linguistics
JF-Expert Member
- Jun 22, 2014
- 4,701
- 4,325
Kwa hiyo agizo limeshaanza kutekelezwa?? Huu unapaswa kuwa mpango wa muda. Wataalamu waje na mpango wa kudumu ambao utaendana na hali ya maendelea ya kiteknolojia na kiuchumi duniani.tuko hapa Nzega askari wametuzuia sababu eti gari inakimbia sana, so tunasubiri kesho tuendelee na safari kuelekea Bukoba. kwa sasa ni kujiachia tu, hakuna namna
Ni kweli maana Igawa pale saa 3 mara nyingi jamaa wanakuwa washaondokaUnajua ni kwanini wanakulaza hapo mida ya saa 4? Ni kuwa wanajua kwa saa 2 tu huwezi kufika Mbeya na wakikuruhusu ni kwamba utaendesha hadi unafika maana baada ya Makambako hakuna checkpoint inayofanya kazi usiku iwapo ya mpakani na Mbeya hawapo.
Barabara ya singida dodoma nyeupeee,mabasi mawili peke yao,wamegongana uso kwa wamelengana kwanza,halafu wakaweka gea wakaanza kutimua vumbi,watu 30 wamekufa papo hapoHayo ni mawazo yako. Ilitakiwa waangalie uwezekano wa kuboresha barabara ili watu watumie masaa sita kwenda mbeya kwa usafiri wa gari. Hii dunia inasonga mbele wala hairudi nyuma. Mtaishia kuwa watumwa milele kwa kukosa maarifa na fikra
Madhara ya kupost ukiwa umebetua makalioAjali haizuiliki. Wenzetu wanatumia kila mbinu kuokoa muda sisi tunafanya kila njia kupoteza muda
Ajali nyingi zinazotokea ni kutokana na ubovu wa barabara. Nina hakika kama ingekua ni mwendo, basi watengenezaji wa magari wangeweka speed ndogo. Jiongeze kijana. Barabara zikiwa pana itasaidia kupunguza hizo ajali. Na isitoshe hiyo ajali unayoisemea wewe ni makosa ya madereva wenyewe na sio speed ya gari. Hata wangeenda na speed ndogo kwa mchezo huo lazima ajali itokee. Hivyo hiyo haiwezi kuwa hoja. Labda ingeniambia waboreshe usalama ili michezo hiyo ifeBarabara ya singida dodoma nyeupeee,mabasi mawili peke yao,wamegongana uso kwa wamelengana kwanza,halafu wakaweka gea wakaanza kutimua vumbi,watu 30 wamekufa papo hapo
Sasa wewe unakuja tna ushauri wa kutanua barabara wafike ndani ya masaa6? Itabidi kuwe na makaburi pembezoni mwa barabara zote
Kuna hatari hata maendeleo yatazidi kuchelewaWaliozoea kusafiri kwa mabasi kwa siku moja kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya na kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza na kwingineko kwenye umbali sawa na huo.
Sasa inabidi wajipange kisaikolojia kutumia siku mbili kukamilisha safari hizo.
Hayo yamebainishwa na Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geofrey Silanda.
Uamuzi huo umetokana na utafiti uliofanywa na mamlaka hiyo na kubaini kwamba mabasi yanayofanya safari kwenye mikoa hiyo hayapaswi kusafiri kwa siku moja
View attachment 376295
Chanzo: EATV
Toa maoni yako