Urusi kuwa na mji wa Bakhmut na Soledar, hasara ni kubwa kuliko faida

Wabongo mna shida sana.
Unaulizwa maswali unashindwa kuyajibu na badala yake unapiga blablaa ambazo ni tofauti na ulichoulizwa. Si bora ungeuchuna tu ungeepuka aibu ya kukosa hoja.
Ombea amani na usalama wa dunia. Huna maswali ya msingi. Yote uliyouliza ni mepesi na inaonyesha kuna vitu huvijui. Amani amani. 🙏🙏🙏
 
Unapoingia vitani huendi kufanya mzaha, hasa vita unayojua ni kwa uhai wa nchi yako, tofauti kabisa na kwenda kutalii kule kwa akina Taliban.
Hahahahaaah ndo maana wanaitaga Tour, 'I had a tour in Iraq and Afghanstan' utawaskia.

Linganisha na kauli nzito ilobeba mamlaka 'We are conducting a special Military operesheni in Ukraine'
 
Kweli ni hasara, kwanini ametumia muda mrefu? Lakini Kuna maswali Je idadi ya askali waiiokufa inaakisi uzito wa Vita. Kweli nihao au pungufu au zaidi ,vip adui yake NATO. YEYE amepata faida gani? Tuangalia Kwa jicho la tatu hivi ni vita vya kuchoshana sio kutafuta ushindi wa haraka.Wangetaka haraka wangetumia nyuklia. Pia ilikuepusaha maafa ya askali wengi SASA hivi Urusi anapigana Kwa uangalifu kuliko pale mwanzoni sababu ameshajua kuwa anapigana na NATO na washirika wao. HIVI NI VITA VYA KISASA ZAIDI KUWAHI KUPIGANWA. UNAHITAJI KUMSOMA ADUII WAKATI UNAENDELEA KUPIGANA
Lini Putin alitamka hilo? Hebu tutajie tu siku na tarehe aliyotamka hilo
Lengo la putini ni kurudisha ukreni yote iwe ya urusi na ndo lengo na alishasema yeye ni peter the great.
Na bdo anataka moldova pia.

Romania na poland wangekuwa sio ndani ya NATO nao yangewakuta.
 
5. Putin amechezewa changa la macho why kiufupi wanamtaka mkuu wa wagnér na ili kumpata nikumpa tonge la nyama na kwa kuwa nimroho atalifakamia ila kichwa chake ndio hali yao while anafakamia nyama. Nyie tulieni Putin atalia kama ubwa alie acha yatima na mama yake while ana nyonya. Hii vita inapigwa kwa akili kubwa sana kiasi Kuna siri siwezi kuziandika hapa ila tulieni Mrusi atalia kiasi Dunia itasikia. Siku za Putin ni fupi sana kuliko kesho na anajuwa muda wake upo ukingoni. Huwezi pigana vita huna chakula huna pesa.
Kwa mfuatiliaji mzuri wa vita hii, nadhani aliisikia ile kauli kuwa wataivuta vita hii kwa muda mrefu kadiri inavyowezekana mpaka watakapohakikisha Urusi siyo tishio tena kwa Taifa lolote.

Ushindi kwa nchi za Magharibi dhidi ya Urusi, wala siyo kuikomboa Bakhmut bali ni kuifanya Urusi imalize resources zake zote kwenye vita. Na baada ya hapo iwe Taifa dhaifu ambalo halitaweza kuwa tishio kwa usalama wa mataifa jirani, na wala asiwe na uwezo ya kusaidia tawala za kidikteta Duniani.

Hiyo ndiyo sababu ya kauli inayorudiwa mara kwa mara, 'tutaendelea kuisaidia na kuiunga mkono Ukraine bila ya kujali vita itachukua muda mrefu kiasi gani'.

Na sasa hivi, tayari uchumi wa Urusi umeanza kuyumba, sarafu inaanguka, mauzo ya mafuta na gas yanashuka, na India ambaye ni mnunuzi mkuu wa mafuta ya Russia amepewa onyo kuwa kama ataendelea kununua mafuta ya Russia, hataruhusiwa kuuza bidhaa yoyote inayotokana na mafuta kwa nchi za Magharibi. Vijana, hasa wataalam wa fani mbalimbali wanazidi kuikimbia Russia wakuenda nchi za Magharibi.
 
Ukweli Urusi ndiyo anaenda vizuri kwani Ukraine licha ya misaada yote kashindwa kuyafukuza majeshi ya Urusi tokea ndani ya Ukraine na hata Ukraine wameshindwa kutuma ndege za kivita Moscow?vita ni piga nikupige sasa mbona Ukraine haendi kupiga Urusi ?kashindwa vipi kufika Urusi?
Nadhani ungefatilia usingeuliza hili la ukreni kupiga urusi
Kama angeruhusiwa hata urusi ingekuwa na maumivu mabaya ila wanazuiwa sana na mghalibi na ndo maana siraha za maghalibi hazitakiwi kurushwa urusi kwa kuwa wanajua urusi itasikia maumivu na kuamua kutumia nyukria kwa kisingizio cha maghalibi.

Urusi ki ujumla vita imemshinda maana amepigana na watu ambao wana siraha za kiwango cha chini ili hali yeye anatumia vyanzo vyake vyote vyenye uwezo mkubwa.
 
Usikimbie au kuteleza kiaina bila kutujibu maswali haya tafadhari.

1. Hebu tueleze ni kwa namna gani Russia anajihakikishia usalama kwa kuchukua Bakhmut na Soledar?

2. Umekataa kuwa Russia/Wagner hawajapoteza wanajeshi zaidi ya 30,000 kwa Bakhmut na Soledar. Wamepoteza wanajeshi wangapi?

3. Kwa kuwa Russia katumia Mercenaries unataka kutuaminisha hao mercenaries siyo sehemu ya Russia kama unavyodai?

4. Hao Red Army wamekufa wangapi Bakhmut na Soledar?

Hebu tujibu hayo maswali tafadhari
Nadhani huyo Covax siyo mfuatliaji mzuri wa hiyo vita. Vifo vya askari wa Urusi ni vingi sana, na hiyo siyo kwa hisia bali kwa uthibitisho toka upabde wa Russia. Hata mkuu wa Wagner aliongea akiwa amesimama katikati ya maelfu ya majeneza ya askari waliokufa vitani akilalamika kuwa askari wake wamekuwa wanakufa kwa maelfu kutokana na kutokuwa na silaha za kutosha. Akatishia hata kuwaondoa askari waliobakia hai.
 
Kweli ni hasara, kwanini ametumia muda mrefu? Lakini Kuna maswali Je idadi ya askali waiiokufa inaakisi uzito wa Vita. Kweli nihao au pungufu au zaidi ,vip adui yake NATO. YEYE amepata faida gani? Tuangalia Kwa jicho la tatu hivi ni vita vya kuchoshana sio kutafuta ushindi wa haraka.Wangetaka haraka wangetumia nyuklia. Pia ilikuepusaha maafa ya askali wengi SASA hivi Urusi anapigana Kwa uangalifu kuliko pale mwanzoni sababu ameshajua kuwa anapigana na NATO na washirika wao. HIVI NI VITA VYA KISASA ZAIDI KUWAHI KUPIGANWA. UNAHITAJI KUMSOMA ADUII WAKATI UNAENDELEA KUPIGANA
Ukraine hawana chaguo jingine zaidi ya kupigana. Huwezi kuuliza eti wanapata faida gani!! Adui ameingia nchini kwao ametwaa maeneo, utakaa kimya?

Kwa upabde wa NATO, kumbuka kuna mataifa wanachama wa NATO yaliyokuwa sehemu ya USSR ambayo tayari yalikwishatishiwa na Russia, nayo kuvamiwa. Kama Russia angefanikiwa alichokitaka kwa Ukraine, next yangekuwa ni hayo mataifa. Mataifa haya yanaiona Ukraine inapigana kwa niaba ya mataifa yao pia.
 
Nadhani hana lengo la kumchakaza myukreini, labda inapobidi ili kutimiza lengo la SMO.

Ila lengo ni ulinzi zaidi ndio maana anapambana apate kushikilia maeneo strategic kiusalama sasa hivi na baadae.

Warusi na wayukreini mbona ni ndugu kabisa hao, anihilation sio lengo ila domination.
Upo wrong kabisa. Fuatilia historia ya mgogoro kuanzia 2014.
 
Urusi atashinda vita hii hata Nato waje na propaganda zipi hawataweza kumshinda Urusi
Kushinda vita ingekuwa ni rahisi kama hii kauli yako, Urusi ingekuwa aliishaikamata Ukraine ndanibya masaa 72 kama alivyotamka Putin.
 
Urusi hana sabau wala nia ya "kuichukua Ukraine yote", kwa hiyo hapa ndipo uchambuzi wako unapoonyesha udhaifu wake na katika mambo mengine uliyoyataja kwenye mada yako.

Sitayaghusa hayo mengine na kuyapa ufafanuzi kwa sasa hivi.
Kama mleta mada ni dhaifu, wewe utakuwa ni dhaifu mara 4 yake.

Mashambulizi ya mwanzo ya Russia yalikuwa wapi? Kwa kushambulia mji mkuu wa Ukraine, alilenga kitu gani? Ukijibu maswali hayo mawili itajulikana kama unaujua huo mgogoro au unausikia juu juu tu.
 
Tangu Urusi aivamie Ukraine Feb 2022 ni miezi 15 sasa, kuna mengi tumeona na kusikia kwa kila upande katika uwanja wa vita.

Kuna maeneo matano (5) ambayo Urusi na Ukraine wameyafanya kuwa ni ngome za mapigano. Miji hii ni Bakhmut, Soledar, Avdiivka, Kreminna na Vuhledar.

Katika miji hii miwili tu ndo imekuwa maarufu zaidi ambayo ni Bakhmut na Soledar. Hii ni kwa sababu ina umuhimu wake katika medani za kivita. Miji hii ni millitary strategic positions.

Urusi iliwekeza nguvu kubwa sana Bakhmut na Soledar, kwa maana ya millitary equipments na personnel. Waliwekeza nguvu kubwa kwa sababu waliamini kuwa wakiiteka Soledar na Bakhmut basi itakuwa rahisi kwao kusonga mbele kwenye miji mingine muhimu kama Slovyansk, Kramatorsk, Sivers'k, na Kostyantynivka. Bakhmut ndio Center (Military Hub) ya kuifikia miji hii sababu ni makutano ya njia kuu kutoka Horlivka, Luhans'ke, Popasna na Lysychans'k.

Urusi Kuichukua Bakhmut na Soledar kajihakikishia kuwa supply logistic (kwa barabara na Reli) itakuwa imara kwenda frontline.

Ni kweli Bakhmut na Soledar ziko mikononi mwa Urusi kwa 100% hilo halina ubishi, akibisha mtu basi ujue tangu akiwa tumboni alikuwa mbishi. Lakini ukweli ni kwamba Hasara ni kubwa kuliko Faida aliyopata.

Nakiri kuwa pande zote mbili zimepoteza resources kubwa (military equipment and personel). Lakini zaidi Urusi imepoteza wanajeshi wake wengi zaidi ya 30,000 waliokufa achilia mbali majeruhi kwa eneo dogo lenye jumla ya SQM 53.9. Bakhmut ina SQM 41.6 na Soledar 12.3. Bado nasisitiza Hasara aliyopata Urusi ni kubwa kuliko Faida aliyopata.

Kuna maswali mengi ya kujiuliza. Mimi nitauliza maswali machache na mengine mtaongezea;

1. Nguvu kubwa na rasilimali aliyowekeza Urusi kwa miezi 15 kwa Bakhmut na Soledar zenye eneo la jumla ya SQM 53.9 zimempa hasara au faida?

2. Kama anaweza kupigana kwa miezi 15 na kufanikiwa kuchukua eneo la SQM 53.9 ambao ni wastani wa SQM 3.6 kwa mwezi. Itamchukua muda gani kuichukua Ukraine yote kwa eneo ambalo hajalichukua zaidi ya SQM 482,960 ?

3. Kama imemchukua miezi 15 kuichukua Bakhmut na Soledar tu kwa direction ya Donetsk ni kweli ataweza kuichukua miji ya Slovyansk, Kramatorsk, Sivers'k, na Kostyantynivka, ukizingatia kuwa kila siku Ukraine wanazidi kuimarisha frontline na anga lao?

4. Urusi ataweza kuishikilia Bakhmut na Soledar kwa miezi 3 ijayo.? Au utakuwa ni ushindi wa muda kama ilivyokuwa Kwa Kherson city, Kharkiv na maeneo mengine?

