US Naval Bases In Africa (AFRICOM): Sababu, Pingamizi, Faida na Hasara

aisee na sasa wale wote ambao hawajazoea kuvaa suti na kuwa kuwa smati wajimini muanze kukwepa kuwepo maeneo ya town wajimini..as kama wengi walivyosema hapa hamkawii kwenda jilia suna la buree kule segerea na keko..hata kama una ka stationery town wajimini zoea zoea tuu kupiga formals ama suti hata ka haina ac...la sivyo mtazidi ichukia serikali yenu...

sasa clinton road zilidekiwa arusha je huyu ambaye anaweza go lala kilimanjaro hotel pale (jina la zamani) si bahari ile inaweza sijui ikafanywaje sijui maanaa...

na wajimini mkiona wazungu wamezidi zidi huko bongo now msishangae ndio mjue watu wako kazini tayari huwa watumwa kabla kabsaaa na ka safari ni february wanaweza kuwa tayari washafika kuweka kambi...

i cant immagine jinsi jiji litakavyokua na pilika pilika bin foleniz..as mie nakumbuka wakati mama bush alipokuja tz ndio mie niliingia bongo siku hiyo masaa machache before u cant immagine how siku hiyo the airport was...halafu immagine wafika pale huna habari kuwa mama bush atatua soon...mwee huduma zilikua faster hizo jus kumake sure pipo wasiwe near the area iitwayo airport....
 
Aje na Balali la sivyo hatutampokea kama anawaficha wahalifu huko kwake na kuanzia sasa tuanzishe kampeni ya kumwambia kuwa kuja kwake hapa patakuwa salama kama Balali atakuwa amekuja naye .

Mkuu Kieleweke,

Salute!
 
Na kule middle east ( Israel, Palestine ) na kule Saudia na U.A.E alipokanyaga kwa mara ya kwanza nako kunaangukia kwenye "dalili ya dharau kwa bara lao"

Bush returned Jan. 16 from an eight-day trip to Israel, the Palestinian-governed West Bank, Kuwait, Bahrain, United Arab Emirates, Saudi Arabia and Egypt. He plans at least a half dozen more trips to the Middle East, Asia, Europe and South America before leaving office next January.

Umenielewa sasa? Sisi ni haka ka whistle stop tour lakini kwenye umuhimu ataenda zaidi ya mara sita kabla ya kumaliza muda wake. Bado unaamini tuko at par na hawa wengine?
 
Na hapo ndo utaona vyombo vya usalama vya bongo viko POWERLESS kwani walinzi kwa sehemu zote Kichaka atakazokwenda watakuwa US tupu. Hata JK anaweza kusachiwa wakati wanaingia IKULU.

Kwani sisi tuna walinzi?

Si afadhari enzi yetu ya jeshi la Mgambo hata bunduki tulifundishwa kushika vizuri?

Hawa vijana wa kurinda Rais wamenenepa matako tu watamlinda nani?

kazi ile unatakiwa kuwa ngangari
 
Sas wapo dar kwa zaidi ya wiki 2. Wengi wa walio ingia sasa hivi ni wala wanaoongea kiswahili fasaha, wanajipenyeza kila kona mpaka uwanja wa Fisi.

halafu wale walioko kwenye Payroll yao huu ndo wakati wa kupeleka kila aina ya Information hasa kuhusu vile videvu kubwa vya Kariakoo.
Inawezekana Osama anatafutwa kila pembe ya dunia kumbe kajaa tele Kariakoo.
 
Mimi kama mwanainji wa inji hii nisingependa huyu kichaka akanyage inji hii.

Na pia kwa niaba ya wazee wa Kirarachi hapa moshi napenda kutuma ujumbe huu kwa wana JF
Shimboni maee!! kimana kyamfeo luimbe haleluya na lusanjo njonyamari tsadu tsose. Ngamulangienyi maka mhya fo mbora na seko.
 
sasa machinga wataanza kunyanyasika ukiuliza utaambiwa bush anakuja kaazi kweli kweli
 
.....katika muda atakao kua hapa muda mwingi atautumua kwenye mahoteli ya kifahari huko porini..arusha ..sio town...dar itakuwa reception two..hope he will have three days here ..it a lot for a seating american president...nadhani anapenda kwenda kuona sehemu ambazo binti zake walivyokuja last time walivutiwa sana hadi wakampigia simu live kumueleza how excited they were...
 
