Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,194
- 10,929
Katika mwaka huu 2023 dunia imeshuhudia vita vikali ambavyo historia haijawahi kuvishuhudia. Bomu la Hiroshima lilikuwa na moto mkali lakini ilikuwa ni wa mara moja halafu ikawa basi ni kuokota wahanga na majeruhi.
Eneo la Mariupol ambalo Urusi ililiteka kutoka Ukraine ilichukua muda mrefu kuweza kufanikiwa kulitia mkononi.
Urusi ilitumia silaha nzito kupambana na kikosi cha Azov kilichokuwa na silaha nzito na kusaidiwa na jeshi mama la Ukraine ambalo nalo lilikuwa na silaha nzito ikiwemo ndege za kivita.Hatimae kikosi cha Azov kilijichimia ndani ya mahandaki ya kiwanda cha Azovstal ambayo yalikusudiwa kujilinda kutokana na mashambulio ya nyuklia.
Katika kukamilsha Ili kukamilisha kulidhibiti eneo hilo Urusi ilitumia zaidi mizinga mizito kwa kuhofia kutumia ndege za kivita wakati Ukraine ilikuwa bado ina uwezo wa kuzitungua ndege za Urusi
Sehemu nyingine iliyoshuhudia vita vikali vilicyohusisha silaha nzito ni Bakhmut ambapo jeshi la Urusi chini ya vikosi vya Wagner vilivyoendeshwa na Prigozhin lilipigana kwa muda mrefu pembeni na ndani ya mitaa ya Bakhmut. Mwishowe vikosi vya jeshi la Ukraine vilishindwa.
Maeneo hayo mawili mapigano yalikuwa ni baina ya majeshi mawili makubwa yenye sialha nzito moja likisaidiwa na jumuiya ya nchi za NATO.
Tukija Gaza katika kumbukumbu za kivita hakuna jeshi liliotumia silaha nzito zaidi na zenye nguvu kuliko jeshi la Israel.Jeshi hilo limekuwa huru kutumia aina zote za silaha ilizonazo.Majumba ya ghorofa yameshuhudiwa yakiporomoka kama maboksi kwa sekunde chache.na kufukia wote waliokuwemo humo.
Mashimo makubwa yamechimbuliwa na silaha hizo zinazopigwa kwa mfululizo usiku na mchana.Cha kushangaza na kinyume na Mariupol na Bakhmut silaha hizo nzito zinazosababisha moto unaoenea Gaza nzima na kusababisha ardhi kutetemeka zinatumika dhidi ya wanamgambo wa Hamas ambao silaha zao zote ni hafifu sana.
Mbali na kwamba mtu atasema huo ni ukatili lakini papo hapo atajiuliza mbona hazileti matokeo yaliyotajwa kama ndio malengo ya kupigwa kwa kiwango hicho.Malengo hayo ni kuwamaliza Hamas na kuwaokoa mateka.
Hapa ni wazi kuwa malengo yaliyotajwa ilikuwa ni sababu na ajenda zimebadilika.Lengo si kuwafuta Hamas pekee wala hakuna umuhimu mkubwa kuokoa mateka kwani kwa akili za kibinadamu inaonesha upigaji wa kiwango hiki kwa asilimia kubwa mateka watakufa pamoja na watekaji wao
Tofauti nyengine kati ya vita vya Mariupol na Bakhmut dhidi ya Gaza ni kuwa vita vya Gaza vinaoneshwa mubashara kupitia kamera zilizotegeshwa na mashirika mbali mbali ya habari yakiongozwa na Aljazeera.
Suali la kujiuliza ni jee ukali wa silaha zinazotumika na ukatili wa Gaza utaishia kwa kushindwa kwa Hamas tu au kuna kitu kingine Mwenyezi Mungu kakipanga kuwaonesha viumbe wake waovu katika kuwaokoa wao na adhabu ya moto mkali kuliko huo na ya milele.Kwa maana vita vitakapomalizika kwa kushindwa Israel kufikia malengo ya wazi waliyoyataja basi binadamu wote watajua kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mwenye nguvu na mshindi wa mwisho.
Kwani Yeye siye yule aliyemuokoa mtume wake Ibrahim a.s kutoka katikati ya rundo la moto wa kuni.Moto ulipomalizika waliotaraji kuona majivu ya Ibrahim a.s wakamuona akiwa amekaa kitako yuhai.
Na jeeYeye siye Yule aliyemfanya Firauni akaukushanya umma wa watu wake washuhudie ushindi wake dhidi ya uchawi wa Mussa a.s.Matokeo yake Mussa akawa mshindi mbele ya macho yake na kuadhirika mbele ya aiowakusanya washuhudie ushindi huo.