#COVID19 Urusi yaidhinishwa chanjo ya kwanza ya CoronaVirus duniani

Rais Vladimir Putin ametangaza kuwa Urusi imeidhinisha rasmi chanjo ya COVID19 iliyotengenezwa na Taasisi ya Galameya iliyopo Mji Mkuu wa nchi hiyo, Moscow

Akizungumza na Mawaziri kupitia mtandao, Rais Putin (67) amesema hii ni mara ya kwanza kwa chanjo dhidi ya CoronaVirus kuidhinishwa duniani

Ameongeza kuwa, chanjo hiyo imepitia hatua zote muhimu na kwamba binti yake aliyekuwa na homa ameitumia na anaendelea vizuri kwa sasa

Hata hivyo, Urusi haijatoa taarifa zozote za kisayansi kuhusiana na chanjo hiyo

===


Russia has officially registered a coronavirus vaccine developed by the Moscow-based Gamaleya Institute, President Vladimir Putin said on Russian state TV on Tuesday.

Speaking in a live teleconference with his cabinet ministers, Putin said the vaccine had gone through all the necessary checks.

The Russian President said one of his daughters has taken the vaccine; he said she had a slightly higher temperature, but that she now feels better.

Reports about Russia's vaccine have come amid concerns about its safety, effectiveness and allegations that the country has cut essential corners in its development.

Russian officials told CNN previously that crucial Phase III trials would take place after state registration of the vaccine.

Russia has released no scientific data on its vaccine testing and CNN is unable to verify its claimed safety or effectiveness.

Critics say the country's push for a vaccine comes amid political pressure from the Kremlin, which is keen to portray Russia as a global scientific force.

Source: CNN
KALAMAGANDA KABUDI Polofesa wa jalalani umesikia hiyooo. .
Jiandae kupeleka ndege yetu kubeba mzigo fasta mapemaa😅😅😅😅
 
Urusi ilituhumiwa siku za nyuma kufanya udukuzi kwenye makampuni ya dawa ya ulaya yanayotafiti chanjo ya Corona.

Nadhani ule udukuzi umelipa...😂😂😂... Urusi ya sasa ni dola ya kijasusi.
 
So this time The Russian Federation won the Vaccine-Race.
Urusi ni dola la kijasusi, taarifa zake ni za kutiliwa shaka siku zote (kumbuka zile tuhuma za wanariadha wake kutumia dawa za kuongeza nguvu) isitoshe inatuhumiwa kuiba taarifa kuhusu chanjo za Corona zinazofanyiwa majaribio na makampuni ya dawa ya ulaya.

Hii chanjo yao ni "Pandora box" kwa mahasimu wao wa magharibi.
 
Bwana Mbonde kutoka dunia ya tatu,anabishana na watu walio tengenezeza vitu kibao vya kisayansi.
Vaccine si rahisi ki hivyo tunvyoaminishwa taking into consideration kuwa viruses hawa have a high rate of mutation! Ngoja tuone, may be!
 
So this time The Russian Federation won the Vaccine-Race.

Russian scientist are formidable - hawavumi lakini wamo sana licha ya mataifa ya magharibi kuwapiga vita sana ili wasijulikane - wana wahujumu na kucopy uvumbuzi wa Warusi hasa katika masuala ya military hardware including aviation.

Kufanikiwa kwa Putin katika chanjo ya COVID-19 kutabezwa sana na utawala wa USA wakishirikiana na Big Pharma Companies pamoja na corrupt WHO wamekwisha anza dirty campaign zao mara waseme Warusi wame cut corners mara waseme Warusi wamefanikiwa baada ya kudukua data base za maabara za utafiti wa chanjo za huko Merikani na Uingereza!! Bottom line is: Mataifa ya magharibi notably US na UK ndio wanajiona wana akili sana kuliko mataifa mengine hapa Duniani. Vita vya kibishara kuhusu chanjo ya Corona ndio imeanza hivyo, tutasikia adithi nyingi za kutisha watu - masuala ya kuipiga vita Huawei yatajirudia
kwenye chanjo ya COVID-19.
 
Vaccine si rahisi ki hivyo tunvyoaminishwa taking into consideration kuwa viruses hawa have a high rate of mutation! Ngoja tuone, may be!
Sio virahisi kwako Mbonde wa dunia ya tatu,huko dunia ya kwanza wameinvest hela nyingi ktk tafiti mbalimbali,hao Russia sio wajinga wanachokifanya wanakijua.
 
Vaccine si rahisi ki hivyo tunvyoaminishwa taking into consideration kuwa viruses hawa have a high rate of mutation! Ngoja tuone, may be!
Nchi zaidi ya Ishirini zikiwemo zenye uwezo unaotambulika kisayansi zimeisha weka order ya mzigo wa chanjo hiyo. Sasa mkuu nchi zote hizi ni mbumbumbu kweli kiasi cha kuingizwa mtegoni na Russia? Jibu ni kuwa nchi hizi zinaamini Russia anaweza kufanya jambo hilo.
 
Chanjo inaitwa Sputnik jina kama la satellite yao ya kwanza.
Wanasema satelite ya Sputinik kipindi hicho iliamsha ari ya kisayansi duniani. Hivyo na chanjo yao hii itasaidia kuamsha ari ya wanasayansi kutafuta mbinu bora zaidi kukabilina na virusi jamii ya corona na vya aina nyingine duniani. Hii inaonyesha jinsi gani Russia wana nia ya heri na utu kwa dunia hii.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom