Asante mkuu
Konda wa bodaboda kwa kunialika.
ndugu
Charles Mkubya,
Kuhusu Rwanda mimi siko "negative" wala "positive" huwa niko objective. Na ndio maana wewe mwenyewe umenisifia kuwa huwa nakuja na data. Mtu anayeongea na data (jumlisha na experience ya kukaa huku na kufanya kazi kwa miaka kadhaa) hawezi kuwa biased hata siku moja. Tofautisha na mtu aliyepita pita kigali kama mtalii.
Kwa bahati mbaya na Tanzania huyu nanihii kaanza kuiga system ya uongozi wa Rwanda. Kwa hiyo siku hizi wala sina maneno mengi sana ya kumuelezea mtu kama wewe juu ya the lie which is Rwanda kwa kuwa hayo "maendeleo" unayoyatamani huyu wa kwetu atatuletea kabla ya 2020!
Kwa mfano serikali inasema HAKUNA NJAA, mapolisi wakadakia kuwa atayesema kuna njaa atatiwa ndani! watu wakiwa objective kwa kutumia data za chakula kuonyesha kuna njaa watapewa kesi za uchochezi! Ndio maana watu pekee mnaotumia real IDs ni watu wenye habari "positive" tu kama wewe ambao njaa mtaita "upungufu wa chakula". Sasa tuje kwenye reality ambayo mtu yoyote anayeishi bongo anajua je tuna njaa hatuna njaa? Zingatia kuwa sheria ya Takwimu hairuhusu takwimu zingine zisizo official kwa hiyo officially HAKUNA. Njoo kwenye chanjo basic kabisa za wajawazito mahospitalini, nenda kwenye mikopo ya elimu, rudi kwenye bajeti ya maendeleo n.k vitu vyote hivyo, ukweli halisi on the ground unapishana na maelezo "positive" ya serikali. Ukishabana uhuru wa media, uhuru wa expression/free speech, utapata "maendeleo" tu lakini ni maendeleo hewa!
sasa huu "uchwara" ambao sisi ndio tunaletewa sasa hivi huko Rwanda Kagame kawaletea toka 1994, kwa hiyo wenzetu hawa ni experts kwenye huu ubashite! Ndio maana kila siku nauliza swali lisilo na majibu kutoka kwa watu kama wewe, kuwa wanyarwanda wanakimbiaga nini huko? Same thing in Ethiopia, ukienda huko utakutana na "maendeleo" makubwa sana ambayo hata rais wetu atatuletea, shirika la ndege ethiopian airlines, mabarabara ya juu na chini, usalama, usafi n.k, lakini haipiti wiki unasikia wamekamatwa waethiopia bongo wanakimbilia sauzi. Why?
Ni kweli kigali ni safi, but ni safi kwa sababu wanataka usafi au ni safi kwa sababu ya show off? Usafi wa kupiga marufuku watu wasiopendeza wasikanyage mjini ndio usafi unaoutaka? Kuna barabara moja jina limenitoka ilipigwa lami watu (commoners) wakawa wanaogopa wanapita pembeni. Ni kwa sababu moyoni mwao wanajua hivi vitu ni kwa ajili ya international community kama sisi na sio wao.
Uhalifu kigali upo tena ule wa kishamba ambao sisi tulishavuka siku nyingi, ule wa kuvamia nyumba kuja kuiba makochi na redio! Of course mimi na wewe most likely tunakaa neighborhood nzuri utasema hakuna crime kabisa! Hata bongo ukifikia masaki hutasikia panya road!
Pita huku kwa hayo:
Hao wanajeshi wanaomwaga kigali kuanzia jioni ni kwa ajili ya kulinda Kagame asipinduliwe na sio kwa ajili ya wanyarwanda. Kama wewe unaona kuna amani katika nchi ambayo kila siku wanajeshi wako mtaani na masilaha mazito basi sawa.
My friend kiufupi sisi wageni ndio tunaopiga hela hapa Rwanda na kuona maisha ya Rwanda ni mazuri (lakini expensive), wenyewe wanapata shida lakini hawana pa kusemea. Ni mtazamo tu lakini.