Charles Mkubya
JF-Expert Member
- Aug 27, 2009
- 206
- 159
Kwanza nianze na kusema kwamba, katika Marais naowaheshimu na kutamani kuwaona wakifanikiwa, basi huyu ni mojawapo.
Niko Kigali kwa muda, mambo niliyoyaona kwa muda mchache niliokaa hapa yanatosha kuelezea aina ya uongozi katika nchi hii.
Jambo kubwa ambalo nimelipenda sana ni usalama katika mji huu..sina hakika na kwingineko lakini kwa hapa Kigali, maafisa wa polisi na jeshi wako active 24 hours na hakuna wizi, uporaji au uhalifu kwa ujumla. Kwa ufupi ni sehemu ambayo waweza kuishi bila wasiwasi kuhusu usalama wako kama raia au mgeni.
Kiuchumi, ni nchi inayokua kwa haraka japo siwezi kuelezea kiundani sababu sina utafiti lakini ukiangalia tu projects, barabara, na services zingine zinatosha kukupa picha ya Rwanda kwa miaka ijayo.
Hivyo, binafsi na kwa niaba ya watu wanaoipenda Rwanda, niseme tunaona kazi kubwa mnayoifanya Wanyarwanda katika kuijenga nchi yenu chini ya Rais Kagame, na matunda yanaonekana, hivyo tunawatia moyo kwa umoja na uchapa kazi mlionao, na mwisho nimpongeze Rais wenu kwa kazi nzuri anayofanya..japo mimi sio mwanasiasa, lakini kuna vitu vingi nimejifunza toka kwake.