Usafiri wa mabasi kwa baadhi ya mikoa sasa kuchukua mpaka siku mbili kufika

safi sana .....naunga mwili hoja tutanyookaje sasa...ila watu watagegedana jamani!!!maana sipati picha ndio bus linalala singida af mnaruhusiwa kwenda kulala loji mpaka saa kumi alfajiri........asanteeeeeeeeeeee
we kwel mchepuko
 
Sikubaliani na Mbeya-Dar Mbeya ni KM 840..hata dereva akitembea kwa 80km/h itakuwa masaa 12 kufika, kusafiri siku mbili kwa umbali huo ni kupoteza Muda ..ila kwa Mwanza, Sumbawanga na Kigoma ni sahihi wawawekee iwe siku mbili..Majinja inafika Sumbawanga siku moja km 1150 si hatari hii, Mwanza Km 1152 kutoka DAR
 
Sidhani kuwa huo utafiti umezingatia vigezo gani..Hapa majibu hatuwezi kuwa nayo bila kusoma huo utafiti na vigezo vya kufikia hayo maamuzi.Ila Dar- Mbeya ni jirani sana,kutumia siku mbili ni upotevu wa muda tu.

Dar to Mbeya ni karibu km 900 tu ukiweka mda wa kupumzika kama saa 1 na gari itembee km80/saa basi gari hilo litatumia saa 12 au 13 kufika Mbeya au Dar.Sasa likiondoka saa 12 asbh ni kwamba saa 1 jioni hadi saa 2 usiku litakuwa Mbeya au Dar sasa kwanini zitumike siku mbili
Inawezekana hujawahi kupanda gari. Unasema gari itembee 80kph hadi mbeya kwa sababu ni 900km? Yaani wewe unachukua 900 unagawa kwa 80. Maajabu gari haiwezi kutoka stendi ubungo na 80kph hadi mbeya. Labda liwe peke yake barabarani na hakuna foleni, hakuna milima kama ndege vile.
 
Ndg zangu wote mie naungana nanyi juu ya udhibiti huu. Hapo tumeweza, na je kwenye pikipiki nini kifanyike?. Maana madhala ni mengi mno yatokanayo na hizi bodaboda, japo zinaturahishia usafiri na athali yake tunaiamuaje?
 
Sijui unaelewa nilichosema au ni kwamba una ulrmavu wa ubongo.Mwendokasi wa 80km/saa it means utatembea km 960 bila kupumzika kwa muda wa saa 12 means 12 asbh hadi 12 jioni. Hapo nimeweka saa mbili za delay time na hata hivyo umbali wa Dar - Mbeya haifiki hata km 860. So bado kuna km 100 ni extra ambayo ni kama mda wa saa 1 umezidi hapo.Haya njoo tena na ulemavu wako.
 
Hayo ni mawazo yako. Ilitakiwa waangalie uwezekano wa kuboresha barabara ili watu watumie masaa sita kwenda mbeya kwa usafiri wa gari. Hii dunia inasonga mbele wala hairudi nyuma. Mtaishia kuwa watumwa milele kwa kukosa maarifa na fikra
Dunia inaenda mbele wao wanabishana nayo.
Badala ya kusolve tatizo wao wanapunguza huduma.

Waweke na bumps kila baada ya 5m njia nzima
 
vyanzo vya ajali Tanzania ni kama ifuatavyo
1) mwendo kasi
2)ubovu wa barabara
nazungumzia mashimo alama za barabaran sehem nying kukosekana na sehemu nying kuwa na kona kali
3)ulevi wa madreva pamoja na uchovu kwani kuna mabasi ya Route ndefu ila yana dereva mmoja
4) rushwa kwa maaskari wa barabara hawa nao wanapenda Mno pesa ya kubrash viatu
5) ushabiki wa abiria wenyewe
6) uchakavu wa vyombo vyenyewe
7) ujazaji wa abiria kupita kiasi

ukiangalia hayo yooote hapo juu utaweza pata solutions ya tatizo la ajali hapa Tanzania. kwa solutions hii tumeamua _kutibu tatizo kwa kutengeneza tatizo_
ntarudi kushauri nin cha kufanya ngoja niendelee kufanya economic analysis impact kwa taifa
USAFIRI HUU UMEKUWA MAARUFU SANA KWA KUWA VITU HIVI VIMEKOSEKANA KATIKA SEKTA YA UCHUKUZI KWA HII NCHI YENYE KILA NEEMA KWA MAANA SIJUI NI KUTOJIELEWA ..TUNAKARIRISHWA UCHUKUZI NI MABASI TU WAKATI SI SAHIHI HATA KIDOGO,
1:USAFIRISHAJI KWA NJIA YA RELI,RELI YA KATI NA TANZANIA&ZAMBIA,TUWAZE HIZI RELI MBILI KAMA KWELI ZINGEFANYANYA KAZI KAMA WAJERUMANI NA WACHINA WALIVYOKUSUDIA JE TUNGEKUWA WAPI?
2.USAFIRISHAJI KWA NJIA YA MAJI:MFANO TOKA DAR MPAKA MTWARA,JE TUNGEKUWA NA MELI NA BOAT ZA KUELEWEKA TUNGEKUWA WAPI?
3.USAFIRISHAJI KWA NJIA YA ANGA:MFANO MIKOA YA MBALI KUTOKA DAR,TUNGEKUWA NA NDEGE AU SHIRIKA LINALOJIELEWA TUNGEKUWA WAPI?
HATA TUKIWEKA SPEED LIMIT 10KM/HR. TUTAENDELEA KUFA TU NA ZAIDI KUJIRUDISHSA NYUMA.WENZETU WASINGEWEZA KUWA NA TRENI ZA UMEME KWA KIGEZO CHA MWENDO...HAPANA.TUWAZE ZAIDI YA HAPA.HATUFIKI HAPO KOKOTE.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Ndg zangu wote mie naungana nanyi juu ya udhibiti huu. Hapo tumeweza, na je kwenye pikipiki nini kifanyike?. Maana madhala ni mengi mno yatokanayo na hizi bodaboda, japo zinaturahishia usafiri na athali yake tunaiamuaje?
Nikikuuliza nini hasa cha ajali nyingi siku hizi unaweza kubainisha vyanzo vyake?
 
The hammer.
Kwanza waendesha bodaboda wengi hawafuati sheria za barabarani. Pili wengi hawajazisomea kabisaaa. Leseni kutolewa bila mtu kupitia kwenye vyuo vifundishavyo udereva na vinatambulika na serikali. Na mwisho hawajali au hawathani uhai wao na abilia wanaotumia huo usafiri
 
Waangalie ajali hizo zinatokea wapi zaidi,unakwenda kubana speed kwenye gari zinazokwenda mbali wakati gari zinazofanya safari fupi mathalan Dar-Mor gari moja inapiga mpaka trip sita kwa siku kwa speed ile ile ya Dar-Mwanza.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
The hammer.
Kwanza waendesha bodaboda wengi hawafuati sheria za barabarani. Pili wengi hawajazisomea kabisaaa. Leseni kutolewa bila mtu kupitia kwenye vyuo vifundishavyo udereva na vinatambulika na serikali. Na mwisho hawajali au hawathani uhai wao na abilia wanaotumia huo usafiri
Ninachukulia kwa haya magari yanayoenda njia kuu.

Anyway,ulevi na kutopumzika,barabara pia na mwendokasi ndo vyanzo vya ajali katika barabara kuu.
 
Sidhani kuwa huo utafiti umezingatia vigezo gani..Hapa majibu hatuwezi kuwa nayo bila kusoma huo utafiti na vigezo vya kufikia hayo maamuzi.Ila Dar- Mbeya ni jirani sana,kutumia siku mbili ni upotevu wa muda tu.

Dar to Mbeya ni karibu km 900 tu ukiweka mda wa kupumzika kama saa 1 na gari itembee km80/saa basi gari hilo litatumia saa 12 au 13 kufika Mbeya au Dar.Sasa likiondoka saa 12 asbh ni kwamba saa 1 jioni hadi saa 2 usiku litakuwa Mbeya au Dar sasa kwanini zitumike siku mbili

Well said
 
Back
Top Bottom