Tanzania inatafuta nini Urusi? (BBC)

Tanzania inatafuta nini Urusi? (BBC)

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,780
Reaction score
2,751
733f9eb0-5eca-11f1-b682-cf91850925ea.png.webp

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameanza ziara ya siku tatu nchini Urusi kuanzia Juni 3 hadi 5, 2026, ambapo atafanya mazungumzo rasmi na Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin, pamoja na kushiriki katika Jukwaa la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF 2026).
Hii ni ziara ya kwanza ya Rais Samia nje ya Bara la Afrika, tangu vurugu za uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, lakini ni ziara ya pili kufanywa na Rais wa Tanzania nchini Urusi tangu 1969 alipozuru Baba wa Taifa, Julius Nyerere.
Na kwa mujibu wa taarifa ziara hii inalenga kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na Urusi katika sekta mbalimbali za kimkakati, zikiwamo biashara na uwekezaji, elimu, sayansi na teknolojia, nishati, madini, kilimo na miundombinu, kwa mujibu wa Ikulu ya Tanzania.
Ziara ya Rais Samia nchini Urusi ni muhimu kiasi gani katika nyakati hizi? Je, Urusi inanufaika na mkusanyiko huu wa viongozi wa mataifa mengine katika nchi hiyo iliyotumbukia katika vita vya miaka minne na nusu sasa?

SPIEF ni nini?

Lengo la mkutano wa SPIEF (St. Petersburg International Economic Forum) ni kujenga na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, biashara, na uwekezaji kati ya Urusi, nchi zinazoibukia kiuchumi, na mataifa mengine duniani.

Mkutano huu, unaofanyika kila mwaka ni jukwaa la kimkakati linalowakutanisha viongozi wa serikali, wawekezaji, na wafanyabiashara ili kujadili mazingira ya uwekezaji na kusaini mikataba mikubwa ya kibiashara.
Pia mkutano wa kuimarisha ushawishi wa Urusi kiuchumi na kisiasa.
Uhusiano wa Tanzania na Urusi ni mzuri kwa muda mrefu. Miongoni mwa biashara kubwa kutoka Urusi zinazouzwa Tanzania ni vifaa vya ulinzi na usalama, ngano na mbolea. Mataifa haya yamedumisha uhusiano mkubwa wa kidiplomasia.

Jiji la Dar es Salaam lilikuwa mwenyeji wa kongamano la uchumi la “Jukwaa la Urusi na Afrika 2016" mwezi Aprili 2016.

Mwezi Oktoba 2019 pamoja na Julai 2023 ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri Mkuu wa wakati huo Kassim Majaliwa ulishiriki katika Mkutano wa kwanza na wa pili wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Urusi na Majukwaa ya Kiuchumi na Kibinadamu.

Putin anataka washirika

c3c13560-5eca-11f1-8b8c-6d33e1d5abb6.png.webp

Vita vya Ukraine vilivyoanza mwanzoni mwa 2022 vimeathiri uhusiano wa Urusi na nchi za Magharibi. Urusi imepata pigo kubwa kwa kukosa washirika wa kibiashara hasa kutoka mataifa hayo, sanjari na kuwekewa vikwazo vinavyolenga kudhoofisha uchumi wake na uwezo wa kugharamia vita.
Kupitia sekta ya Nishati, Marekani na nchi za Ulaya zimeweka vikwazo uuzaji wa mafuta na gesi asilia ya Urusi katika soko la kimataifa. Kwa sasa Urusi inategemea sana soko la Asia na Afrika.
Vilevile mataifa hayo yameiondoa benki kuu na benki nyingi za Urusi kwenye mfumo wa kimataifa wa miamala ya kifedha (SWIFT), pamoja na kufungiwa kwa akaunti na mali za benki hizo nje ya nchi.
Vikwazo havikuishia hapo, pia kuzuia akaunti za benki, kukamata mali (kama vile majengo na boti za kifahari), na kuweka zuio la kusafiri kwa maafisa wakuu wa serikali na wafanyabiashara wakubwa wanaomuunga mkono Rais Vladimir Putin.
Pia mataifa ya Ulaya na Marekani, yamezuia uuzaji wa teknolojia muhimu, vipuri vya ndege, na vifaa vya kijeshi kwenda nchini Urusi ili kukwamisha uwezo wao wa kijeshi.
Vikwazo hivi vinampa Putin kila sababu ya kutafuta washirika wapya nje ya bara la Ulaya na Marekani. Afrika na nchi kama Tanzania ni sehemu ya mkakati wa Urusi wa kuboresha washirika wake wa kiuchumi na kidiplomasia.