5. Kwa kuwa Prigozhin amesema tarehe 25/05/2023 atawaachia Russian Regular troops ili wakapate mapumzika na mafunzo zaidi. Je, Russia regular troops watamudu peke yao kuushikilia mji wa Bakhmut bila Wagner?
Mkuu umeanza mada vizuri sana kuelezea umuhimu wa Bakhmurt kwa ufasaha kabisa.

Lakini maswali yako yanajijibu yenyewe kwenye hoja yako.

Kwenye swali 1, nguvu kubwa sio kumiliki eneo bali kukalia eneo ili kuwezesha operation kwenye mingine. Hii sio kwa Urusi tu hata Ukraine imefanya hivyo kwa kujua kuippteza Bakhmurt ni kupoteza maeneo mengi yanayolindwa strategically na Bakhmurt. Ni kama hapa Tanzania poppte unapoona kuna kambi ya jeshi hilo eneo ni mahsusi kulinda maeneo fulani nyeti.

Swali 2: swali lina ukakasi kwa maana umeifanya Urusi kwa miazi 15 imechukua mile 59. Hii si kweli chukua eneo lote la Ukraine lilichukuliwa gawanya na miezi ndio ujue kwa kipindi chote amefanikiwa kwa kiasi gani kwa siku, week, Mwezi au miezi 15. Ni kweli maeneo hayo mawili yalikua na ugumu sana kwa sababu tu ya unyeti wake.

USA amepigana miaka 11 huko Afganistan lakini alishindwa kuyafikia baadha ya maeneo na ndio maana siku tatu tu US walipotangaza kuondoka wenyewe walichukua nchi yao na vifaa vita vyote vya kijeshi vya US vilichukuliwa. Nimekupa huu mfano utambue ugumu wa kufika baadhi ya strategic area au umuhimu wa kuwa na stratevic position over your opponent.

Swali 3:Umelijibu katika maelezo yako kwamba kuanguka kwa Bakhmurt kunaongeza urahisi wa usafirishaji wa vifaa na wapiganaji na kurahisisha kuvamia maeneo mengine. Ingawa lengo la Urusi sio kukalia maeneo ya Ukrain bali kuondoa silaza zote za NATO, kuifanya Ukraine isiingie NATO, na kuondoa element zote za kinazi.

Swali 4 n 5, yanashabihiana. Umetoa mfano wa Kakhiv na kwengine waliwithdraw ndio kwa sababu ya risk kubwa iliyokuwepo ya kubomoa dam na kuvunja Daraja na kugawa wanajeshi waliopo ngambo ambapo wangekosa namna ya kupata msaada wa haraka wa vifaa na hata wapogananaji busara ikaonekana warudi nyuma hadi ngambo ya mto. Sambamba na hilo hata walichokuwa wanataka kukilinda hakipo eneo husika wakarudi nyuma kulinda askari na vifaa badala vipelekwe sehemu yenye uhitaji.

Kumbuka Ukraine anapigana na kikundi cha mgambo well trained Wagner, hawana ndege, hawana air power vyote vipo kwenye jeshi la Urusi. Unawezaje kuhoji uwezo wa Jeshi la Urusi kushilikia eneo husika kama Wagnerwataenda mapumziko.

Tutapata taarifa ya raia wa nchi ngapi wamehusika kupigania Bakhmurt upande wa Ukraine soon tutapata taaifa na wangapi walikuwa neutralized
 
Una flaws nyingi kwenye andiko lako:
1. Unaongelea ukubwa wa gharama ila hauzitaji.
2. Umeweka baadhi ya namba ila hujaweka Source.
3. Hebu jiridhishe hapo kwenye 'SQM'. Unajua Heka Moja ya shamba Ina SQM 70?
 
