USAHIHI: Kuhusu uvumi wa John Mnyika

USAHIHI: Kuhusu uvumi wa John Mnyika

Raia Tanzania wameweka front page, hivi haya magazeti mbona hayakamatwi
 
1467607345589.jpg
 
Sawa sawa mnaweza kuandika lolote mnalotaka ila hakuna Mnyika mpuuzi kiasi hicho. Maccm mmekaa mda mrefu bila kutibua amani UKAWA hivyo mnadhani propaganda zenu zitasaidia.
Kaushauri tu;
Laiti ccm mngejikita zaidi kwenye maongozi yawezayo kuleta maendeleo kwa taifa mkaonesha uwezo wa kuliongoza taifa kuelekea kwenye mafanikio wala si kulitikisa taifa kwa kuminya demokrasia.
Hakuna na nasema hakuna Mtanzania asiyeona mambo mema mnayofanya, hakuna mtu anayetaka kuambiwa kuwa hili ni zuri au hili ni baya. CCM mkitenda mema mtatawala milele, ila mkiendelea kuminya demokrasia, mtaendelea kutawala bila ridhaa ya watawaliwa.
Tendeni mema, acheni kutumia watu kudidimizza upinzani. Tutawaangalia hao wapinzani, tutawapima na mwishoni tutawapa haki yao wanayo stahili. 2020 is not far, tumuunge mkono rais akiinue chama kilipotumbukia si kwa migongo ya watu.

slaa yuko wapi? rais wa mioyo ya watu?
 
Kama katibu mwenezi bavicha anaandika vitu shallow namna hii bila substance, inasikitisha sana.
Comment yako inasikitisha zaidi na kudhihirisha ulivyo shallow zaidi kwenye ubongo wako...
 
Pamoja ya kwamba siamini juu ya taarifa kuwa Mnyika ametamka kuwa Lowasa ndiye awe wa kawanza kuhukumiwa kwenye mahakama Division ya mafisadi, ila ukimya wa Mnyika una leta mashaka. Mnyika wa 2010-2015 alikuwa ni machachari sana. Na nilishangaa kuona katika wabunge wasiopungua kumi waliofukuzwa kwa ubabe wa Spika ati Mnyika hayupo. Ingekuwa ni Mnyika wa 2010-2015 nadhani habari ingekuwa nyingine.
 
Hivi mnawashwa na ninI? Si tumewaachia nchi mtawale mnavyopenda. Dola mnayo, hazina mnayo, matrillion mliyoyaficha uswis na kwingineko bado yapo salama na matrillion ya maden mliyosababisha kwa kuiba tunawalipa na hata tukifa watoto na vizazi vijavyo watawalipia. Licha ya yote hayo badoo tuu. MNABOA
Yaani, hawajiamini..
 
slaa yuko wapi? rais wa mioyo ya watu?

Mkuu tukuulize wewe ambaye ulikuwepo akiingia Chadema, ukauona mkataba wake na hicho chama. Nalijua moja tu; Chadema si mamake Slaa wala babake Mnyika. Wala, sio chama cha kufa na kuzikana. Kama kikimuudhi atakihama na kuhamia kingine mchana kama alivyojiunga mchana.
Acheni propaganda, Njooni tuunde upinzani wa kuling'oa hili jini kizee miaka zaidi ya 50 bado linaogopa upinzani. We are done with yuuuuuu. Mtabanaaa lakini ipo siku mtabanua
 
Juzi zimevuma hapa za kile kilichosemwa ni waraka aliotoa John Mnyika akitaka lowassa akamatwe kwa ufisadi.
Mimi sio mwandishi mzuri sana au sio mwanasiasa mzuri ila nna maswali mengi kichwani. Natilia shaka juu ya huu waraka unaweza kuwa ni wa kutengenezwa, kwanini?
1. Kwanini ccm wasitafute ukumbi wakalipia na kumweka mnyika ili atoe ya moyoni kama ilivofanyika kipindi cha uchaguzi pake dr. Alivyojitokeza kwenye vyombo vya habar na kutoa tamko kuhusiana na lowassa kipindi hicho huku mpango huo ukifadhiliwa na ccm? Ingekua ni kweli ccm wangekwisha lipia ukumbi ili mnyika aongee na waandishi wa habari kuhusiana na tamko hilo.
2. Kwann mnyika asiongee kipindi chote hicho iweje aje atoe tamko hilo leo na sio siku nyingine?
3. Myika anapenda kuandika habari zake kwenye page yake ya twitter na Facebook lakini kwa warraka huu imekua tofauti, waraka uliandikwa kwenye page za vijana wa lumumba.
 
Mnyika mwenyewe ameishaukanusha waraka huo achana na hayo.
 
Mkuu tukuulize wewe ambaye ulikuwepo akiingia Chadema, ukauona mkataba wake na hicho chama. Nalijua moja tu; Chadema si mamake Slaa wala babake Mnyika. Wala, sio chama cha kufa na kuzikana. Kama kikimuudhi atakihama na kuhamia kingine mchana kama alivyojiunga mchana.
Acheni propaganda, Njooni tuunde upinzani wa kuling'oa hili jini kizee miaka zaidi ya 50 bado linaogopa upinzani. We are done with yuuuuuu. Mtabanaaa lakini ipo siku mtabanua

mwaka wa 23 huu, kila uchaguzi tunasema hivyo....una hamu iwe hivyo, bahati mbaya hao unaowaamini hawana mawazo kama wewe

komaa, andamana, ongea fanya ufanyavyo kama mpinzani...TUME IBADILIKE, ukimaliza vita ya tume ndio tungee mengine haya...grow up kid
 
Sijamuona Mh. John Mnyika kwenye media kwa muda mrefu sasa tangu uchaguzi mkuu 2015 uishe. Mh. Tunamiss sana mpambanaji nguli katika siasi. Je, yupo masomoni au wapi?
 
Wapi? Mbona wapambanaji wengine kama akina Kabwe Zuberi, Lissu Tundu nawaona mara leo kaswekwa rumande mara yupo mahakamani mara yupo na media kila kukicha
 
Yupo mpaka leo hii bado haamini kama aliemdhihaki wanaishi nyumba moja!
 
Kivipi yaani? You mean under the same roof...? Ina utata kisiasa...
 
Back
Top Bottom