Us embassy na vioja vya baadhi ya wafanyakazi

Re: Us embassy na vioja vya baadhi ya wafanyakazi

pole sana mwanamapinduzi,
hebu tuanze kufikiria kujiajiri hata kama hatuna mitaji, tujaribu kufikiria utauza nini ili upate chochote na usivunje sheria,
nchi yetu bado mbichi sana
it is better to start from the scruch .
usifikirie mambo makubwa sana . mfano hebu fikiria azam anauza icecream na anapata hela
hata wewe unaweza uza hata samaki, maandazi, hata mapapai au machungwa na ukatoka haya ni mawazo yangu tu. kamayatakukera
nisamehe ila nachukia sana watu wanavyo nyanyasika maana hata mimi nyamenitokea sana. pole sana.
hili ndilo soko holela.

Wewe ni shujaa, wewe ni mwanaharakati, wewe ni mtu makini, hivyo ndiyo navyoweza kuanza kujibu post yako. Mtu mzima, mawazo ya kuajiriwa nimeshaondokana nayo muda mrefu sana (mtu mwingine najua atahoji why attending interview and all these complains-Hicho si kigezo wala si sababu), nimefanya kazi karibu 6 years kwangu mimi nimeshachoka sana, na mahali fulani nilifanya kwa 4 years consecutively nilikuwa tayari nimechoka to the extent ilifika mahali nataka kuandika resignation in 24 hrs bila sababu yoyote nyingine zaidi ya kuchoshwa na mazingira yale yale ya kazi, kazi zilezile, watu wale wale, ofisi ile ile, meza, computer, vitendea kazi etc. Hivyomawazo ya kuajiliwa ni 5% katika maisha yangu, na tayari nilishachukua hatua naendelea vyema.
Nimefurahi sana kwa ushauri wako mkulu, na nijuavyo mimi wewe utakuwa mjasiliamali wa ukweli. Hebu niku-pm tupeane strategies.
Waitwao wasomi wengi wa Tanzania wameishia kuonekana smart sana kwa mavazi lakini ni matatizo matupu, mishahara wanayolipwa, benefits wanazopata ni nonsese, there are very few ambao wanaweza simama na kusema we achieved in employments, but majority hakuna kitu, ucharwa mtupu. Vijana wengi wameingia mikopo ya kununua mitumba ya magari, na usiku hawana hata pa kuyalaza zaidi ya za ofisi za chama au Polisi...aibu sana. Na mwisho wa siku kwa sababu ya mishahara isiyotosha wamekuwa kwenye frustration nyingi sana.
Tunahitaji kuubadirika sana katika fikra zetu ili kujikomboa.
Stay blessed.
 
ur absolutely true bro. It's very confusing. Database shows Interview was scheduled from 8pm to 2pm, at the same time at 11:20am am told they are almost done. At the same time again, i was told i will last for 1hr.i.e. from 11:15am-12:15am.....pagumu sana.
Natumaini hizo ni typo mkuu..!
 
Kulikuwa na breakdown ya communication hapo. Walipokupigia simu walikuambia interview itakuwa “Tuesday 2nd May around 11am” which is wrong because tarehe 2 May ilikuwa Jumatatu. Kuna possibilities mbili hapo. Either wewe hukusikia vizuri or aliyekupigia simu alikosea kwa kukusudia au kutokusudia. Aliyekupigia simu alikuwa anaongea Kiingereza chenye accent ya kimarekani au ya kibongo? At the end of the day, only records of the conversation will enable us to know who made the blunder. Lakini kuna issue nyeti zaidi which need to be explored.

Unasema ulipoenda ubalozi walikuambia kuwa interview itakuwa Tuesday 3rd April. Ina maana mwezi mmoja nyuma? Au ulimaanisha Tuesday 3rd May? Whatever the date, pia walikuambia interview itakuwepo kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 8 mchana. Nilivyoelewa hapo ni kwamba huo ndio muda uliopangwa siku hiyo kwa ajili ya interview. Kila mtu hapo atakuwa alipangiwa muda wake.

