Usalama wa ndege za Precision ukoje?

Usalama wa ndege za Precision ukoje?

Nimesafiri nao mara kadhaa wanajitahidi na wamefanya vizuri kipindi hiki Air Tz ni mfu.lakini ubora wa ndege zao kweli unatia shaka sana na sijui kama serikali yetu imeweka mainjinia kuhakiki usalama wa abiria muda wote?

Dola milioni 129 wakaletewa ndege zenye matundu!!!

Ushauri tuu kama kuna mtu anadhani ndege za Precisionair siyo "Airworthness" aripoti tuu kwa mamlaka husika tusingoje kuja kupeperusha bendera ya Taifa nusu mlingoti. Lakini nachelea kukubaliana na wengi wenu kwani ndege zinakaguliwa kimataifa na kila baada ya masaa fulani lazima engine, body, landing gears nk. zifanyiew maintenance ndiposa zipewe kibali cha kuendelea kuruka

Hapana ndugu yangu usimuhukumu mtoa hoja, ni kweli kabisa kabisa kuna baadhi ya ndege ambazo ni zile za mwanzo kabisa, usalama wake ni mdogo sana. zile ndege ni chakavu sana, hata mie nilipanda moja mwaka jana ilikuwa inapitia Musoma, ilikuwa inahangaika hata kufunga matairi, viti vilikuwa ni chakavu sana. kama wewe ni msafiri wa Mza Dar hutoweza kuzijua, ila waendao Mtwara, Musoma Shinyanga na kwingineko kusiko na abiria wengi watakuwa wanazijua.

Inawezekana wanatumia ndege nzuri kwa baadhi ya route, sijawahi kusafiri nao kwenda Musoma, Mtwara au Shinyanga. Lakini kwa route ya Dar-Kia-Entebbe-Zanzibar, wanatumia ATR-72 zenye hali nzuri. Pia nakumbuka ndege hizi zilinunuliwa zikiwa mpya.

Ni kweli hizo ndege zina matobo kama dala dala au mleta hoja ni mwongo?
Mleta hoja muongo kwa kweli. Miye nimepanda mara nyingi sana. Mwz - BK- Mwz, Mwz-Dar- Mwz, hata ile ya Mwz- Nairobi ni nzuri sana.
Suala hapa ni customer care! nitaungana na wenzangu kuhusu customer care mbovu. hasa cancellations na ucheleweshaji.
Wanajaribu kama ndege pekee zilizo angani TZ kwa wingi.

nafikiri badala ya kubishana hapa,taarifa hizi zingewasilishwa kwa wahusika kuchunguza tuhuma hizi..kwasababu kama ni kweli basi ni bomu linalosubiri kulipuka na kuchukua roho za ndugu zetu

Hawa ndio waliokuwa nyuma ya kifo cha Air Tanzania na sisi tukashangilia sasa tunalalamika ndivyo sivyo!

Tulalamike Air Tanzania tunaitaka au tulalamike Precision Air inavuja? Labda tuna tatizo la kutokujuwa nini tunatakiwa kudai kwa nguvu zetu na sauti zetu zote, au wakati watu wanadai vitu vya msingi tunawaona ni wapiga kelele na wanachodai hakina uhusiano na mambo yetu kabisa.

Haya ni watunda ya ujinga wetu kuachia Air Tanzania ikatokomea bila kuhoji na bado tutagonga glass na kunywa whisky, wine na bia kwa kuwa hayakuwa yanatuhusu.

Nilisafiri nayo kwenda Nairobi mwaka jana yaani nilikaa tokea asubuhi hadi nilikuja kusafiri saa 11 jioni ningali na watoto wadogo nimeichukia sana wana huduma mbovu kupita maelezo

...eeh mungu,nijalie na mimi nipande ndege,hasa hizo ili niweze kuchangia katika hili...!!

October 2010 nilishawai kuwapelekea malalamiko kwenye ofisi zao pale NIC Building/Samora kuhusu cancellation za safari na kuhusu viti chakavu. wakadai watashughulikia. Tena wanakujibu kwa dharau kuonyesha kwamba hakuna alternative kwa local transport lazima utumie usafiri wao hata kama upendi. Natumaini moja ikianguka na kuua watu kadhaa may be watasikia.

Hilo ndilo jibu.

na sisi ambao hatujawahi panada ndege si ndo itakuwa ishu kupanda kama mamboa yenyewe ndio hayo

Mtoa hoja ana chuki binafsi au anatumiwa na washindani wa hii biashara kuichafua Precision Air. Mimi ni mtumiaji mkubwa wa huduma zao, ndege zao ziko katika hali nzuri sana. Nyingi ni bado mpya na hata huduma zao ndani ni za kuridhisha. Tatizo lao ni ucheleweshaji (si mara zaote) na pia ukizidisha hata kilo moja wanakulipisha.....ie hawana uhusiano mzuri na wateja ktk mzani.