Ukweli ni Urusi yupo Ukraine kwa miezi kibao sasa na Uongo ni Ukraine kudai atawapiga Urusi licha ya kupata misaada mingi tokea NATO
Hebu tutajie misaada ambayo Ukraine amepata kutoka NATO ni ipi na ni lini
 
Kwahiyo wewe umeona kweli kuhakikisha usalama na kuwepo kwa Russia ni gharama ndogo kweli? Analysis yako ni ya layman militarily kuna sehemu ndogo 10km lakini ina umuhimu kuliko eneo lenye 10000 Square kilometer, nani kakwabia kwa 30.000 jeshi ndo walikufa Russia katimia macenary sio Red army......bado urusi inanguvu hata Nato inakubali kabisa.
Afadhali umemjibu na hiyo no.2
Kwa maelezo yake ana amini kwakuwa eneo lenye ukubwa fulani, limetekwa kwa muda fulani basi na eneo lililobaki litatekwa kwa proportional hiyo hiyo.
Kwakua mpaka dakika ya 15 tumeshashinda goli moja basi ikifika dakika 90 tutakuwa tumeshapata magoli 6.
Mpaka HT watujaruhusu goli, basi hadi kipenga cha mwisho hatutakua tumefungwa.
Ameathiriwa sana na Somo la physics.
 
Kwa mfuatiliaji mzuri wa vita hii, nadhani aliisikia ile kauli kuwa wataivuta vita hii kwa muda mrefu kadiri inavyowezekana mpaka watakapohakikisha Urusi siyo tishio tena kwa Taifa lolote.

Ushindi kwa nchi za Magharibi dhidi ya Urusi, wala siyo kuikomboa Bakhmut bali ni kuifanya Urusi imalize resources zake zote kwenye vita. Na baada ya hapo iwe Taifa dhaifu ambalo halitaweza kuwa tishio kwa usalama wa mataifa jirani, na wala asiwe na uwezo ya kusaidia tawala za kidikteta Duniani.

Hiyo ndiyo sababu ya kauli inayorudiwa mara kwa mara, 'tutaendelea kuisaidia na kuiunga mkono Ukraine bila ya kujali vita itachukua muda mrefu kiasi gani'.

Na sasa hivi, tayari uchumi wa Urusi umeanza kuyumba, sarafu inaanguka, mauzo ya mafuta na gas yanashuka, na India ambaye ni mnunuzi mkuu wa mafuta ya Russia amepewa onyo kuwa kama ataendelea kununua mafuta ya Russia, hataruhusiwa kuuza bidhaa yoyote inayotokana na mafuta kwa nchi za Magharibi. Vijana, hasa wataalam wa fani mbalimbali wanazidi kuikimbia Russia wakuenda nchi za Magharibi.

Youn have a point. Kwamba;
1. Bakhmut imetumika kama trapping position kwa Russia ndo maana akapeleka resources kubwa. Matokeo yake kapoteza wanajeshi wengi na vifaa vingi (Heavily inflicted) with small gain. Ni njia ya ku drain resources zake. Kwenye hilo kuna hoja.

2. USA, German and allies wana prolong vita kwa lengo la kumdhoofisha Russia na kujua uwezo wake unakoishia ili mwisho wa siku asiwe na madhara kwa nchi zingine. Hiyo ni hoja ya msingi ina mashiko.

3. Russia anazoofishwa kiuchumi. Uchumi wake unazidi kusinyaa. Vita ikiendelea atashindwa kui finance na hataweza kushinda hii vita.
 
5. Putin amechezewa changa la macho why kiufupi wanamtaka mkuu wa wagnér na ili kumpata nikumpa tonge la nyama na kwa kuwa nimroho atalifakamia ila kichwa chake ndio hali yao while anafakamia nyama. Nyie tulieni Putin atalia kama ubwa alie acha yatima na mama yake while ana nyonya. Hii vita inapigwa kwa akili kubwa sana kiasi Kuna siri siwezi kuziandika hapa ila tulieni Mrusi atalia kiasi Dunia itasikia. Siku za Putin ni fupi sana kuliko kesho na anajuwa muda wake upo ukingoni. Huwezi pigana vita huna chakula huna pesa.
Wewe tumainie una uandishi fulani wa kiboya sana. Eti unasema "kuna siri siwezi kuziandika hapa" !! Una siri gani wewe mlamba makombo wa Sukuma Gang?
 
Tangu Urusi aivamie Ukraine Feb 2022 ni miezi 15 sasa, kuna mengi tumeona na kusikia kwa kila upande katika uwanja wa vita.

Kuna maeneo matano (5) ambayo Urusi na Ukraine wameyafanya kuwa ni ngome za mapigano. Miji hii ni Bakhmut, Soledar, Avdiivka, Kreminna na Vuhledar.