Wakati ulipokwenda ubalozini kwa mara ya kwanza kwa nini hukuwaliza pia interview yako itakuwa saa ngapi? Kama tarehe waliokupa mwanzo ilikuwa imekosewa, then it is also likely that muda wako wa interview utakuwa ulikosewa pia. Inaonyesha ulichofanya wewe baada ya kupewa tarehe mpya, ulidhani muda wa interview utakuwa ule ule uliopewa mwanzoni kwenye simu (11am). Kwa nini uliuamini huu muda uliotajiwa mwanzoni kama ni sahihi? Why did you only verify the date but not also the time for the interview? Pia umesema uliambiwa interview intaanza saa “11:15am-12:15am”? Una maana kuanzia saa tano asubuhi mpaka saa sita za usiku? I am lost here.

Na huyo mtu ambaye wanasema aliwasiliana na wewe kukuambia ufike saa 4 asubuhi na kuwa interview itaanza saa 4:15 mpaka saa 5: 15 asubuhi ni yupi? Ni yule aliyekupigia simu au ni yule aliyekupatia tarehe mpya ulipokwenda ubalozini?

My observation ni kwamba kama ulienda ubalozini kuverify tarehe sahihi ya interview (ambayo ulipewa) lakini hukuverify pia muda wa interview (ukidhania kuwa muda uliombiwa mwanzoni kwenye simu ni sahihi) then, you should also carry the blame.

Posts zako nyingine pia zinanichanganya. Umesema kuwa the “Database shows Interview was scheduled from 8pm to 2pm, at the same time at 11:20am. am told they are almost done. At the same time again, i was told i will last for 1hr.i.e. from 11:15am-12:15am” Una maana kuanzia saa mbili usiku mpaka kesho yake saa nane mchana? Hata kama ulikuwa unamaanisha from 8am to 2pm, still huo ndio muda waliokuwa wameutenga kwa ajili ya interview ya watu wote, na sio wewe tuu. Interviews zinawezwa kumalizwa kabla ya muda uliopangwa kulingana na idadi ya interviewees waliohudhuria.

Pia nashangaa watu wanatoa pole tuu bila hata kusoma jinsi mtoa mada anavyojichangaya kwenye posts zake. Kama interview yenyewe ingekuwa na maswali ya kuandika saa kwa kingereza, then kwa mantiki hii sidhani kama ungepita. I am sorry for sounding so cruel but I am responding to what you wrote. Otherwise, you need to clarify what you said above especially the times.

Ninafikiri kuna point hapo...kosa ni wewe kuassume kwamba interview itakuwa saa tano tarehe 3 kama walivyokupigia simu, pia ilipofika pale ilibidi uwaeleze kuhusu ile simu uliyopigiwa pamoja na confusion zake na kisha uombe mwongozo unaoeleweka.....pia walipokuambia ni tarehe 3 may kuanzia saa mbili mpaka saa nane ilibidi ufike pale asubuhi. Anyway masaibu yameshakukumba na unayoweza kufanya ni mawili, mosi kumuandikia barua balozi wa marekani hapa tanzania umueleze mambo yote hayo japokuwa kutakuwa hamna ushahidi wa kutosha lakini hilo litawasha taa vichwani mwao na watakuwa makini siku zijazo, pili, siku yoyote ukiitwa kwenye interview ya muda flani uende masaa mawili au matatu kabla ili kukwepa ubabaishaji.
 
Ndugu
hao ni wale wale watanzania wenzako wanakinaisha mbaya si hapo tu yaani ogopa kupiga simu bora ajibu kwa msg ubaki na ushahidi ma dear................................................................
Watanzania wana roho mbaya kama mavi hasa wakikamata nafasi za hr ama secretary..nakwambia waone mambo yanahusu ajira ama cheki lohh ni shida kweli hizi kazi zingine zinaitaji wito wa mungu kwa kuwa wanagaiana na mameneja shida tupuu....
 
Samahani sana uliyeleta hii mada pole kwa msumbuko, ila nakuomba ujisahihishe kwenye kuandika kimombo umekosea sana na imefanya ubadili maana uliyotaka kuitoa

Sasa nakushauri uwe unasoma unachoandika na kama unaona hauelewi basi edit kama unaelewa na abdo kuanika uwanjani uliyokosea nakuomba ujitahidi kujifunza mengi kusoma online kutumia dictionary kujifunza masaa kwa kiingereza etc

Kwa mimi naona unaweza kuwa haukuelewa mengi ya ulichoambiwa naomba ukae chini na utaona mwenyewe

Na pia kama bado unahuakika 100% una haki ya kulalamikia embassy na kuwaeleza experience yako uliyopata andika e-mail iende kwa balozi na cc kwa watu wengine google hata ofisi zao za US na hii itasaidia wajirekebishe.
 
