Usalama wa ndege za Precision ukoje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usalama wa ndege za Precision ukoje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lunyungu, Sep 13, 2011.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Tangia nimekuja hapa Nchini nimepata ndege za Precision mara kadhaa sasa .Lakini kama kawaida ndege hizi zinatisha na bado zinaruka .Najiuliza maswali mengi lakini nisema kuna tume itaundwa baada ya ajali kutokea maana ndiyo Tanzania yetu.

  Ndugu zanguni kwa wale ambao mmeshawahi kutumia ndehe hizu hebu niambieni juu ya hali ya vioo kwenye ndege hizi, viti ni chakavu ile mbaya , jana nimepanda ndege ina matobo kama daladala.

  Juzi nilipanda ukuta wake ukiwa unacheza kama vile waingiza upepo .Hivi kweli wana usalama wa ndege hizi wapo au wanajua ila wanafumbia macho jambo hili ?

  Ndege za Precision ni kama daladala kabisa na hata huhutaji uchunguzi wa kina maana ukiingia tu unaona shida zote hizo nilizo taja hapo .Kuna moja niliwahi kupanda ikawa hata haipozi hewa na uko ngani lakini joto kama uko beach na hakuna miti ya kujikinga .

  Sasa wana tatizo la delays na flight cancellation. Hakuna wa kulalamika Watanzania wanachelewa mpaka matibabu lakini wao wako kimya tu. Je tunangojea litokee jambo tuunde Tume na kusema waziri ajiuzuru ?
   
 2. F

  Fred Otieno Member

  #2
  Sep 13, 2011
  Joined: Apr 8, 2007
  Messages: 17
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  kuna moja ya jumatatu asubuhi ikitoke dar to Mtwara ilikuinavuja sehemu ya mizigo ,maana baadhi ya mizigo ililowa kabisa. ni hatari sana hizi ndege
   
 3. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu mimi sijawi kupanda ndege za Precision ngoja ni subiri maoni ya watu wengine,ili niweze kuchambua pumba ni zipi na mchele ni upi..kama ni chuki binafsi au ni kwa manufaa ya taifa.

  Nina assume umeshapeleka haya malalamiko head office yao,wao wanasemaje?
   
 4. k

  kinyongarangi Member

  #4
  Sep 13, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nDEGE HAIWEZI KUWA IMETOBOKA MPAKA WANAPOKAA ABIRIA IKARUHUSIWA KURUKA!!!!!. HAPA KUNA CHUMVI NYINGI IMEONGEZWA MAANA MIMI NATUMIA NDEGE HIZI KILA MARA. TATIZO LAO HASA NI CANCELLETION YA SAFARI HASA WANAPOKUWA WAMEPATA WATEJA WACHACHE. nDEGE ZAO ZA ATR ZOTE NI NZURI SANA
   
 5. a

  alles JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 14, 2006
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  October 2010 nilishawai kuwapelekea malalamiko kwenye ofisi zao pale NIC Building/Samora kuhusu cancellation za safari na kuhusu viti chakavu. wakadai watashughulikia. Tena wanakujibu kwa dharau kuonyesha kwamba hakuna alternative kwa local transport lazima utumie usafiri wao hata kama upendi. Natumaini moja ikianguka na kuua watu kadhaa may be watasikia.
   
 6. Bundewe

  Bundewe JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pamoja na kwamba kuna kachumvi kidogo kameongezwa, lakini hawa jamaa sasa hivi wanaboa. Nadhani tatizo lao kubwa ni huduma duni na poor customer care. issue za ku overbook kwao ni za kawaida. Unakuta ndege in excess ya abiria 8. Tumewahi kuachwa KIA kuanzia saa moja usiku mpaka saa 7 usiku, maana ndege yetu ya saa 1 ili overbook. Hawa jamaa ni kama tanesco, wana ukiritimba kwa sasa.
   
 7. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtoa hoja ana chuki binafsi au anatumiwa na washindani wa hii biashara kuichafua Precision Air. Mimi ni mtumiaji mkubwa wa huduma zao, ndege zao ziko katika hali nzuri sana. Nyingi ni bado mpya na hata huduma zao ndani ni za kuridhisha. Tatizo lao ni ucheleweshaji (si mara zaote) na pia ukizidisha hata kilo moja wanakulipisha.....ie hawana uhusiano mzuri na wateja ktk mzani.
   