Katika miji hii miwili tu ndo imekuwa maarufu zaidi ambayo ni Bakhmut na Soledar. Hii ni kwa sababu ina umuhimu wake katika medani za kivita. Miji hii ni millitary strategic positions.

Urusi iliwekeza nguvu kubwa sana Bakhmut na Soledar, kwa maana ya millitary equipments na personnel. Waliwekeza nguvu kubwa kwa sababu waliamini kuwa wakiiteka Soledar na Bakhmut basi itakuwa rahisi kwao kusonga mbele kwenye miji mingine muhimu kama Slovyansk, Kramatorsk, Sivers'k, na Kostyantynivka. Bakhmut ndio Center (Military Hub) ya kuifikia miji hii sababu ni makutano ya njia kuu kutoka Horlivka, Luhans'ke, Popasna na Lysychans'k.

Urusi Kuichukua Bakhmut na Soledar kajihakikishia kuwa supply logistic (kwa barabara na Reli) itakuwa imara kwenda frontline.

Ni kweli Bakhmut na Soledar ziko mikononi mwa Urusi kwa 100% hilo halina ubishi, akibisha mtu basi ujue tangu akiwa tumboni alikuwa mbishi. Lakini ukweli ni kwamba Hasara ni kubwa kuliko Faida aliyopata.

Nakiri kuwa pande zote mbili zimepoteza resources kubwa (military equipment and personel). Lakini zaidi Urusi imepoteza wanajeshi wake wengi zaidi ya 30,000 waliokufa achilia mbali majeruhi kwa eneo dogo lenye jumla ya SQM 53.9. Bakhmut ina SQM 41.6 na Soledar 12.3. Bado nasisitiza Hasara aliyopata Urusi ni kubwa kuliko Faida aliyopata.

Kuna maswali mengi ya kujiuliza. Mimi nitauliza maswali machache na mengine mtaongezea;

1. Nguvu kubwa na rasilimali aliyowekeza Urusi kwa miezi 15 kwa Bakhmut na Soledar zenye eneo la jumla ya SQM 53.9 zimempa hasara au faida?

2. Kama anaweza kupigana kwa miezi 15 na kufanikiwa kuchukua eneo la SQM 53.9 ambao ni wastani wa SQM 3.6 kwa mwezi. Itamchukua muda gani kuichukua Ukraine yote kwa eneo ambalo hajalichukua zaidi ya SQM 482,960 ?

3. Kama imemchukua miezi 15 kuichukua Bakhmut na Soledar tu kwa direction ya Donetsk ni kweli ataweza kuichukua miji ya Slovyansk, Kramatorsk, Sivers'k, na Kostyantynivka, ukizingatia kuwa kila siku Ukraine wanazidi kuimarisha frontline na anga lao?

4. Urusi ataweza kuishikilia Bakhmut na Soledar kwa miezi 3 ijayo.? Au utakuwa ni ushindi wa muda kama ilivyokuwa Kwa Kherson city, Kharkiv na maeneo mengine?

5. Kwa kuwa Prigozhin amesema tarehe 25/05/2023 atawaachia Russian Regular troops ili wakapate mapumzika na mafunzo zaidi. Je, Russia regular troops watamudu peke yao kuushikilia mji wa Bakhmut bila Wagner?
Hapo kwenye SQM uko sahihi kweli!!!?? Yaani mji uwe na SQM 53!!!???
 
5. Putin amechezewa changa la macho why kiufupi wanamtaka mkuu wa wagnér na ili kumpata nikumpa tonge la nyama na kwa kuwa nimroho atalifakamia ila kichwa chake ndio hali yao while anafakamia nyama. Nyie tulieni Putin atalia kama ubwa alie acha yatima na mama yake while ana nyonya. Hii vita inapigwa kwa akili kubwa sana kiasi Kuna siri siwezi kuziandika hapa ila tulieni Mrusi atalia kiasi Dunia itasikia. Siku za Putin ni fupi sana kuliko kesho na anajuwa muda wake upo ukingoni. Huwezi pigana vita huna chakula huna pesa.
Sitaki kuamini kuwa unamaanisha ulichoandika! Kama unamaanisha basi pole sana, ujinga ni mzigo.
 
Back
Top Bottom