Habari wana JF.
Leo nakuja na story hii: Muda huu nikiandika ujumbe huu natoka Ubalozini kwa lengo la kufanya usaili (Interview) wa kazi. Ijumaa ya tarehe 29 April majira ya saa 4 asubuhi nilipokea simu ya kupewa taarifa. Taarifa ilikuwa hivi"
Us Embassy: Are you Mr.....?
Mimi: yes..........
Us Embassy: Did you applied for ......job,
Mimi: Yes i did
Us Embassy: Your required to attend the English language test (interview) on Tuesday 2nd May around 11am, we advise to be there at least 15 minutes before time, the interview will last for 1 hrs.
Mimi: Ok. Thank you and i appreciate for your consideration:

Nilichofanya: Niliandika kwenye Diary yangu kwa kumbukumbu, masaa 2 baada ya simu hiyo nikastuka tarehe na siku vinatofautiana, nikajaribu kupiga simu kupata uhakika tena, bahati mbaya simu haikupatikana. Niliamua kwenda Ubalozini jumatatu kwa malengo mawili, 1. Kuhakiki tarehe, siku na muda. 2. Kama nitakuta kuna interview kwa maana ya tarehe 2 April nitafanya. Nilifika receiption nikaeleza shida yangu na walipoangalia database yao waliona jina langu na nilikuwa scheduled Tuesday 3rd April na wakasema interview ipo kuanzia saa 2 asubuhi mpaka 8 mchana. (Nili note kwamba kama interview ni ya saa 1, basi tutakuwa katika ma group tofauti na mimi nitakuwa kwenye ule muda niliotajiwa tangu mwanzo)

Leo nimekwenda kwa maana ya kuzingatia muda ule wa saa 5 asubuhi. Nimefika hapo nikaambia nimechelewa na wenzangu wanakaribia kumaliza. Nikahoji iweje nimechelewa na muda nilioambiwa ndo huu? na hii si mara yangu ya kwanza kuitwa kwa interview hapa. Wakaomba wacheck then watanipa mrejesho nyuma (Feedback). Baada ya 5 minutes nikaambiwa tunasikitika mtu uliyewasiliana nae anadai alikwambia ufike saa 4 asubuhi na interview itaanza saa 4:15 mpaka saa 5: 15 asubuhi hivyo umechelewa.

Observation:
Nilipoongea na walinzi walionyesha nyuso za mashaka flani, na wakasema kuna wengine wamerudishwa kwa sababu kama hiyo hiyo-kuchelewa. Na walioingia kwa interview ni watu 12 tu.
Swali: Hivi ule uzushi na zengwe tulilozoea huku uswahili kwetu (Private sector i.e. NGOs, Companies, na mpaka serikali) imeshafika mpaka kwa wenzetu? na kama ni hivyo, ni kwa sababu tu wanaofanya kazi huko bado ni watanzania wenzetu au kuna uzembe flani kwa baadhi ya wafanyakazi hapo Ubalozi?

Pole sana ndugu yangu kwa yaliyokusibu lakini ninachoweza kukwambia hilo ndio zengwe la wenzetu lilivyo nikiimanisha hakukuhitaji tena ila tu hawakuwa na namna ya kukwambia straight! Hayo nshakutana nayo hata ughaibuni...pole mkuu!!
 
pole mkuu. Hapo wanatafuta jinsi ya kukukwepa ili interview waingie watu wao tu!
 
Acheni unafiki na kum discourage mshikaji,cha msingi kila mtu ana mipango yake kimaisha,unaweza kuajiriwa pia maisha yako yakawa mazuri kuliko mjasliamali pia hata mjasiriamali anaweza kuwa na maisha bora kuliko mwajiriwa, cha msingi ni wewe mwenyewe kuwa na mipango yenye ufanisi.
 
... Did you applied for ......job,
...Your required to attend....

... Did you applied for ......job, (ULITAKIWA UANDIKE "DID YOU APPLY...", sio "DID YOU APPLIED...")

...Your required to attend.... (ULITAKIWA UANDIKE "YOU ARE REQUIRED...", sio "YOUR REQUIRED...")

Kwa kuwa ilikuwa ni English Language test, bila shaka hiyo nafasi haikuwa riziki yako, maybe ungeikosa kwa makosa kama hayo. Najua Language tests huwa zinahusisha uwezo wa kusoma, kuandika, kuongea na kusikia! Pole sana ila samahani kama post hii itakukwaza!
 
Mkuu naoma nikuulize swali. Ulipogundua kuwa tarehe mbili ilikuwa Jumatatu na sio Jumanne ulienda ubalozini. Wakaangalia database yao wakakuta interview yako ilikuwa scheduled Jumanne 3rd May. Pia kama ulivyosema walikuambia kuwa interviews zitakuwa kuanzia saa 2 asubuhi mpaka 8 mchana. Je, uliwauliza interview yako itakuwa saa ngapi? Kama uliwauliza walikujibu itakuwa saa ngapi?

Hapo kwenye red unaposema 11:15am to 12:15am kuna tofauti ya zaidi ya saa moja hapo. Saa 6 usiku kwa English ni 00:00am kama umeset clock kwenye 24-hour format. Lakini kama umeset clock to 12-hour format then saa sita usiku itakuwa 12.00am.

Kwa faida ya wana JF, hapo kwenye red, ukishaweka masaa katika format ya masaa 24, basi hakuna tena cha am wala pm. Hivyo saa sita usiku ni 00:00 na si 00:00am. Format ya masaa 24 inaondoa kabisa matumizi ya am na pm.
 
Pole sana Mwanamapinduzi,

Matatizo hayo yapo sana kwenye balozi za wageni zilizopo nchini. Mimi mwenyewe nimeshakumbana na matatizo kama hayo kwenye Ubalozi wa India hapa nchini. Japo langu halikuwa la kazi.Suala langu lilikuwa kuomba nafasi na udhamini wa kwenda kusoma Shahada ya Uzamili India. Cha kushangaza, walichukua mtu ambaye hata rekodi zake za O level na A Level achilia mbali za Bachelor hazina mashiko kabisa wakaniacha mimi mwenye Daraja la Kwanza O na A level na Upper Second ya GPa 3.8 (Sheria Mlimani). Nilipofanya uchunguzi sana nikaambiwa wale weusi wenzetu wanaofanya kazi pale wanawamegea mapande ndugu zao. Mwaka huu pia kuna Bwana mdogo wangu aliomba kwenda kusoma India Bsc. in Compuetr Science na alikuwa tayari ana Diploma ya Computer Science. Wakampigia pande jamaa wanayefahamiana naye mwenye III akapeta. Dogo alipomvaa jamaa mmoja anaitwa Sanjev Manchanda pale ubalozini jamaa alikuwa anashindwa hata kujieleza. Nadhani nao wanafaidika kwa Commission fulani hivi.

Ubalozi wa pili ni Ubalozi wa Sweden, nina jamaa ana aunt yake pale, alipata admission ya kusoma Masters Sweden na Ubalozi ukampa Scholarship,mimi nilipokwenda kujaribu kuulizia,wakasema (waswahili wenzetu) kuwa ubalozi hauna arrangement kama hiyo, yaani kwa kweli bongo ni maudhi tupu
 