Tanzania inatafuta nini Urusi?

be94e5f0-5eca-11f1-b682-cf91850925ea.jpg.webp

Baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 na tuhuma za vurugu pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu zilizofuatia, Tanzania imejikuta ikikabiliwa na shinikizo linaloongezeka kutoka kwa mataifa ya Magharibi. Umoja wa Ulaya na Marekani zimekuwa zikitoa matamko, maazimio na hatua mbalimbali zinazoonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa kisiasa nchini.
Kwa upande wake, Serikali ya Tanzania imeendelea kusisitiza umuhimu wa kuheshimiwa kwa uhuru wa taifa, kutokuingiliwa kwa mambo yake ya ndani na kuheshimiwa kwa mamlaka ya taasisi zake. Hata hivyo, hali hiyo haijazuia kuendelea kwa ukosoaji kutoka kwa baadhi ya washirika wa Magharibi. Bunge la Ulaya, kwa mfano, limelalamikia kuzuiwa kutembelea Tanzania kufuatilia hali ya haki za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria.
Wakati huo huo, Marekani nayo imeonyesha wasiwasi wake. Muswada uliowasilishwa katika Seneti ya Marekani unataka mapitio ya uhusiano kati ya Washington na Dodoma, ikiwemo biashara, misaada ya maendeleo na ushirikiano wa usalama. Aidha, hatua ya kuweka vikwazo vya usafiri kwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Faustine Mafwele, imeongeza ishara kwamba uhusiano kati ya pande hizo unapitia kipindi kisicho rahisi.
Katika mazingira hayo, ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Urusi inaweza kutazamwa kama jitihada za kuimarisha ushirikiano na mshirika mwingine muhimu wa kimataifa. Wakati mataifa ya Magharibi yakiongeza shinikizo, Moscow inaweza kuonekana kama fursa ya kupanua ushirikiano katika biashara, uwekezaji, nishati, elimu, teknolojia na diplomasia.
Kwa mtazamo wa kisiasa, Tanzania na Urusi kwa nyakati tofauti zimejikuta zikikosolewa na baadhi ya mataifa ya Magharibi. Ingawa mazingira yao ni tofauti, hali hiyo inaweza kuchochea haja ya kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na kutafuta maeneo mapya ya maslahi ya pamoja.
Hivyo basi, swali la "Tanzania inatafuta nini Urusi?" linaweza kujibiwa kwa namna mbili. Kwanza, ni kutafuta fursa mpya za kiuchumi na maendeleo. Pili, ni kupanua wigo wa mahusiano ya kimataifa ili taifa lisitegemee upande mmoja pekee katika dunia inayobadilika kwa kasi.
Kadri milango ya Magharibi inavyoonekana kuwa na masharti zaidi, ndivyo Tanzania inavyoendelea kutafuta na kuimarisha urafiki na washirika wengine wa Mashariki.

Chanzo: BBC
 
View attachment 3600349

View attachment 3600350

View attachment 3600351

Mama ana tuhuma za kujibu na sio kukimbilia Urusi.
 
Tanzania president visits Russia as Western ties fray​

Tanzanian President Samia Suluhu Hassan begins a three-day state visit to Russia on Wednesday, meeting counterpart Vladimir Putin at a time when her country's reputation in the West has been badly damaged.

Western diplomats and rights groups have accused her government of massacring hundreds of people during election unrest in October and of conducting a spate of abductions and murders of critics in the run-up to the vote.

The United States has said it is reviewing relations with Tanzania in the wake of the violence, and last week sanctioned a senior police officer over the torture of two well-known activists.

By contrast, Putin was one of the first to congratulate Hassan for winning 98 percent of the vote.

Relations have been warming since. A Russia-Tanzania Business Council was created in January and last month Air Tanzania announced the launch of flights from Dar es Salaam to Moscow by the end of the year.

Hassan has been unapologetic about the political crackdown in her country, describing activists and protesters as "disrespectful children" who should be "beaten with canes".

