Usafirishaji hatari wa Tv kuanzia Inch 60

Usafirishaji hatari wa Tv kuanzia Inch 60

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,197
Reaction score
10,710
Ebu leo wanandugu njooni tuzungumze kidogo. Mara nyingi sana huwa napishana mitazamo na watu juu ya namna ya usafirishaji wa tv kubwa kuanzia inch 60 na kuendelea. Huwa nawaambia kama umeweza kupata milion 1+ kwaajili yakununua tv ya ndoto yako kwanini ushindwe kutoa elfu 50 ya usafiri tv yako ifike salama bila wasiwasi??
1758908383212.jpg

Hivi kweli tv ya milioni 1+ kama hii ubebe kwenye bodaboda Kariakooo hadi Tabata?? Ebu njooni tuzungumze tuweke wazi tatzo huwa lipo wapi? Yaani mnapata ugumu gani kutoa pesa ya usafiri kwa tv kubwa kama hizi?
 
Aisee, kuna mtu leo anapelekewa TV mbovu, nimeona kabisa imeangushwa hapo Kimara na bodaboda. TV ya Kichina something Star nn sijui. Sema ndogo 32”

Mimi nikitoa Mil 1 ninunue TV haunishawishi kwa free delivery. Naifuata na request bolt ya gari narudi home.
 
Mtu ana nunua TV ya milioni ila anashindwa kutafuta usafiri mzuri kwa elfu 50 Tu. Hivyo hivyo hata Friji mtu ana nunua la milioni ila anapakia kwenye boda boda...wanalidondosha chini wanafuta futa vumbi wanakufikishia wanakwambia litulize washa baadae...ndio imeisha hivyoo..

Kuna shida sana kwenye uelewa wa watu. Au sijui ni mazoea au ndio kubana matumizi
 
Wapuuzi tu hawa. Neno free delivery linawadanganya
 
Hapo mteja anafanyiwa delivery,ni wauzaji ndio wanarisk hivyo sio mteja.
Mzigo ukishakua kwenye boda hivyo huo bado ni mali ya sisi wauzaji, chochote kitakachotokea kinamhusu muuzaji sio mteja
Yani mteja amenunua bidhaa kwako yenye thamani zaidi ya 1M+ unashidnwa kumsafirishia kwenye usafiri salama na wenye hadhi sawa na mali alionunua? Hivi customer care Tz bado tatizo sana!
Wew mwambie bei ya Tv mfano ni Tsh 1,560,000 ukijua hiyo elfu 60 ni for delivery pakia kwenye IST mfikishie kwake.
 
Back
Top Bottom