 8. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu ulipanda ndege ya kwenda wapi wasema nzuri.Je ukiwa kwenye ndege hizo abiria watakiwa kuusikia mngurumo wa ndege.Haweza kuwa na ndege nzuri 2 kati ya 8 wategemea nini hapo.Je service ya ndege hizo.Ukweli kiama kingine chaja.Je wajuwa ndege wanazoitwa mpya zimetengenezwa lini na huko zilikotoka zimetumika kwa muda gani.Tatizo tumezoeya mitumba sasa kila kitu Tanzania ni mitumba
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Wanacancel safari halafu wanadanganya watu kuna matatizo ya kiufundi. Khaa!
   
 10. SenBoy

  SenBoy Member

  #10
  Sep 13, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 15
  Hapana ndugu yangu usimuhukumu mtoa hoja, ni kweli kabisa kabisa kuna baadhi ya ndege ambazo ni zile za mwanzo kabisa, usalama wake ni mdogo sana. zile ndege ni chakavu sana, hata mie nilipanda moja mwaka jana ilikuwa inapitia Musoma, ilikuwa inahangaika hata kufunga matairi, viti vilikuwa ni chakavu sana. kama wewe ni msafiri wa Mza Dar hutoweza kuzijua, ila waendao Mtwara, Musoma Shinyanga na kwingineko kusiko na abiria wengi watakuwa wanazijua.
   
 11. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Je nani anasikia hili.?
  Nashukuru ujumbe umefika mkuuu.
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Hili ni bomu, tunangoja lipasuke na kupoteza roho za watu ndipo tutaunda tume ambnayo hatutawatangazia tume imegundua nini. Na baada ya hapo tutaendelea na shughuli nyingine za kichama na serikali bila mtu yeyote kuchukuliwa hatua. Hii ndiyo hali halisi ya Tz
   
 13. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Ni kweli hizo ndege zina matobo kama dala dala au mleta hoja ni mwongo?
   
 14. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Mi sio Mpenzi wa hizo ndege ni bora nipande basi kuliko ku-risk maisha yako na hizo ndege za mitumba
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  hahahaha! Mwongo.
   
 16. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mimi nimepanda hizo ndege hakuna hilo tatizo,na huyu mtu naona anajichanganya au ni ndoto nini?
  kwa sababu watu wengine wanapanda madaladala kutwa nzima akifika nyumbani kwa sbb ya uchovu anaanza kuota amepanda ndege.
   
 17. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Wandugu ni vizuri kuchukua tahadhali kabla ya ajali. Tunakubali kwamba Precion wamejitahidi kutoa huduma hata hiyo finyu ambayo Air Tanzania wameshindwa. Lakini ni vyema pia kuangalia Usalama wa wasafiri na haki zao za msingi za customer care.Hivi hakuna vyombo vya kuchunguza makampuni haya mara kwa mara na kuwana kama bado wankidhi viwango? Nauliza
   
 18. M

  Mfwalamanyambi JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 434
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mara yangu ya kwanza kusafiri na ndege ilikuwa ni Precision Air toka Dar hadi KIA kwa kweli sikutambua tatizo lolote. Lakini mara ya pili nilipanda South African Airways toka Dar-Joh'berg hapo ndipo nikaweza kulinganisha ubora wa ndege na kugundua mapungufu ya precision air. Hata hivyo tushukuru kwa hili shirika kuwepo maana nchi yetu haina hata ndege moja.
   
 19. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Kampuni ya Precisionair kuingiza ndege saba mpya Tanzania

  Na Andrew Msechu

  KWA mara ya kwanza nchini, Kampuni ya Precision Airlines imeingiza ndege moja mpya kati ya saba aina ya ATR 72-500, ikiwa ni sehemu ya mkataba wa Dola za Kimarekani 129milioni (zaidi ya Sh150 bilioni).


  Ndege hiyo ni sehemu ya mkataba ambao ulisainiwa hivi karibuni kati ya Precision na Kampuni ya ATR ya Toulouse, nchini Ufaransa kwa ajili ya kuingiza ndege saba mpya na vifaa vya ndege za ATR kwa nchi zote za Afrika.


  Akizindua ndege hiyo kwa niaba ya Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge jana, Kaimu Mkurugenzi wa Usafirishaji katika wizara hiyo, Kirenga Ndomino alisema hatua hiyo ya Precision, ni changamoto mpya katika sekta ya usafiri wa anga nchini, hasa katika kuimarisha sekta ya uzalishaji na utalii wa ndani.


  Ndomino alisema uamuzi wa Precision kuingia mkataba huo mkubwa zaidi kati ya Precision na ATR ambao haujawahi kusainiwa na kampuni yoyote binafsi ya ndege nchini, hasa kwa ajili ya kuingiza ndege mpya saba ndani ya miaka mitatu, ni mfano wa kuigwa katika juhudi za kuboresha sekta ya usafirishaji wa anga nchini.


  "Hii si ndege ya kwanza kuzinduliwa na Precision, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa hii ni kampuni ya kwanza kuingiza ndege mpya nchini, pia imeweka historia ya kuwa kampuni ya kwanza Afrika Mashariki na kati kuagiza ndege mpya kutoka kiwandani baada ya kampuni ya Kenya Airways. Kampuni nyingine zimekuwa zikitumia ndege zilizokwishatumika," alisema Ndomino.


  Aliongeza kuwa kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kuboresha sekta ya usafirishaji wa anga nchini, serikali inaendeleza juhudi za kufanya maboresho makubwa kwenye viwanja vya ndege nchini kwa kuanza kwa awamu ya pili ya ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Kiamataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, kuanzia mwezi ujao kwa gharama ya zaidi ya Euro25 milioni.


  Kaimu Mkurugenzi huyo alisema ukarabati huo unaodhaminiwa na Benki ya Dunia, pia utaviwezesha viwanja vingine saba vya Arusha, Mafia, Bukoba, Shinyanga, Tabora, Kigoma na Sumbawanga kufanyiwa ukarabati mkubwa, mradi ambao tayari umeshaanza.


  Mkurugenzi wa kampuni ya Precision, Alphonse Kioko alisema uamuzi wa kuwapo kwa sasa usafiri wa anga nchini unaweza kuwa rahisi zaidi kutokana na uamuzi wao wa kuingiza ndege mpya kutoka kiwandani, ambazo zitahakikisha usalama na mazingira mazuri zaidi kwa wateja na wao.


  "Siku hii ya leo si ya kawaida kwetu, ni siku mpya katika utaratibu mzima wa utoaji wa huduma kwa wananchi wa Tanzania, tuna uhakika wa kuwahakikishia huduma bora zaidi, kwa haraka na raha zaidi, tunawashukuru wadau wetu wote waliotuwezesha kufika hapa tulipo leo" alisema Kioko.


  Akizungumza katika makabidhiano ya ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 70, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Precision, Michael Shirima alisema ndege hiyo inaungana na ndege nyingine nne za Precision ambazo zinaendelea kufanya kazi nchini.


  "Tunaamini kuwa kutokana na uhusiano mzuri uliopo baina ya Precision na serikali na wateja wake ni moja ya sababu kubwa ya kutufanya tuwepo hapa leo, pia uthabiti wa ndege hizi za ATR unatufanya tujisikie fahari ya kuwakaribisha na kuwahakikishia usalama na raha kila mnaposafiri na sisi," alisema Shirima.


  Kampuni hiyo iliyoanzishwa mwaka 1996 pia inatarajia kuingiza ndege nyingine aina ya Boeing 737-300 mwishoni mwa mwezi huu, pia imethibitishwa na Shirika la Viwango vya Usalama wa Anga Duniani na kuwa mwanachama wa IOSA.
   
 20. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Hapo Kwenye RED Shirika letu halija shindwa ila limefilisiwa na Mataka pamoja na Viongozi wa Serikali na Precions walikuwa waiba Spare kwenye Ndege zetu, hao ndio waliochangia kufa kwa Shirika letu
   
Loading...