale tuliopanda boeing yao ya tarehe 11/9/2011 ilikuwa iondoke dar saa tano kamili tumeondoka saa sita na dkk ishirirni. Sasa ndani, nafasi economy ilijaa wengine wakasimama, mhudumu mmoja akatumia busara kuwahamishia wale waliokosa seat kwenda business class.
Wale amabao hawakuondoka jana yake waliletwa hapo uwanjani saa kumi asbhi na ndio tuliondoka nao hiyo saa sita na dkk ishirini.
Nawapa big up fly540 hebu igeni kwao msije mkadhani wanawaloga.
 
Tangia nimekuja hapa Nchini nimepata ndege za Precision mara kadhaa sasa .Lakini kama kawaida ndege hizi zinatisha na bado zinaruka .Najiuliza maswali mengi lakini nisema kuna tume itaundwa baada ya ajali kutokea maana ndiyo Tanzania yetu.

Ndugu zanguni kwa wale ambao mmeshawahi kutumia ndehe hizu hebu niambieni juu ya hali ya vioo kwenye ndege hizi, viti ni chakavu ile mbaya , jana nimepanda ndege ina matobo kama daladala.






Juzi nilipanda ukuta wake ukiwa unacheza kama vile waingiza upepo .Hivi kweli wana usalama wa ndege hizi wapo au wanajua ila wanafumbia macho jambo hili ?

Ndege za Precision ni kama daladala kabisa na hata huhutaji uchunguzi wa kina maana ukiingia tu unaona shida zote hizo nilizo taja hapo .Kuna moja niliwahi kupanda ikawa hata haipozi hewa na uko ngani lakini joto kama uko beach na hakuna miti ya kujikinga .

Sasa wana tatizo la delays na flight cancellation. Hakuna wa kulalamika Watanzania wanachelewa mpaka matibabu lakini wao wako kimya tu. Je tunangojea litokee jambo tuunde Tume na kusema waziri ajiuzuru ?


hapo kwenye delaying ndipo wanakera.. na sababu kubwa ni ubovu wa mara kwa mara ya ndege zao... nakumbuka kuna siku nilikuwa natoka mwanza tulichelewa zaidi ya masaa matatu kwasababu mfumo wa mawasiliano wa ndege wa ndani ulileta shida.. wakajaribu kerekebisha tukaondoka huku wakiwa hawana uhakika tukaingia dar saa 5 usiku... kesho yake nilitakiwa niende zanzibar asubuhi matokeo yake tukaenda saa sita mchana coz ndege iliyokuwa imepangwa inadaiwa ilikuwa ime expire mda wake na inatakiwa ifanyiwe cheku up ili iruhusiwe tena kuruka.. kwa mujibu wa sheria zao za anga wanavyodai.. saa ndege pekee ya waliyotegemea ni ile tuliyokuja nayo kutoka mwanza jana yake ... ambayo baadae waliamua kuacha kutoitumia kwasababu ili develop tatizo lile lile lililotokea mwanza.. ikabidid watuunganishe abiria wa arusha na zenji.. kwa dnege ya arusha.. tulishushwa kwanza zenji then wakaenda arusha.... inabidi hawa jama wajirekebishe..
 
When I brought up this topic sikuwa na maana ya kuwachafua watu hawa bali usalama wangu kwanza na si tofauti .Ndege hizi zina matatizo mno na mie siongelei delays kama wengi bali naongelea ubovu .Mtu kabisha na nimetaja ndege na namba zao go check niyasemayo then njoo bisha au niiye muongo .Nimezipanda ndege hizi na kweli kila mara naomba Mungu tu kufika salama ila kuna siku mtakuja kuona tume inaudwa wakati watu wamesha teketea kisa pesa na si maisha ya walipa kodi na wajenzi wa Nchi hii .
 
mwezi ujao wanataka ku issue IPO (shares) ku raise 28 billion kwa ajili ya kununua ndege mpya.
 
kuna moja ya jumatatu asubuhi ikitoke dar to Mtwara ilikuinavuja sehemu ya mizigo ,maana baadhi ya mizigo ililowa kabisa. ni hatari sana hizi ndege

Something must be done before it is too late. Yale majanga ya Urusi na DRC yasije tufika hapa. Hivi SUMATRA hili haliwahusu au kuna chombo kingine maalum kwa ndege?
 
nDEGE HAIWEZI KUWA IMETOBOKA MPAKA WANAPOKAA ABIRIA IKARUHUSIWA KURUKA!!!!!. HAPA KUNA CHUMVI NYINGI IMEONGEZWA MAANA MIMI NATUMIA NDEGE HIZI KILA MARA. TATIZO LAO HASA NI CANCELLETION YA SAFARI HASA WANAPOKUWA WAMEPATA WATEJA WACHACHE. nDEGE ZAO ZA ATR ZOTE NI NZURI SANA

Hilo ulilolitaja wewe ni tatizo moja tu. Kwani kama wewe hujiu hilo maana yake halipo? Don't be suppressive
 
Hujapanda daladala inaitwa 540,utagundua hiyo precisionair ina stds karibia na british airways kama sio airforce one kabisaa! Hebu muache shirima wa watu,apete!
 
Mhhhh! Inatisha sana. Hili ndio tatizo linalosababishwa na kutokuwa na chombo cha kukagua hizi ndege kila mara ili kuhakikisha zina viwango vinavyokubalika kimataifa ili ziweze kufanya safari zake toka location A hadi location B. Mpaka ndege moja ya kampuni hii ianguke na nchi kuwapoteza Watanzania wengine labda ndio macho ya wahusika kule Mawasiliano yatafunguka na kuanza ufuatiliaji. Hatuhitaji kusubiri mpaka ajali itokee.

Kama ndege hizi zina matatizo chungu nzima kama yalivyoorodheswa na muanzishaji wa uzi huu basi kwa maoni yangu hazihitaji kuruhusiwa kusafiri mpaka matatizo hayo yote yatakaporekebishwa na kufanyiwa ukaguzi na wataalam (kama tunao nchini) ili kuhakikisha wasafiri wanaotumia ndege hizi wanasafiri katika hali ya usalama.
 
Tatizo kubwa la ndege za TZ kwa uzoefu wangu ni delays (siyo PW tu hata 540 & ATC enzi za uhai wake). Ila ndege zetu so far zina record nzuri sana (nadhani sababu ni kwamba zile A, B C & D checks zinafanyika kama inavyotakiwa). Kurekebisha uchakavu wa viti, rangi, etc. ni muhimu, lakini zaidi ni kuzifanya ziwe aesthetically pleasing. Kuna mtu amewahi kupanda, e.g., Air Burkina?
 
Back
Top Bottom