usafiri wa Precion air ni aibu tupu

Wana jf,
Katika siku.za hivi karibuni usafiri wa anga kwa kutumia kampuni ya precion air umekuwa kama kituko kutokana na kubadilisha ratiba za usafiri mara kwa mara .Sio siri ni afadhali kusafiri kwa basi kwenda mikoa ya kaskazini kuliko kutumia precion air

Mkuu ulikuwa unaenda kwenye operation sangara au vua gamba?
 
kubadili ratiba sidhan kama ni ishu sana, nishawai subirishwa masaa kadhaa Schiphols aepot na KLM, Pia Luftansa pale Berlin alkadharika KQ Lagos, kwa sabubu hii au ile.
Ila customer care nadhani ndo ya kuangalia isije kuwa CUSTOMER SCARE, hilo bila shaka CEO Kioko anauwezo wa kudili nalo.
 
Pole Nyati....................we have to live with it i think hadi Serikali hii itakapotoka madarakani................au sio?
 
Last edited by a moderator:
Pole Nyati....................we have to live with it i think hadi Serikali hii itakapotoka madarakani................au sio?

Nafikiri hapa Serikali haihusiki kwani hii ni kampuni binafsi. Pia nikifanya tathmini kwa wenzetu Kenya, mambo ni yale yale, tena wakati mwingine waweza sema afadhali ya jana.
 
Mi ambako 540 inaenda it is my flight of choice na wenyewe wakileta za kuleta napiga chini![/QUOTE Tatizo huwa wanaanza vizuri wakishaona wamekamata soko wanajisahau, hata hao 540 utaona huduma zao baada ya kipindi kifupi kijacho kama zitakuwa hivyohivyo.
 
Zile flights za connection ziko vizuri sijaona ubaya wa customer care lakini uzuri nilikutana na wanaume wako counter, hata wale wa JNB wako vizuri wale mabinti wahudumu kidogo walijtahidi kwa kweli.
 
labda kama wamebadilika ila ukweli nimepanda sana precision mwanza dar and kia to dar kipindi nipo nyumbani ukweli sijawahi kuona ndege mbaya namaanisha kimazingira kuwa kuna mende viti vimechoka ila wanatatizo la muda tu hapo ukweli ndio ubovu wao. kama wamefikia huko sijui mamlaka ya ndege huko nyumbani wanafanya nini nahisi hili wanahusika nalo abiria hawezi kupanda ndege kama viti vinaweza kung'oka kirahisi ni hatari kwake hasa kwenye kuondoka na inapoland. na vile vile watu wawe wakweli ili wahusikia wajue wapi pa kurekebisha na vile vile nahisi kuna suggestion box pale tupia kitu chako pale.
 
Ndugu yangu alikaa kwenye kiti ambacho mkanda haufungi...kawaita wahudumu wakajidai kama nao wanashangaa...you can imagine unapanda ndege yenye mkanda mbovu.

Ila sishangai sana ndege nyingi za Africa zisizoenda nchi za ulimwengu wa kwanza ni bora ipae tu. Maana ulimwengu wa kwanza wanakagua safety na hawatakuruhusu uingize ndege kwao ikiwa haijakidhi viwango.

Kuna rafiki yangu wa Ghana ananambia ndege zao wanaita majeneza maana AC hazifanyi kazi basi mkishuka wote mmelowa jasho na mnakaribia kuzimia..Eti AC mbovu ndege inatumia feni...nilicheka nikaona wahongo walikuwa kama watatu wote wakasema habari ndo hiyo.
 
Wana jf,
Katika siku.za hivi karibuni usafiri wa anga kwa kutumia kampuni ya precion air umekuwa kama kituko kutokana na kubadilisha ratiba za usafiri mara kwa mara .Sio siri ni afadhali kusafiri kwa basi kwenda mikoa ya kaskazini kuliko kutumia precion air

halafu serikali imeuchubua tu, vikija kuua watu, ndo tutaona sarakasi za kujitetea, hivi hii haifanani na ile ya MV SKIGIT kweli? au kwa sababu hivi vindege vinabeba abiria kiduchu???? lakini si roho za binadamu hizo???? halafu inatuchafulia image ya secta yetu ya usafiri wa anga.
 
Nadhani PW wana matatizo waliyokuwa nayo ATC. Miaka ya nyuma nilisafiri kutokea Kinshasha na Ethiopean Airlines kwenda Addis ili kuunganisha kwenda Dar. Kwa vile Ethiopean Airlines ilichelewa waliwapigia simu ATCL watuunganishe kutokea NRB badala ya Addis. ATC Wakakubali. Tulipotua NRB ATC walikuwa hawana ndege. Ilibidi tula pale Hotel 680. Siku ya pili yake ilikuwa ni Jumamosi tulipanda ATC asubuhi na kufika DSM. Siku iliyofuatia (Jumapili) ilikuwa nisafiri na ATC kwenda Gaborone Botswana. Baada ya kupumzika kidogo nikaamua kujaribu ku-confirm safari yangu ya Jumapili. Nikaambiwa wamebadilisha na kuwa ndege ilikuwa inaondoka siku hiyo (Jumamosi) saa nane. Sikuweza kuamini nikaweka simu chini, nikaanza kutafuta usafiri wa kwenda airport. Nilipofika Botswana nikawa sina mwenyeji wa kunipokea kwani sikuwaarifu na enzi zile Botswana kulikuwa hakuna taxis. Nilipata shida kidogo.
 
Back
Top Bottom