Usalama na maendeleo ya Rwanda chini ya Rais Kagame

Usalama na maendeleo ya Rwanda chini ya Rais Kagame

Kwanza nianze na kusema kwamba, katika Marais naowaheshimu na kutamani kuwaona wakifanikiwa, basi huyu ni mojawapo.
Niko Kigali kwa muda, mambo niliyoyaona kwa muda mchache niliokaa hapa yanatosha kuelezea aina ya uongozi katika nchi hii.
Jambo kubwa ambalo nimelipenda sana ni usalama katika mji huu..sina hakika na kwingineko lakini kwa hapa Kigali, maafisa wa polisi na jeshi wako active 24 hours na hakuna wizi, uporaji au uhalifu kwa ujumla. Kwa ufupi ni sehemu ambayo waweza kuishi bila wasiwasi kuhusu usalama wako kama raia au mgeni.

Kiuchumi, ni nchi inayokua kwa haraka japo siwezi kuelezea kiundani sababu sina utafiti lakini ukiangalia tu projects, barabara, na services zingine zinatosha kukupa picha ya Rwanda kwa miaka ijayo.

Hivyo, binafsi na kwa niaba ya watu wanaoipenda Rwanda, niseme tunaona kazi kubwa mnayoifanya Wanyarwanda katika kuijenga nchi yenu chini ya Rais Kagame, na matunda yanaonekana, hivyo tunawatia moyo kwa umoja na uchapa kazi mlionao, na mwisho nimpongeze Rais wenu kwa kazi nzuri anayofanya..japo mimi sio mwanasiasa, lakini kuna vitu vingi nimejifunza toka kwake.
Wizi wa madini ya wacheza ndombolo, proceeds ndio zinajenga Rwanda
 
Hakika inatia moyo wenzetu wanacho cha kujivunia katika maendeleo ya nchi yao.
Uko maeneo gani mkuu?.Niko mitaa ya Remera hapo maeneo ya Hilltop hotel jirani na uwanja wa ndege Kigali.
Lingine la kufurahisha ni ule msitu wa NYUNGWE jinsi unavyolindwa katika nyanja zote za usalama na usafi wa mazingira.
 
Hakika inatia moyo wenzetu wanacho cha kujivunia katika maendeleo ya nchi yao.
Uko maeneo gani mkuu?.Niko mitaa ya Remera hapo maeneo ya Hilltop hotel jirani na uwanja wa ndege Kigali.
Lingine la kufurahisha ni ule msitu wa NYUNGWE jinsi unavyolindwa katika nyanja zote za usalama na usafi wa mazingira.

Niko maeneo haya haya mkuu, KG 173 st
 
Sawa mkuu waambie jamaa huko nyumbani kwamba tunalo la kujifunza kutoka Rwanda.

Hawawez elewa nyumban mana wako na bashiiiii mda huu ndio utajua kua Tz wajinga weng tho wanasema rwanda ndogo sasa Hyo Kongo ambayo n kubwa na ndo nchi yenye rasilimali kubwa africa ambayo ijachimbwa iko wap.Kua mtanzania n kaz kweli kweli
 
Wizi wa madini ya wacheza ndombolo, proceeds ndio zinajenga Rwanda

Mbona humsemi America kajaza wanajesh wa Monusco unajua kaz yao au unadhan wanawapaka poda madada wa kikongo au ndio ubongo ako una giza JK alipeleka JWTZ east DRC unajua kaz yao au ndio Na wewe ile coca cola nanhii.
 
Wastani wa pato la taifa (GDP) kwa mwaka ni
Rwanda 723 dola za Marekani
Tanzania 960 dola za Marekani

Rwanda kiuchumi ya kawaida tu.
Ukifuata takwimu kwa nchi hizi za kwetu utaingia chaka hasa kwa Taifa kama Tanzania ambayo walipa kodi ni milioni 3 na ndio maana ukiingalia Kenya ipo juu ya nchi zote za Afrika mashariki kwa bajeti yake hata kuwa tegemezi kwa wafadhili lakini ukienda kwa maisha ya mmoja mmoja unakuta hatutofautiani sanaaaaaaa hasa kwa wananchi wa kawaida.
 
Back
Top Bottom