Ukizidisha hata kilo moja wanakulipisha kama njia ya ku-discourage usibebe zaidi ya uzito unaoruhusiwa. Ikumbukwa kuwa ndege za ATR hazina capacity kubwa, sana sana ni maximum abiria 70 kwa ile ya ATR72 na abiria kama hamsini hivi kwa ATR42. Kutokana na size ya hizi ndege suala la maximum take-off weight linazingatiwa mno ili kuepusha rubani kuendesha ndege iliyopitiliza uzito na hivyo kusababisha risk na kutumia mafuta mengi zaidi.

Hapo Kwenye RED Shirika letu halija shindwa ila limefilisiwa na Mataka pamoja na Viongozi wa Serikali na Precions walikuwa waiba Spare kwenye Ndege zetu, hao ndio waliochangia kufa kwa Shirika letu

Mmmhhh ndege za Precision Air za mwanzo zilikuwa LET 410 halafu wakaanza kutumia ATR ndipo wakaongeza Boeing 737. ATC hawajawahi kuwa na ndege zinazofanana na za Precision Air, hata Boeing yao ni ya kisasa kidogo kuliko zile za ATC, sasa spea waliiba ili zitumike wapi wakati ndege hazifanani?

Tangia nimekuja hapa Nchini nimepata ndege za Precision mara kadhaa sasa .Lakini kama kawaida ndege hizi zinatisha na bado zinaruka .Najiuliza maswali mengi lakini nisema kuna tume itaundwa baada ya ajali kutokea maana ndiyo Tanzania yetu .Ndugu zanguni kwa wale ambao mmeshawahi kutumia ndehe hizu hebu niambieni juu ya hali ya vioo kwenye ndege hizi, viti ni chakavu ile mbaya , jana nimepanda ndege ina matobo kama daladala .Juzi nilipanda ukuta wake ukiwa unacheza kama vile waingiza upepo .Hivi kweli wana usalama wa ndege hizi wapo au wanajua ila wanafumbia macho jambo hili ? Ndege za Precision ni kama daladala kabisa na hata huhutaji uchunguzi wa kina maana ukiingia tu unaona shida zote hizo nilizo taja hapo .Kuna moja niliwahi kupanda ikawa hata haipozi hewa na uko ngani lakini joto kama uko beach na hakuna miti ya kujikinga .

Sasa wana tatizo la delays na flight cancellation .Hakuna wa kulalamika Watanzania wanachelewa mpaka matibabu lakini wao wako kimya tu.Je tunangojea litokee jambo tuunde Tume na kusema waziri ajiuzuru ?

......not to mention ndege zao nyingi ni za propellers na hivi karibuni nime-experience long delays ya flights zao kama mara 5. Mara nyingi kama kuna alternatives huwa sipandi PW

Tangia nimekuja hapa Nchini nimepata ndege za Precision mara kadhaa sasa .Lakini kama kawaida ndege hizi zinatisha na bado zinaruka .Najiuliza maswali mengi lakini nisema kuna tume itaundwa baada ya ajali kutokea maana ndiyo Tanzania yetu .Ndugu zanguni kwa wale ambao mmeshawahi kutumia ndehe hizu hebu niambieni juu ya hali ya vioo kwenye ndege hizi, viti ni chakavu ile mbaya , jana nimepanda ndege ina matobo kama daladala .Juzi nilipanda ukuta wake ukiwa unacheza kama vile waingiza upepo .Hivi kweli wana usalama wa ndege hizi wapo au wanajua ila wanafumbia macho jambo hili ? Ndege za Precision ni kama daladala kabisa na hata huhutaji uchunguzi wa kina maana ukiingia tu unaona shida zote hizo nilizo taja hapo .Kuna moja niliwahi kupanda ikawa hata haipozi hewa na uko ngani lakini joto kama uko beach na hakuna miti ya kujikinga .

Sasa wana tatizo la delays na flight cancellation .Hakuna wa kulalamika Watanzania wanachelewa mpaka matibabu lakini wao wako kimya tu.Je tunangojea litokee jambo tuunde Tume na kusema waziri ajiuzuru ?
Mwaka huu mwezi January nilipanda hiyo Precision kwenda Mwanza tiketi ikiwa kwenda nakurudi,niliyoyaona ilibidi wakati wa kurudi ni rudi na basi na nikasamehe hiyo nauli yangu,hilo ni jeneza linalopaa,ni sawa na zile ndege za DRC(kwa waliofika na kupanda ndege za DRC zikiwa zinasafiri usafiri wa ndani)

Names calling kwenye mambo ya msingi will never make a great thinker hata siku moja .Heshima mbele na angalia mie sikurupuki na jamvi hili wengine si wasema hovyo tunaweza lakini umri na heshima zetu mbele .So ukiwa hujui acha kuchangia badala ya kuwaudhi watu .
Mimi Lunyungu sina lolote la kuweza kunifanya niwe na beef na shirika hili ndege .Shirika hili nilianza kupiga kelele nalo miaka 5 nyuma .Hawasikii maana wanajua pesa yaweza kuongea na wakaendelea .Niliwahi kum face Kioko baada ya air hostess ku missbehave ndiyo siku joto ndani ya ndege ilikuwa issue kubwa mno na we were sweating kama kawaida ya watanzania hakuna aliye fungua mdomo kasoro mimi pekee .

