lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,485
Wakati wa vita ya Guba nilicheka kidogo pale vita ilipokua ngumu. USA iliilalamikia Russia kuwa,Russia imewagawia wanajeshi wa Iraki mawani za kuweza kuona usiku (gizani) wakati wao Wamarekani wanazo,Halafu waliilaumu Russia kwa kuwapa Iraki vifaa vya KUKWEPESHA malengo ( shabaha) kwani kila Wamarekani wakipiga maeneo fulani walikua wakikosa shabaha.Pia waliilaumu Russia kwa kuipa Iraki mitambo ya mawasilianao ambayo kila Wamarekani wakijaribu kunasa mawasilaano ya Askari wa Iraki,Askari wa Iraki waliweza kubadili mawasiliano hivyo kuwapa wakati mgumu wanajeshi wa Marekani.Lakini vyote hivyo Russia alikana alisema hajampa Iraki.Sasa kiliconichekesha ni hivi.Marekani alitaka kupigana vita vyepesi kwa taifa dhaifu kama Iraki wakati yeye akiwa na kila aina ya vifaa vya kivita tena vya hali ya juu sana.Yeye askari wake karibu wote walikua na miwani wakati Iraki ni watu wachache tu tena nadhani ni baadhi ya wale Rupublican Guards.Hivyo Super power analalamika kua nchi ndogo kuwa na miwani za kuona usiku,kuwa na vifaa vya kupoteza malengo na kuwa na vifaaa bora vya mawasiliano.Kichekeso ni kama Timu ya taifa ya Ujerimani yenye kila kifaa cha soka inapokutana na Taifa stars iliyoyopewa pengine msaada wa viatu vya kuchezea kwenye mvua halafu German iilaumu labda Spain kuipa Taifa Stars viatu vya kuchezea wakati mvua ikinyesha.Ni maajabu,Hapo sasa Super power alitamani nci ndogo kama Iraki isiwe na silaha ili apigane kwa kiulaini.