Usafiri wa mabasi kwa baadhi ya mikoa sasa kuchukua mpaka siku mbili kufika

Inawezekana hujawahi kupanda gari. Unasema gari itembee 80kph hadi mbeya kwa sababu ni 900km? Yaani wewe unachukua 900 unagawa kwa 80. Maajabu gari haiwezi kutoka stendi ubungo na 80kph hadi mbeya. Labda liwe peke yake barabarani na hakuna foleni, hakuna milima kama ndege vile.
umenena kweki bro
 
Point yako naiunga mkono, ila kwenye spidi 100 hapo sikubalian nawe, 80 inatosha kabisa kwa safari ya siku moja, ila wasipitie mizani, sidhani kama kutapatikana ajali kwa hiyo spidi ya 80.

Nimeshauri 100 kuwa ni ya kiwango cha juu, ili kuwa na wastan wa walau spidi 60 au 70 kwa safari, sehemu za 50km/h tunazo nyingi sana kwenye barabara zetu. Lakini pia 100 ni spidi ya kawaida sana kwa magari yetu ya kisasa lakini pia sehemu kubwa ya barabara zetu zimeboreshwa.
 
mi naamini kwamba chanzo halisi cha ajali hapa tanzania bado hakijawekwa wazi, maana ukisema ni speed kubwa huwa haiko straight kwamba ni sahihi
 
Kuna jambo la msingi ambalo baadhi ya wananchi huwa mnalikosa linapokuja swala la mwendo kasi hasa wa magari ya abiria. Kwamba gari likiendeshwa 80km/hr basi baada ya saa moja, litamaliza km 80!

Dhana hii ni sahihi pale tu eneo husika litakua halina vizuizi kama alama za 30/50km/hr, milima, matuta, traffic jam na michoro mbali mbali iliyochorwa katikati ya barabara ambayo inakataza kulipita gari lililoko mbele yako hadi utakapokutana na mstari unaoruhusu, nk.

Ni kwamba kuna maeneo kama Mlima Kitonga, gari hupanda kwa takriban dakika 30, kona za zinazoanzia Mikumi unapoelekea Iringa (Iyofi?), sehemu zenye matuta barabarani, maeneo ambayo mwendo kasi hautakiwi kuzidi 50Km/Hr, michoro inayotoa maangalizo mbali mbali na maeneo mengine korofi.

Ni makosa kufikiri kuwa maeneo hayo gari litakuwa likienda 80Km/hr kuanzia Dar hadi Mbeya, ukiondoa maeneo ya kuchimba dawa na kula kwa dakika 10 kama kuku.

Lakini kuna wakati hata yale maeneo ambayo ni mazuri, unakutana na malori matatu au zaidi yanaongozana, lakini mbele yako sio salama, huwezi kwenda 80Km/hr kama vile umekaririshwa! (Angalia picha zilizowekwa hapo juu)

Wazo hili la kugawa safari limekuja limechelewa. Na kwa kweli kinachotakiwa, ni kuzifanyia barabara zetu kitu ambacho naweza kukiita 'Road calibration'.

Kwamba Summatra na vyombo vingine vya Usalama barabarani wa 'establish' muda sahihi wa kutoka eneo moja kwenda jingine eg Dar - Iringa.

Watoke na gari waendeshe kwa kufuata na kuzingatia sheria zote za Usalama barabarani (Maeneo ya 50km/hr yazingatiwe, sehemu za kuchimba dawa - kujisaidia, kwenye kona za Iyomvi na Mlima kitonga wazingatie michoro barabarani) na sehemu za kujiachia watembee 80km/hr.

Kisha kwa kutumia wataalamu wa IT, itengenezwe programme maalumu, ambapo gari likitoka tu Ubungo, taarifa ya gari, dereva, muda aliotoka muda wa kufika Kibaha, Chalinze, Morogoro, Mikumi, Ruaha Mbuyuni na hatimae Iringa itakuwa inatolewa toka kwenye system.

Kitakachofuatia, kwenye kila eneo, watakuwepo Matraffic kwa ajili ya kuhakiki muda gari lilipofika against ratiba ambayo dreva atakuwa nayo. Kama atakuwa ndani ya muda, fomu isainiwe na aruhusiwe kuendelea, kama atakuwa amewahi, alimwe faini na gari izuiliwe hapo hadi muda wa kuondoka ufike.

Ni vizuri adhabu zikapitiwa upya ziwe kali kwa madeva na ziende mbali zaidi ziwahusu wamiliki wa magari. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kupunguza utitiri wa askari wa Usalama barabarani ambao kwangu mimi nachelea kusema hauna tija kwa sababu tunazidi kushuhudia ajali kila uchao.

Naomba dhana kuwa ajali hazizuiliki tuiondoe kwenye vichwa vyetu kwani haina ukweli isipokuwa kwa baadhi ya matukio, kama mwamba au jiwe kuporomoka ghafla, au mti kuanguka ghafla na kuziba barabara, lakini kugogangana uso kwa uso, kwangu ni uzembe uliokithiri!

Wasalaam!
 
39533a57969d7fad358debe98d06aca8.jpg
 
safari ndefu lazima tulale njiani sasa hapo ndio ninapokumbuka zamani aza ya super najmunisa na zeber
 
Hayo ni mawazo yako. Ilitakiwa waangalie uwezekano wa kuboresha barabara ili watu watumie masaa sita kwenda mbeya kwa usafiri wa gari. Hii dunia inasonga mbele wala hairudi nyuma. Mtaishia kuwa watumwa milele kwa kukosa maarifa na fikra
Kusema ukweli Tanzania inahitaji utafiti wa hali ya juu. Kwani kwa sasa hata kwenda hapo Mororgoro tu muda unaotumika ni mrefu. Na naungana nawe kuwa ni vema kuangalia jisni ya kupunguza muda. Sina hakaika kama analysis imefanyika hiyo ya kulala njianai na social implication yake. Naunga mkono juhudi zote za serekali za kuzuia ajali lakini ni vema kuangalia changamoto kuu moja kwani kuna changamoto ambayo imewahi kusemwa nami nimei- experience recently. Ni hili la watu kujenga kando ya bararabara na hata bila ya vibao vya kupunguza mwendo bado tu busara sehemu yenye mji/ kaya za watu utapunguza mwendo tu katika kuendesha. Sasa njia nzima inaanza vamiwa na makazi ya watu ina maana speeed itabidi ipungue hivyo mpaka kufikia 2025, kwenda Mororgoro itachukua masaa sita badala ya matatu. Sijui watalaamu hili wanasemaje?
 
Wakati wenzetu wanakimbia sisi bado tumelala na siku tukiamka tuanze kunyata,kutembea na hatimae kukimbia wenzetu watakua wameshapaa miaka mingi.Na siku Africa tutajua kutumia muda ndo siku tutakayoamka.Tafakari.
 
Back
Top Bottom