She brings a business delegation to Moscow hoping to cement deals in trade, tourism and minerals during the first state visit to Russia by a Tanzanian president since the country's founding father, Julius Nyerere, travelled there in October 1969.

Trade currently stands at just over $307 million annually and the only concrete joint project is a planned uranium mine that has been on the drawing board for more than a decade.

Russia can use the support "even if just for an abstention for a critical vote at the UN" over the war in Ukraine, said a former political science professor at the University of Dar es Salaam, who was too scared to give his name due to repressive measures in the country.

"Russia is being opportunist... It doesn't have a massive amount to gain, but it is taking the opportunity of a weakened (Tanzanian) administration," added Fergus Kell, of British think tank Chatham House.

A government report into last year's election violence said 518 people were killed but did not say who was responsible, and there has been little sign of accountability.

=======================================================

Kwa watumiaji wa Kiswahili

Rais wa Tanzania Azuru Urusi Wakati Mahusiano na Mataifa ya Magharibi Yakidorora

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anaanza ziara rasmi ya siku tatu nchini Urusi siku ya Jumatano, ambapo atakutana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin. Ziara hiyo inafanyika wakati sifa ya Tanzania katika mataifa ya Magharibi imeathirika kwa kiasi kikubwa.

Wanadiplomasia wa Magharibi na mashirika ya kutetea haki za binadamu wameishutumu serikali ya Samia kwa madai ya kuhusika na mauaji ya mamia ya watu wakati wa vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi wa Oktoba mwaka jana, pamoja na madai ya utekaji na mauaji ya wakosoaji wa serikali kabla ya uchaguzi huo.

Marekani imesema inafanya tathmini upya ya uhusiano wake na Tanzania kufuatia vurugu hizo. Wiki iliyopita, iliweka vikwazo dhidi ya ofisa mmoja mwandamizi wa polisi kwa madai ya kuhusika katika mateso ya wanaharakati wawili maarufu.

Kwa upande mwingine, Putin alikuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza kumpongeza Samia baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi kwa asilimia 98 ya kura.

Tangu wakati huo, uhusiano kati ya Tanzania na Urusi umeendelea kuimarika. Mwezi Januari, Baraza la Biashara la Urusi na Tanzania lilianzishwa, na mwezi uliopita shirika la ndege la Air Tanzania lilitangaza mpango wa kuanzisha safari za moja kwa moja kati ya Dar es Salaam na Moscow kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Samia amekuwa akitetea hatua za serikali yake dhidi ya wapinzani na waandamanaji, akiwataja baadhi yao kuwa ni “watoto wasio na nidhamu” wanaostahili “kupigwa viboko”.

Katika ziara hiyo, ameambatana na ujumbe wa wafanyabiashara wenye lengo la kuimarisha ushirikiano katika biashara, utalii na sekta ya madini. Hii ni ziara ya kwanza ya rais wa Tanzania nchini Urusi tangu baba wa taifa, Julius Nyerere, alipozuru nchi hiyo mwezi Oktoba mwaka 1969.

Kwa sasa, thamani ya biashara kati ya Tanzania na Urusi ni takribani dola za Marekani milioni 307 kwa mwaka. Mradi pekee mkubwa wa pamoja ni mpango wa uchimbaji wa madini ya urani ambao umekuwa ukipangwa kwa zaidi ya muongo mmoja bila kuanza kutekelezwa.

Mwanasayansi wa siasa wa zamani kutoka University of Dar es Salaam, ambaye hakutaka kutajwa jina kwa kuhofia hatua za kisiasa, alisema kuwa Urusi inaweza kufaidika hata kwa kupata uungwaji mkono wa Tanzania au angalau kutopiga kura dhidi yake katika maamuzi muhimu ya Umoja wa Mataifa kuhusu vita vya Ukraine.

Naye Fergus Kell wa taasisi ya tafiti ya Chatham House alisema:

“Urusi inatumia fursa iliyopo. Haina faida kubwa sana ya kupata, lakini inachukua nafasi ya udhaifu wa utawala wa Tanzania kwa sasa.”
Ripoti ya serikali kuhusu vurugu za uchaguzi wa mwaka jana ilieleza kuwa watu 518 waliuawa, lakini haikubainisha waliohusika na mauaji hayo. Hadi sasa, kumekuwa na dalili chache za kuwawajibisha wahusika wa matukio hayo.

Chanzo:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom