Urusi: Ndege iliyoanguka Misri ililipuliwa

Urusi: Ndege iliyoanguka Misri ililipuliwa

Sexer

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
8,513
Reaction score
8,276
Ndege iliyoanguka Misri ililipuliwa.
Urusi imethibitisha kuwa ajali ya ndege ya Metrojet iliyoanguka na kuua watu zaidi ya 200 katika rasi ya Sinai nchini Misri mwezi uliopita ilikuwashambulizi la kigaidi.

Mkuu wa idara ya usalama wa taifa Alexander Bortnikov amemualeza rais Vladimir Putin kuwa ndege hiyo iliangushwa na bomu lenye uzani wa kilo moja.
Bomu hilo lilikuwa sawa na ile yenye viungo vya TNT.

Abiria wote 224 waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliangamia.

Wengi wao walikuwa ni watalii kutoka Urusi waliokuwa wametokea Sham al Sheikh.

Bortnikov alipokamilisha maelezo yake kwa rais Putin, rais huyo pamoja na mawaziri wengine wakuu waliiunuka na kunyamaza kimya kwa muda kabla ya rais Putin kuapa kulipiza kisasi.

Aidha rais huyo wa Urusi aliapa kuwasaka na kuwaadhibu waliotekeleza mauaji hayo.

Putin pia aliapa kuendelea mashambulizi ya ndege nchini Syria.

Chanzo: BBC Swahili
 
Nini hapo kitakuwa kinaendelea? Je western countries ndio waliopanga tukio na kuangamiza abiria wote ili kumuonya Putin aachane na agenda yake kumsupport Asaad? Je inawezekana west walifadhili mpango huu kuikomesha serikali ya Moscow?

Hao terrorists wanaodhaniwa kufanisha tukio hili waliwezaje kupenyeza bomu ndani ya ndege wakati ulinzi mkali ulikuwepo?

Ngoja tuone hii game inavyoenda.
 
Mkuu nadhani hao ni IS!
 
Ila Nchi zikiungana kusema ukweli zitawafutilia mbali hao IS
 
Kwani bomu lilikuwa ndani ya ndege? au kombora limepigwa kutoka nje?
 
Siku za hawa mashetani yanosponsor isis etc zinahesabika
 
Kwa hiyo cia wako juu zaidi kuliko kjb. Si walikataa mpaka us walivyosema kuwa ilipigwa ndio leo wanakubari
 
nilisema tangu awali kuwa USA ni wajanja sana. RUSSIA atakuja kujilaumu kwa kukurupuka. Ninachokiona mbele yangu VITA YA SYRIA, RUSSIA IPO SIKU ATAJIKUTA ANAPIGANA PEKE YAKE.
 
Egypt says its experts are being joined by teams from Russia and also the Republic of Ireland, where the Airbus 321 was registered.
It crashed over the Sinai peninsula, killing all 224 people on board.
Egypt dismissed as "propaganda" claims that militants linked to Islamic State (IS) brought down the aircraft.
President Abdul Fattah al-Sisi told the BBC that it was too early to say what had caused the crash.
 
Sasa kwa nini mwanzoni walikataa?

Manake waliambiwa na Marekani hiyo ndege ilidondoshwa na bomu wao wakajifanya wajuaji.

Mwishowe wameisoma namba na kukubali.

USA baby:usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2:
 
Ila Nchi zikiungana kusema ukweli zitawafutilia mbali hao IS

sidhani kama ita-work. kumbuka kulikuwa na Al-Qaeda, sasa wapo Boko Haram, Al-Shabab. hujamalizana na hao wameibuka IS. who knows what follows next.

makundi yote ni kama vile yapo invisible na yana sympathizers wao kila pahala - wengine tunao ndani ya nyumba zetu na wengine tunalala nao vitandani mwetu kama wake au waume.

fight against terrorism should see beyond combative options. over the years, combativeness has done nothing but cause the innocent world play right into the terrorists' hands. terrorists have nothing to lose, while the world has - and the loss is always colossal!

there's no army - or super power for that matter - that can conquer over terrorism. none. zilch.

hivi kuna ubaya gani wa kukaa meza moja na hawa terrorists? mataifa mengi ya magharibi yanaamini katika Ukristo...kwa nini wasijifunze kutoka kwa yule mleta Ukristo mwenyewe (Yesu) ambaye alikula na kunywa katikati ya watesi wake? Yesu ambaye wafuasi wake walipomkata sikio mmoja wa watesi wake Yeye aliwakemea wafuasi na akamrudishia sikio mahali pake yule mtesi??

mataifa ya magharibi (na wafuasi wao) huwa wanasoma Biblia ipi??
 
Tunaambiwagwa russia ni hatari sana kijeshi, vp tena ndege zao zinalipuliwa? Na sasa russia yuko vitani na IS lakini IS bado ipo
 
Sasa kwa nini mwanzoni walikataa?

Manake waliambiwa na Marekani hiyo ndege ilidondoshwa na bomu wao wakajifanya wajuaji.

Mwishowe wameisoma namba na kukubali.

USA baby:usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2::usa2:

Walitaka wajiridhishe kwa uchunguzi wao
 
Tunaambiwagwa russia ni hatari sana kijeshi, vp tena ndege zao zinalipuliwa? Na sasa russia yuko vitani na IS lakini IS bado ipo

Tofautisha vita na ugaidi
 
Toka sku ya kwanza US na Uk walishasema ile ndege ilidunguliwa na magaidi,urusi wakakataa...sasa wamejionea wenyewe
Mmi nlishasema middle east kuingia ni lazima ukubali madhara kama haya...Putin kama ana intel ya kutosha ataweza kuwapata but sidha kama anayo
 
Siku zote nasema Suruhisho si makombora ya angani,mataifa yote makubwa yakiungana us,china,uk,france,russia italy nk wakipeleka majeshi yao ardhini na angani is wataisoma namba
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom