Usafiri wa mabasi kwa baadhi ya mikoa sasa kuchukua mpaka siku mbili kufika

Ndio maana jana nimeshangaa nimemsafilisha wife toka dom kwenda dar yaani toka saa nne asubuhi wameingia dar saa moja na nusu usiku
 
vyanzo vya ajali Tanzania ni kama ifuatavyo
1) mwendo kasi
2)ubovu wa barabara
nazungumzia mashimo alama za barabaran sehem nying kukosekana na sehemu nying kuwa na kona kali
3)ulevi wa madreva pamoja na uchovu kwani kuna mabasi ya Route ndefu ila yana dereva mmoja
4) rushwa kwa maaskari wa barabara hawa nao wanapenda Mno pesa ya kubrash viatu
5) ushabiki wa abiria wenyewe
6) uchakavu wa vyombo vyenyewe
7) ujazaji wa abiria kupita kiasi

ukiangalia hayo yooote hapo juu utaweza pata solutions ya tatizo la ajali hapa Tanzania. kwa solutions hii tumeamua _kutibu tatizo kwa kutengeneza tatizo_
ntarudi kushauri nin cha kufanya ngoja niendelee kufanya economic analysis impact kwa taifa

Hii ni kweli na nahisi itasaidia sana, maana kuna baadhi ya Magari kiukweli yanakimbia sana hadi wasafiri wanalalamika ndani ya gari, lakini madereva wanakuwa hawajali, japo na abiria ni kweli wengine wamekuwa chanzo cha ajari hizi
 
Muda hauna thamani Afrika..... Kwanini wasiboreshe huduma za reli, kweli Mby kwa siku mbili ni Crime Against Humanity
 
Madereva wa Tanzania eti wanadhibitiwa na trafiki, je hao trafiki wanadhibitiwa na nani!?
Baadhi ya madereva wana reseni feki, je, huko trafiki nako uhakiki wa vyeti umeshafanyika!?
Basi tuweke wazi na TBS wahakikishe kila gari inayoingia Tanzania itengenezwe maalumu kutozidi spidi 60mph
 
Ahsante ni kulana mate puchi tu hamna namna
Una maanisha maambukizi ya ukimwi yataongezeka? na bajeti za kulala njiani? na-imagine wanafunzi wale wanaosoma shule moja afu ni me na ke, na wako bus moja au tofauti alafu sehem ya kulala ni the same area...watagegedana tu kwa wale wapenda dyudyu
 
Tulichorogwa na marehemu ni kutokutambua kua time is money, siku mbili umekaa tu kwenye basi hauzalishi, nchi inapataje kodi? sema hawa wenye mamlaka hawana mwalimu anayesahihisha matamko yao, laiti angekuwepo kwa haya majibu wanayotoa wangekua wanapata SIFURI.
 
SULUHISHO NI MABASI YAONDOKE STENDI SAA 10 ALFAJIRI NA MADEREVA WAWE 3 MATAJIRI WASIWE MABAILI KUWALIPA NA POLISI WAJIPANGE KUHAKIKISHA USALAMA WAO KUANZIA MUDA HUO WA SAA 10 BASI YATAFIKA SALAMA NA WATAPUNGUZA SPIDI MAANA MUDA WA SAFARI UMEONGEZWA.
abiria wafike sa8 usiku stand? hapo hapana nakataaaaaaaaaaa
 
acha iwe hvyo maana hakuna namna sasa..ajali zimezidi..jana maeneo ya Dumila- Kwamb nimeona basi imeanguka sijajua madhara gani imeleta.
 
Ili kupunguza ajali kabisa wangefanya mabasi yatumie siku tatu. Hapo uhitaji hata trafic barabarani.
 
Ndugu ukifika na basi lako Makambako saa 4:00 huvuki kwenda Mbeya unalazwa hapo, labda kama check points wana muda tofautitofauti
Unajua ni kwanini wanakulaza hapo mida ya saa 4? Ni kuwa wanajua kwa saa 2 tu huwezi kufika Mbeya na wakikuruhusu ni kwamba utaendesha hadi unafika maana baada ya Makambako hakuna checkpoint inayofanya kazi usiku iwapo ya mpakani na Mbeya hawapo.
 
Back
Top Bottom