Nimesoma taarifa ya ujio wa George W.Bush wa Marekani katika gazeti la Tanzania Daima


George Bush anakuja

na Mwandishi Wetu

HATIMAYE imethibitishwa kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi tano za Kiafrika ambazo Rais wa Marekani, George W. Bush, atazitembelea katika ziara yake ya siku sita barani humu.
Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini jana, ilizitaja nchi nyingine ambazo Rais Bush atazitembelea kuwa ni Benin, Ghana, Liberia na Rwanda.

Taarifa hiyo ilisema kuwa ziara hiyo ya Rais Bush inadhihirisha ushirikiano wa karibu uliopo kati ya Marekani na bara la Afrika.

Ziara hiyo ya siku sita imepangwa kuanza Februari 15 na kukamilika Februari 21, mwaka huu. Katika ziara hiyo, Rais Bush anatarajiwa kuzungumzia masuala mbalimbali, hasa jinsi ambavyo nchi yake imekuwa ikilisaidia bara la Afrika.

Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kapteni John Chiligati alisema kuwa, Kamati Kuu ya Taifa imepokea taarifa toka kwa Rais Jakaya Kikwete kuwa Rais Bush anatarajia kufika hapa nchini Februari 16 na anatarajiwa kukaa hadi Februari 19 akiwa katika ziara ya kikazi.

Chiligati alisema kuwa Kamati Kuu imepokea kwa heshima taarifa hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa Marekani imekuwa ikiisaidia nchi yetu katika maeneo mengi.

“Ziara hii tuitumie katika kuimarisha uhusiano wetu na Marekani, wananchi wajiandae katika ugeni huu mkubwa,” alisema Chiligati.

Taarifa ya Ubalozi wa Marekani ilisema kuwa, moja kati ya mambo yatakayozungumzwa na Bush ni pamoja na Mpango wa Dharura wa Rais wa Kupunguza Makali ya UKIMWI (PEPFAR) na Mpango wa Rais wa Kupambana na Malaria (PMI).

Ukimwi na malaria ni kati ya magonjwa ambayo yanagharimu maisha ya watu na uchumi wa bara la Afrika.

“Marekani ndiyo nchi inayotoa misaada mingi zaidi kwa Tanzania; katika mwaka 2008 peke yake, thamani ya misaada ya Marekani kwa Tanzania ni zaidi ya dola milioni 648,” inasema taarifa hiyo ya ubalozi.

Aidha, ubalozi huo, unabainisha kuwa tangu 2003, Marekani imetoa kiasi cha dola milioni 818.4 kusaidia vita dhidi ya ukimwi nchini Tanzania. Katika kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria, Marekani imetoa misaada ya dola milioni 76.5.

Akiongelea kuhusu misaada inayotolewa na Marekani kwa Tanzania, Rais Bush alisema: “Moyo wetu wa kujali unapaswa kudhihirishwa kwa kuwasaidia watu wanaotaabika na magonjwa… tuna mkakati ambao unafanya kazi: Ni kuunga mkono mkakati ambao umeleta tofauti katika maisha ya watu zaidi ya milioni moja, katika kipindi cha muda mfupi.”

Taarifa hiyo ilisema kuwa ziara ya kihistoria ya rais huyo wa Marekani nchini Tanzania, itaimarisha zaidi uhusiano uliopo kati ya wananchi wa Marekani na wananchi wa Tanzania.

Taarifa hiyo ya ubalozi ilieleza pia katika ziara hiyo, Rais Bush ataambatana na mkewe, Raula. Aidha, katika kila nchi atakayofika atakutana na kufanya mazungumzo na marais kuhusiana na ushirikiano, demokrasia, fursa za kiuchumi, uwekezaji na haki za binadamu.

Sisi watanzania wa kawaida tuna sababu yoyote ya kujiandaa na ujio huu?

Ushirikiano: Kituo cha kijeshi?
 
Hivi Bush anakuja kama mgeni wa serikali au mgeni wa CCM? Nimeuliza kwa sababu namwona Chiligati akipokea taarifa hiyo kwa heshima, au?
 
Kichaka anakuja kuhakikisha kuwa TZ hawafanyi biashara na Iran na Korea.....check hii news...
New Uranium discovery in Tanzania

1 2 3 4 5 (0 votes) Written by Asia Business News
Friday, 18 January 2008
 
Hakuna matata...Karibu Africa Katika Mwezi huu wa wapendandanao..
Nasikitika sana Kwamba Tony Hakufanya hivyo..Japo Mlionekana wote Kuhaidi hivyo...

Labda Tony atakuja This summer!!
 
Hakuna matata...Karibu Africa Katika Mwezi huu wa wapendandanao..
Nasikitika sana Kwamba Tony Hakufanya hivyo..Japo Mlionekana wote Kuhaidi hivyo...

Labda Tony atakuja This summer!!

Huyu Bushi anakuja hapa kutuletea nini? au kuchukuwa nini?

Majibu:

1)haipiti siku 90 kuanzia bushi amalizapo ziara ya Tanzania mtasikiya kuwa, Tanzania yamegunduliwa mafuta kwa wingi.

2) haipiti siku 60 toka aje mtasikia Tanzania wametiliana mkataba wa amani na Merekani na merekani wamepewa kisiwa au ardhi ya kufunguwa besi yao ya kijeshi.

3) Tanzania kunaanza kuchimbwa uranium.

Hizo ndio sababu zinazomleta Tanzania. Tutakumbushana siku zinavyokwenda!
 
SAWA...Mbona sisi Raisi alipo kwenda Haikupita siku nyingi Matangazo ya TV kuitangaza Tanzania ndani ya America Yaka anza...

Haya Hebu tuone...
 
Kituo cha kijeshi cha Afrika kinataka kijengwe Bongo na pia uranium wanataka kuhakikisha wao watakuwa na umiliki wa namna moja au nyingine ili isiangukie mikononi mwa 'magaidi'
 
Kituo cha kijeshi cha Afrika kinataka kijengwe Bongo na pia uranium wanataka kuhakikisha wao watakuwa na umiliki wa namna moja au nyingine ili isiangukie mikononi mwa 'magaidi'

Kuna gaidi zaidi ya Bushi alyeuwa watoto zaidi ya million Iraq, kwa kosa gani? Au walikuwa magaidi? au walikuwa na silaha za maangamizi? au walienda kulipuwa marekani? au ni kwa ajili ya mafuta yao? au simply kwa dini yao? au, au, au...
 
SOURCE: BBC LONDON JANA JIONI
MWANANCHI

JANA KATIKA KIPINDI CHA MATANGAZO YA JIONI KULITOLEWA MATANGAZO RASMI YA SERIKALI KUHUSU UJIO WA RAIS BUSH,MOJA KATI YA VITUKO VILIVYOJILI NI MAVAZI AMBAYO WAANDISHI WA HABARI WANATAKIWA KUVAA SIKU HIYO. KULIKONI IWE BUSH TURais Bush wa Marekani kukaa Tanzania siku nne ziara ya Afrika
*Kutembelea Arusha, Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu


Rais George Bush anatarajiwa kukaa kwa siku nne nchini Tanzania kati siku saba za ziara yake kutembelea Bara la Afrika.


Akizungumza katika kikao cha wahariri kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jana, Msemaji wa ubalozi wa Marekani nchini, Jeffery Salaiz alisema katika ziara hiyo Rais Bush atatembelea mikoa ya Dar es Salaam na Arusha.


Alisema kwamba ziara hiyo ina malengo makuu matatu, ambapo kwa pamoja yanadhihirisha nia ya Marekani kuijali Afrika.


Wakati wa ziara hiyo, Bush atakagua baadhi ya miradi mbalimbali ambayo serikali chini ya uongozi wake imekuwa inasimamia na kufadhili kwa karibu.


Alitaja miradhi hiyo kuwa ni ya Ukimwi na Malaria ambayo kwa sehemu kubwa imesaidia idadi ya wagonjwa na vifo vitokanavyo na malaria katika Visiwa vya Pemba.


Rais Bush anatarajiwa kuanza ziara ya kutembelea nchi tano za Afrika kuanzia Februari 15 hadi 21. Nchi hizo ni Benin, Tanzania, Rwanda, Ghana and Liberia.


Marekani ni moja ya nchi ambazo ni wafadhili wakubwa kwa Tanzania, ikiwa imetoa Sh700 bilioni kwa mwaka huu. Kuanzia mwaka 2003 Marekani imetoa zaidi ya Sh700 bilioni kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya Ukimwi.


Katika mradi wake wa kupambana na malaria, Marekani imekwishatoa zaidi ya Sh77 bilioni.


Ziara ya Bush inatarajia kujenga uhusiano mzuri kati ya nchi hizi mbili na kuitangaza Tanzania duniani kwa kuwa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa wanatarajiwa kuaambatana naye.


Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Marekani kukaa Tanzania kwa siku nne kwani mara ya mwisho Rais wa nchi hiyo, Bill Clinton alipotembelea nchini mwaka 2003 alikaa nchini kwa masaa matatu tu.
 
Back
Top Bottom