Wewe ni shujaa, wewe ni mwanaharakati, wewe ni mtu makini, hivyo ndiyo navyoweza kuanza kujibu post yako. Mtu mzima, mawazo ya kuajiriwa nimeshaondokana nayo muda mrefu sana (mtu mwingine najua atahoji why attending interview and all these complains-Hicho si kigezo wala si sababu), nimefanya kazi karibu 6 years kwangu mimi nimeshachoka sana, na mahali fulani nilifanya kwa 4 years consecutively nilikuwa tayari nimechoka to the extent ilifika mahali nataka kuandika resignation in 24 hrs bila sababu yoyote nyingine zaidi ya kuchoshwa na mazingira yale yale ya kazi, kazi zilezile, watu wale wale, ofisi ile ile, meza, computer, vitendea kazi etc. Hivyomawazo ya kuajiliwa ni 5% katika maisha yangu, na tayari nilishachukua hatua naendelea vyema.
Nimefurahi sana kwa ushauri wako mkulu, na nijuavyo mimi wewe utakuwa mjasiliamali wa ukweli. Hebu niku-pm tupeane strategies.
Waitwao wasomi wengi wa Tanzania wameishia kuonekana smart sana kwa mavazi lakini ni matatizo matupu, mishahara wanayolipwa, benefits wanazopata ni nonsese, there are very few ambao wanaweza simama na kusema we achieved in employments, but majority hakuna kitu, ucharwa mtupu. Vijana wengi wameingia mikopo ya kununua mitumba ya magari, na usiku hawana hata pa kuyalaza zaidi ya za ofisi za chama au Polisi...aibu sana. Na mwisho wa siku kwa sababu ya mishahara isiyotosha wamekuwa kwenye frustration nyingi sana.
Tunahitaji kuubadirika sana katika fikra zetu ili kujikomboa.
Stay blessed.

Hapo red ni kigezo ndugu yangu, huwezi ukasimama publicly kusema mawazo ya kuajiriwa yameisha wakati unaendelea kusaka ajira kwa usongo mkubwa ! Unless ufafanue unamaanisha nini ? Pia, ujasiriamali si jambo jepesi, linahitaji uvumilivu na pia ujasiri. Kama kukosa tu hiyo interview unajaa temper namna hii je ndani ujasiriamali ndio itakuwaje ? Maana huku nako kuna kujuana kusiko na mfano ndio uweze kufanya dili zako vinginevyo lazima umwage mlungula wa kutosha, na kwa kila unachofanya TRA wapo mgongoni kwako, so unatakiwa uslow down na temper kama kweli unategemea ujiunge katika kundi letu la ujasiriamali.
 
... Did you applied for ......job, (ULITAKIWA UANDIKE "DID YOU APPLY...", sio "DID YOU APPLIED...")

...Your required to attend.... (ULITAKIWA UANDIKE "YOU ARE REQUIRED...", sio "YOUR REQUIRED...")

Kwa kuwa ilikuwa ni English Language test, bila shaka hiyo nafasi haikuwa riziki yako, maybe ungeikosa kwa makosa kama hayo. Najua Language tests huwa zinahusisha uwezo wa kusoma, kuandika, kuongea na kusikia! Pole sana ila samahani kama post hii itakukwaza!

Kaka nakubaliana na wewe kwa 100% na wala siwezi kukwazika na hili post yako hata kidogo kwani lengo ni kukosoa na hatimae kuboresha/kujifunza. Kumbuka at the time naandika hii post ni muda mfupi mara baada ya kutoka US Embassy, hivyo unaweza ku-weigh out nilikuwa katika hali gani. Wakati huo huo nimeahirisha mipango niliyokuwa nayo na iliyonihitaji kukutana na watu tena muhimu sana, na kwa issue ambazo ni nyeti sana. Anyway, bado nikushukuru kwa observation yako. Lakini ikumbukwe pia, hapa suala li kupata hiyo kazi, issue ni kwanini iwe hivyo. Watu wachache wame-concentrate na issue ambazo si za msingi wala kiini cha tatizo (Typing errors, Time, grammar e.t.c), najua hayo pia yana maana lakini kwa wakati wake na kwa mada husika.
Naomba niwashuru wote kwa michango yenu.
Hitimisho: Ninaandika barua kwa ubalozi kutoa dukuduku langu ili hali hii isije kujitokeza hata kwa watu wengine (Ikumbukwe nikiwa Ubalozi, walinzi walishangaa pia kwanini leo watu wengi wamechelewa, na walioingia kwa interview idadi yao ilikuwa 12).
Moderator: Naomba mjadala huu uishie hapa. Asanteni sana.
 
Hapo red ni kigezo ndugu yangu, huwezi ukasimama publicly kusema mawazo ya kuajiriwa yameisha wakati unaendelea kusaka ajira kwa usongo mkubwa ! Unless ufafanue unamaanisha nini ? Pia, ujasiriamali si jambo jepesi, linahitaji uvumilivu na pia ujasiri. Kama kukosa tu hiyo interview unajaa temper namna hii je ndani ujasiriamali ndio itakuwaje ? Maana huku nako kuna kujuana kusiko na mfano ndio uweze kufanya dili zako vinginevyo lazima umwage mlungula wa kutosha, na kwa kila unachofanya TRA wapo mgongoni kwako, so unatakiwa uslow down na temper kama kweli unategemea ujiunge katika kundi letu la ujasiriamali.

Hahahah! Entrepreneur wangu umenifurahisha sana. Well, naposema si kigezo lengo langu nikueleza issue hapa si mimi kukosa hiyo interview, issue kwa nini wafanye uhuni wa namna hii? Maana yake ni kwamba itatokea kwa watu wengine, na kama ni hivyo kwanini wapote muda wa mtu. Ukweli i was furious kwasababu niliahirisha kikao cha majadiliano ya mambo muhimu sana ambacho kilipaswa kufanyika asubuhi hiyo hiyo ya siku ya interview na kiliahirishwa.
Kuhusu Ujasiliamali najua hilo kaka kwasababu nimo tayari katkia hilo, hivyo lugha unayoiongea naielewa vyema tu.
Ajira: Kama nilivyotangulia kusema, kwa kufanya kwangu kazi 6 years tayari nimejifunza vitu vingi pia si haba, hivyo naongea lugha ambayo kimsingi najua wapi nimesimamia, na kwa maana hiyo ndiyo maana nimekuwa so selective hata katika ku-apply au ku-attend interviews.
Conclusion: Nashukuru sana kwa post yako mkuu. Be blessed (Nitaku-PM for more discussion na kupeanana mikakati ktk ujasiliamali)
 
Poa kaka, nimekupata fresh. After all unavyoingia ktk ujasiliamali tokea kwenye ajira lazima uingie na steps za umakini, huwezi ukakurupuka kwa siku moja.

Cheerz !!
 
Toka mwanzo,pamoja na kuona hizo typos na grammars nilitaka niseme kitu kam hiki tu. Sijui kwanini ishu ikachukua path tofauti kabisaa...Andika complaints mkuu.si kwa ajili yako,ni kwa ajili ya wengine kesho. Huu uswahili upo kote duniani,lakini nchi hii umezidi sana,umeingia mpaka mahala usipodhani. Tangu Ikulu mpaka kwa balozi nyumba kumi kumi. Lini watu wanaostahili watakaa mahala wanapostahili? Andika,ila nina uhakika kama wataipata waswahili,wataichanilia mbali unless wawe na bifu wao kwa wao.
Hitimisho: Ninaandika barua kwa ubalozi kutoa dukuduku langu ili hali hii isije kujitokeza hata kwa watu wengine (Ikumbukwe nikiwa Ubalozi, walinzi walishangaa pia kwanini leo watu wengi wamechelewa, na walioingia kwa interview idadi yao ilikuwa 12).
.
 
Mkubwa nikupe pole kwa adha hiyo ya aina yake, kwenye maelezo yako nilivyoyapitia nikagundua baadhi ya mambo ambayo huenda ikawa chanzo (source) cha kukukosesha opportunity hiyo,
(1). Cha-kwanza nahisi labda wewe mwenyewe ulipata hamasa ya furaha ulipopata taarifa hiyo ya kuitwa kwenye interview kiasi usiamini kama hilo lingetokea kwako na ikafikia mahala ukajikita zaidi na wazo la kwenda kufanya i/view na ufahamu wa maelekezo mengine ukatoweka kwa hamasa hiyo ya furaha,
(2).Cha-pili huenda labda mtoa taarifa (ubalozini) au mpokea taarifa (wewe) mlipishana katika kuelewana katika lugha (kiingereza) japo simaanishi kwamba haujui / kufahamu kiingereza, (hili huwatokea wengi nikiwemo hata mimi) ndo maana ukataka kwenda kuhakiki siku hiyo ya j3 ili kujua uhakika wako wa siku ya interview.
Ninachoshauri kama rizki haipo mkubwa mahala hapo achana nao na usonge mbele na mabo mengine kwani mtoa RIZKI ni MUUMBA mwenyewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom