Iliwahi nikuta hii, nilinunua Tv, Hisense nch 40.
Mie nilijua wananileleta kwa Uber au tax, nyie naletewa iko kwa boda afu kishandu.
Dadekiii nilimuambia rudisha uliko itoa, na ikabadilishwe, sina hakika km iko salama hii,
Tukaanza kuzozana na boda yule, mara nikawarukia dukani, wanajibu vipi mbna mwenzio aliyekuja dukani kakubali ipakiwe kwa boda, (nilimuagiza mtu akanichukulie pale).
Nikawaambia free delivery ndo huyu kishandu? Msinitanie nakuja huko huko dukani, na niliwaendea tulisanukiana hapo, nikabadilisha na nikakodi tax kurudi nayo home.
Sina utani na pesa zangu, bora unichezee mie, ila sio vitu vyangu. Lol