Usafiri wa mabasi kwa baadhi ya mikoa sasa kuchukua mpaka siku mbili kufika

Ajali nyingi zinazotokea ni kutokana na ubovu wa barabara. Nina hakika kama ingekua ni mwendo, basi watengenezaji wa magari wangeweka speed ndogo. Jiongeze kijana. Barabara zikiwa pana itasaidia kupunguza hizo ajali. Na isitoshe hiyo ajali unayoisemea wewe ni makosa ya madereva wenyewe na sio speed ya gari. Hata wangeenda na speed ndogo kwa mchezo huo lazima ajali itokee. Hivyo hiyo haiwezi kuwa hoja. Labda ingeniambia waboreshe usalama ili michezo hiyo ife
Eheee! Ndio ninachotaka kusema,kwamba akili za madereva wetu zinatakiwa kufanyiwa kazi,hata upanue barabara vipi bila kushughulika na akkli za madereva ni kazi bure
 
Kwakua madereva na wenye mabasi wameshindwa kupunguza kabisa ajali.hatuna la kubisha acha iwe hivo 40k/h kama Rwanda!
Mtu anayetoka rwanda akifika huku apande ndege zetu za aridhini nadhani anaweza akashukia njiani, maana 40kph ni kama bajaji.
 
Upuuzi, barabara ziwe njia Tatu au nne waone kama ajali zitakuepo
 
Hata kama mtanipinga lakini nasema;
Mchawi wetu sio huo mwendo kasi kwani hakuna bus linalokwenda hiyo safari kwa siku mbili. Ingelikuwa hivyo, basi kila siku tungesikia ajali.
Naomba badala ya SUMATRA kuwasumbua wasafiri, hebu waambieni wahusika na utengenezaji barabara wajirekebishe. Kila siku huwa miye nasema Tz hatuna wasomi wa Mipango. Tunafanya, tunapambana na lile lililo mbele yetu tu. Fore Planning hatuna kabisaaaa.
Barabara inajengwa kutokana na magari yaliyokuwepo miaka 20 ilopita. Unategemea nini hapo ka si msonamano usio kwisha. Mradi unabuniwa, unachukua miaka 10 kabla haujatekelezwa. Ukijaanza, tiyari watu wesha jenga majumba ya kudumu kule pembezoni. Mitaro ya maji inaleta maafa kwa watu.
Ushauri;
Msiwaletee watu matatizo mengine. Rekebisheni barabara wala hakuna mwendo kasi. Bus likilala njia, mabaya yatokanayo na vituo hivyo mtakavyo weka, ni makubwa kuliko hiyo ajali mnayoidhania. Ukimwi, mimba zisizotarajiwa na hata wasafiri kupoteza mali zao kwa kuibiwa na mambo kama hayo.
Hamjifunzi kitu kutokana na miji ambayo madreva wa malori hufanya vituo?? Ukimwi unaenea ka upepo. Watoto wengi wameacha shule na kulowea guest. Sasa ongezeni na mabasi nadhani mtaongeza na ruzuku ya madawa ya kujikinga.
 
Sidhani kuwa huo utafiti umezingatia vigezo gani..Hapa majibu hatuwezi kuwa nayo bila kusoma huo utafiti na vigezo vya kufikia hayo maamuzi.Ila Dar- Mbeya ni jirani sana,kutumia siku mbili ni upotevu wa muda tu.

Dar to Mbeya ni karibu km 900 tu ukiweka mda wa kupumzika kama saa 1 na gari itembee km80/saa basi gari hilo litatumia saa 12 au 13 kufika Mbeya au Dar.Sasa likiondoka saa 12 asbh ni kwamba saa 1 jioni hadi saa 2 usiku litakuwa Mbeya au Dar sasa kwanini zitumike siku mbili wakati muda wa mwisho basi kutembea barabarani ni saa sita usiku.
Umesahau fileni ya kutoka Ubungo,hrf km 00000 dar mpk chalinze sehem KUBWA ni 50 speed kwa saa,hrf ukifuatana Na roli linaloenda speed 30 Na hapo huruhusiwi kuovateki sijui kama utaenda mbeya kwa Massa 12.hrf wanaosafiri kila siku wataoumizwa Na hili ni wafanyabiashara.lkn wale wanaosafili Mara Moja kwa mwaka wao sawa,serikari iangalie pia miundombinu,barabara hizihizi guta,baiskeli watembea kwa miguu mikokoteni punda,matrekta.nk.hata hivyo tz Luna Madereva bwana
 
Hii ni sawa kwa mtazamo, ila watu wanaopata dharula wapite wapi kuwahi ratiba zao muhimu?
 
Mpango wa kuhakikisha Ndege mbili Bombadier za kutoka Canada zinapata wateja lukuki umewiva,jamaa wana akili sana hawa, hujawaelewa tu:)
 
Kuna bahari nimekutana nayo kwenye mitandao kidogo imenisikitisha, najua wanayafanya haya kwa nia njema tu hasa usalama wa watanzania, ila kwa kweli kutoka Dar mpaka Mbeya au Mwanza kwa siku mbili siungi mkono hata kidogo.

Wakati wenzetu wanarahisisha mambo, wanajitahidi kuweka miundo mbinu ambayo itawawezesha kuyafikia maeneo ya mbali yanayo fanana na haya ya kwetu kwa muda mfupi zaidi mwaka hadi mwaka, nyie mnajitahidi kweli kweli kuturudisha enzi za mwalimu.

Tulisha toka kwenye siku mbili tukaja siku moja tena masaa tu, mnarudi tena kwenye siku mbili, wanaosemaga mtu akizeeka huwa akili inarudi anakuwa kama ya mtoto kuna ka ukweli, yaani tushazeeka sasa tuko kwenye harakati za kurudi utotoni, nategemea watu wa Kigoma na Bukoba kutumia siku tatu sasa, yaan speed ya 50km/HR si bora utembee na baiskel tu.

Atleast mngeweka hata aina mbili za magari/mabasi, let's say ya 50, 80, mengine 100, abiria achague mwenyewe anasafiri na basi la aina gani, Mnawaumiza wamilik wa mabasi, kama alikua aingize bil 1 kwa mwaka means nusu ya pesa ndio imepotea hvyo.

Wafanyabiashara ambao wanafanya mizinguko ya biashara labda mara mbili kwa wiki mmewaharibia tayari mzunguko wao, mnaongezea watu gharama za njiani ambazo hazikuwepo, mnapoteza muda wa watu bila sababu yeyote. Tukutane kwenye gari za magazeti mpaka tutakapo kuwa na uwezo wa kusafiri kwa ndege.
 
Waliozoea kusafiri kwa mabasi kwa siku moja kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya na kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza na kwingineko kwenye umbali sawa na huo.

Sasa inabidi wajipange kisaikolojia kutumia siku mbili kukamilisha safari hizo.
Hayo yamebainishwa na Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geofrey Silanda.

Uamuzi huo umetokana na utafiti uliofanywa na mamlaka hiyo na kubaini kwamba mabasi yanayofanya safari kwenye mikoa hiyo hayapaswi kusafiri kwa siku moja


View attachment 376295

Chanzo: EATV

Toa maoni yako
Naona wanataka watu warudi kwenye train kilazima sasa ...
 
Barabara zipanuliwe.barabara tulizonazo ni nyembamba kiasi kwamba magari yanapishana kwa shida.
Usafiri wa usiku urudishwe,na mwendo udhibitiwe.kusafiri usiku itakuwa inamshawishi dereva kuendesha kwa mwendo wa kawaida,matairi hayatapasuka hovyo,na uchumi utakuwa mara mbili(wenye magari watakuwa na gari mbili zinazoenda mchana na usiku,hoteli na vituo vya mafuta vitakuwa na uhakika wa kuuza mafuta mchana na usiku na askari watakuwa na malipo zaidi)!!
 
Na Hawa wa jirani wanaojiingiza wenyewe kwenye maroli nyuma tunawasaidiaje?
 

Attachments

  • IMG-20160731-WA0005.jpg
    IMG-20160731-WA0005.jpg
    66.6 KB · Views: 36
Back
Top Bottom