Usafiri Dar - Mtwara, King Yassin Tours hongera

Mimi nikajua wanagawa k wiii watu tunatoa lock

Umekaa serious baba wa familia unakuja kulia lia humu ndani kisa maji ya moto yaliowekwa majani yabadilike rangi
Yani na kusifu unasifu eti kila sehemu wanatangaza upo wapi
Wewe ni mwanaume braza kituo sio muhimu utangaziwe we jua tu unaenda wapi.
Hata kama mfano unaenda moro wakikushusha chalinze unamalizia tu kwa mguu

Au nakosea ndugu zangu?😂😂
Mitano tena😂
 
Hao jamaa wanajitahidi kwa huduma , kusini mikoa ya mtwara na Lindi bado kunahitaji ukombozi mkubwa sana kwa biashara ya abiria maana ni kama ndo wanaaanza.

Abiria kule hana haki zake za msingi , kumbuka hawana hata Miaka 10 ya mabasi mazuri ,kwa sababu njia ilisumbua sana kule,
Usishangae unapanda Basi halafu konda anakuomba pesa ya begi ulilobeba Kama mzigo mbali na nauli .

Mabasi mazuri kusini yapo muda tu sema labda huduma mbovu maana nakumbuka miaka ya 2000 kulkuwa na basi kampuni ya NAJMA mbona lilikuwa bomba tu kwawaki ule??
 
Wewe utakuwa unaongelea vitu pasipo na latest information, kifupi una kariri maisha. Maning Nice ameingiza Gari sita njia ya kusini mwezi novemba 2020 mpaka rangi amebadilisha, Braza hata picha niliyoiipost hapo juu huiyoni hizo namba za Gari au aina ya Gari?!! Acha kukurupuka au unajifunza kureply message!??
hamjui maning nice huyo na iyo ndio idadi ya basi anazoagizaga hajawahi agiza basi moja
 
Upo. Sawaa kabsa binafsi ntakuwa mteja wao wa kudumu ,safar ya mtwara na king yassin tour ni nzuri sanaaaa .hawana makuu hawa watu ,ila wasilewe sifa wakizingua tutawachana vile vile
 
King yassin yupo poa sana, Kusini nimetumia Buti la zungu la hio king yassin nikweli wanagawa chai ila mimi sio mpenzi wa kula njiani
 
Unanikumbusha mabasi ya Arusha to Dodoma, hotel wanayosimama pale babati nje ya mji hakuna escape route aseee, hata muuza karanga akisogea nje ya hotel wanamkamatisha kwa mgambo, alafu uliza bei yao ya chapati kwa chai mh!, utarudi kimya kimya kwenye basi na kutafuta usingizi !.
Pale Babat wanapokula mabasi i pana balaa , nimewahi kusafiri na njaa Siku moja nikitokea dodoma ,
Maana niliuluzia samosa Bei niliyoambiwa haikulingana na nilichokiona .
 
Mabasi mazuri kusini yapo muda tu sema labda huduma mbovu maana nakumbuka miaka ya 2000 kulkuwa na basi kampuni ya NAJMA mbona lilikuwa bomba tu kwawaki ule??
Mwaka 2000 barabara ya Lindi ilikuwa ni mbaya sana , tena muda wa masika ilikuwa inafunga kabisa
Lindi Kama ukombozi.miaka ya 2013 14 na mabasi mazuri yalianza 2015 Kama sikosei
 
Mwaka 2000 barabara ya Lindi ilikuwa ni mbaya sana , tena muda wa masika ilikuwa inafunga kabisa
Lindi Kama ukombozi.miaka ya 2013 14 na mabasi mazuri yalianza 2015 Kama sikosei

Mwaka 2006 vipande vingi ndio vilikuwa vinaunganishwa hadi 2008 barabara tayari, na ukizungumzia mabasi mazuri unamaanisha ya kichina? Lakni hayo makampuni buti la zungu, wifi nae, najma yote yalikuwa na mabasi mazuri kwa wakati ule maana ukiondoa Scandinavia sehemu nyingi basi zilikuwa zafanana
 
Weka record zako vizuri , 2008 barabara ya Lindi bado ilikuwa mbovu, nimelala Siku mbili kipande cha nyamwage, mohoro kilikuwa na madimbwi ya kufa mtu
Halafu buti wifi nae na najma kwa Miaka hiyo walikuwa na Basi mbovu sana ,
Mabasi mazuri njia hiyo labda kuanzia mwaka 2013
 
Basi hazikuwa mbovu ila barabara ndio zilikuwa mbovu usiwe mbishi, NAJMA alikuwa na mabus mazuri tu tena enzi zile ilikuwa najma 2x2 hakuwa na basi mbovu
 
Kweli kabisa jamaa,ukifika pale daraja la mkapa unapewa na historia kidogo.

Sio basi safari nzima miziki na movie tu.
 
Basi hazikuwa mbovu ila barabara ndio zilikuwa mbovu usiwe mbishi, NAJMA alikuwa na mabus mazuri tu tena enzi zile ilikuwa najma 2x2 hakuwa na basi mbovu
Inawezekana tunatofautiana namna ya ku define Basi nzuri , Basi kuwa 2x2 sio kigezo

Inaonekana pia huijui kusini vizuri maana umesema 2008 barabara ilikuwa tayari wakati Miaka hiyo nyamwage hadi somanga ilikuwa madimbwi yanayomiliki Hadi kambale , Tunduru Basi zuri wameanza kupanda nadhan mwaka 2017 baada ya barabara kukamilika.

Hakuna namna ya Basi zuri ku operate kwenye barabara mbovu , mkishakuwa na barabara mbovu mtapanda mabasi mabovu tu, angalia Basi za kwenda newala na nachingwea na kigoma .
 
Back
Top Bottom