Usain Bolt alibaguliwa na mtangazaji wa runinga ya Marekani

Usain Bolt alibaguliwa na mtangazaji wa runinga ya Marekani

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,276
1471538084280.jpg


Mtangazaji wa Marekani Ellen Degeneres 'alimbagua' bingwa wa olimpiki katika mbio za mita 100, Usain Bolt, kwa misingi ya rangi.

Hii ni baada ya mtangazaji huyo wa runinga ya marekani, kuweka picha akiwa amemdandia Usain Bolt na kuandika kwenye Twitter kwamba ameshapata mbinu mpya ya kuwashinda wapinzani wake.

Mashabiki wa Bolt wamelaani picha hiyo wakisema ni kumnyanyasa Bolt na kumfananisha na farasi ama punda.

Ellen Degeneres, amejibu shutma za mashabiki wa bingwa wa mbio za mita 100 Olimpiki Usain Bolt kuwa yeye si mbaguzi wa rangi.

Ellen anayetambuliwa kwa machachari yake, amesema mashabiki wa Bolt wameielewa vibaya picha hiyo na kujitetea yeye si mbaguzi wa rangi na anapinga kitendo hicho.
 
Ni kweli sio mbaguzi charity yako inasaidia sana watu weusi.....sio mbaguzi kama wengine yaani sio mbaguzi wa wazi!!
 
bolt hawamuwezi wamarekani wanalijua hili
moja ya vitu vinavyowaumiza
 
Kama kuna ujinga... basi ni kudai hii picha ina chembe yoyote ya ubaguzi

Huyo dada na bolt ni washikaji, jamaa mwenyewe kazungusha around the world baada ya kuipata hiyo picha

Hakuna kitu kinakera kama inferiority complex na tabia ya baadhi ya sisi weusi kutafuta kiki na kuplay a victim... probably we are more racists than hao wazungu
 
Umeielewa story iliyoko behind the picture? “Nimepata mbinu mpya ya kupambana na maadui zangu” got that?
Mimi nimeelewa tofauti na wewe mkuu,siku zote naamini uelewa wa mtu katika mambo flani unategemeana na vile akili yake inavyowaza,ukiwa na hisia za kubaguliwa tambua kabisa kuna sehemu unaweza kujibagua mwenyewe hata kama hujafanyiwa hicho kitu.

"We are what we think"
 
1471550966730.jpg
acheni kutetea nyinyi hawa jamaa wameanza enzi hizo mpaka leo wanaendeleza..!

Na wana style nyingi yakubagua
 
Watu weusi wana inferiority complex inawasumbua,sijaona ubaguzi wowote hapo zaidi ya kutokujiamini tu......!

Nakuunga mkono 100% Yaani mara nyingine tunakuwa over sensitive!

Huyu mama was just joking, kwamba angependwa abebwe na mtu mwenye kasi ili ashinde. Kwanza kitendo cha kubebwa ina maana wana urafiki wa namna fulani tayari. Lakini watu wako tayari yo make mountains out of mole hills!
 
ngozi nyeusi tunapenda sana kuwa victims. ubaguzi ni kitu ambacho sisi tunatamani kiwepo ili tupate sababu ya kuendelea kuwalaumu wazungu kwa matatizo yetu. kwa fikra hizi bara la Africa litaendelea kuwa maskini kila siku.
 
ngozi nyeusi tunapenda sana kuwa victims. ubaguzi ni kitu ambacho sisi tunatamani kiwepo ili tupate sababu ya kuendelea kuwalaumu wazungu kwa matatizo yetu. kwa fikra hizi bara la Africa litaendelea kuwa maskini kila siku.
Rudi tena... hujaeleweka
 
Back
Top Bottom