Ndege ambazo nimepata kuna shida ya ubovu na uchakavu wa viti na hata ukiingia chooni hakifugi wala haki flash .Hakuna toilet papers na maji hayatoki kabisa .Kweli waweza kusema hii ni ndege ?

Ushahidi nakupa .Ndege ya jana PW 423 nilikuwa natoka KIA kupitia ZNZ naomba yeyote aingie ataona ninalosema kuna shimo liko wazo na choo hakina maji .Eneo linaonyesha kama kulikuwa na handle but it is no longer there na pako wazi .Nilishangaa sana sana .

Tarehe 22 August nilipanda PW 407 toka Dar kwenda Musoma then Mwanza ilikuwa inacheza bodi kwa ndani upepo unajaa na kutoka unaona kwa macho ikicheza na ukigusa iko kama uko nje bati linachezewa na upepo nilimwita crew nikamweleza akaona na akasema samahani atafikisha taarifa lakini akasema kila mara wanaeleza yote lakini wakubwa hawajali .

Ndege ya ajabu kabisa kuliko zote ilikuwa na ref hii 0031 PW 549250 hii ilikuwa sawa na daladala na sikuamini nilicho kiona hata vit nimechanika achilia mbali makelele na landing na taking off ya ajabu .

I am a frequent flier wa ndege za hapa nchini na ndege zote za Kimataifa .Ninajua ninalo sema hapa .Ukianza matusi ukaanza tuhuma nakushangaa sana sana lakini kuna siku mtakumbuka hii thread .Precision na usalama wa Watanzania tukae macho sana .Pesa kwao mbele na maisha yetu .Serikali inajua yote haya lakini kama kawaida hawajali wanangoja tume baada ya tukio .You wait and see .

Tuache matusi na tuhuma hizi ndege zina shida sana let alone ujinga wao wa huduma na dharau kwa wateja .Mie naongelea ubovu wa ndege zao so gear wala engine zao bali kitu kama choo, nk hazifai .

Ndege hizi hizi huwa zinashindwa kutua kila mara na kurudi ama KIA au Dar kwa sababu nyingi za ufundi leo mnatetea ujinga huu ?

nDEGE HAIWEZI KUWA IMETOBOKA MPAKA WANAPOKAA ABIRIA IKARUHUSIWA KURUKA!!!!!. HAPA KUNA CHUMVI NYINGI IMEONGEZWA MAANA MIMI NATUMIA NDEGE HIZI KILA MARA. TATIZO LAO HASA NI CANCELLETION YA SAFARI HASA WANAPOKUWA WAMEPATA WATEJA WACHACHE. nDEGE ZAO ZA ATR ZOTE NI NZURI SANA

Katumwa huyu, mie nilifikia hatua ya kuwaandikia emeil ya pongezi kwa huduma na ubora wa ndege nilivyouona, wameboresha huduma ndege zao ni safi, kama nitamuunga mkono ni ile moja tu kubwa iendayo Nairobi, kidogo inaonekana imechoka. zile zingine zote mimi nazifagilia na sasa wamenunua nyingne kubwa kwanda Bondeni. big up precision mnatutoa kimasomaso.

Mi sio Mpenzi wa hizo ndege ni bora nipande basi kuliko ku-risk maisha yako na hizo ndege za mitumba

SWALA HAPA SI MAPENZI,SOMETIMES U HAVE TO,SABABU ZA KIKAZI,SWALA NI KWANINI WANAHATARISHA MAISHA YA WATZ JANA MELI JUZI BASI LEO KANDEGE HUKO MEYA!AND SOON HIZO PRESISSION,WHATS WRONG WITH OUR GOVERNMENT?WANANGOJA WATU WAPOTEZE MAISHA NDO TUME TUME TUME,KWANINI WASIANZE TUME SASA?

Nimesafiri mara kwa mara na Precision sijaona matatizo ya kiufundi (MIMI SI FUNDI ) naona ndege zao ni nzuri na nyingi ATR ni mpya sasa hayo mengine labda tupate ufafanuzi wa wataalamu sio abiria

Nimesafiri mara kwa mara na Precision sijaona matatizo ya kiufundi (MIMI SI FUNDI ) naona ndege zao ni nzuri na nyingi ATR ni mpya sasa hayo mengine labda tupate ufafanuzi wa wataalamu sio abiria

Poor customer service by the ground staff and flight attendants, arrogant management, dilapilated and outdated fleet of ATR aircrafts and constant flight delays etc
PW should change their name to "Imprecission Air"
Can't wait for ATC's grand comeback!!

Back
Top Bottom