CNN: Leo Urusi imeuteka rasmi mji wote wa Bakhmut licha ya silaha kali za USA+NATO zilizomiminwa Ukraine kuilinda Bakhmut

Sikirimimimasikini

JF-Expert Member
Dec 27, 2019
2,919
15,604
CNN yaripoti kuwa hatimae leo Wagner wameukomboa mji wote wa Bakhmut licha ya jitihada kubwa za Marekani + Uingereza + Ujerumani + NATO kutuma kila aina ya silaha walizoziamini (kupitia mahesabu ya kwenye makaratasi) kuwa zingekuwa mwarobaini (a.k.a. game changer) wa kuishinda Urusi vitani.

Silaha hizo zilizoshindwa na kufeli vibaya mbele ya ma-security guards wa kampuni ya ulinzi ya kirusi (Wargner group company) kwenye uwanja wa vita wa Bakhmut ni pamoja na HIMARS na HARM za mMarekani, Leopard 2 tank ya Mjerumani, challenger 2 tank ya Muingereza (hizo ni chache tu kama mifano ila zipo nyingi tele).

Prigozhin, kiongozi wa kampuni ya ulinzi ya Wagner, aliyeonekana leo akiwa ndani ya nguo za kivita kwenye safu za wapiganaji huko Bakhmut, ametangaza kuwa wamehitimisha mapigano ya nyumba kwa nyumba na kuikomboa Bakhmut yote leo mchana wa saa sita. Na akaongeza kuwa wanatarajia kuukabidhi rasmi mji huo wa Bakhmut kwa jeshi la Urusi wiki ijayo tarehe 25 May na kisha wao (Wagner) waondoke wakapumzike na kufanya mazoezi yao ya kivita kujiandaa na majukumu mengine watakayopewa na Putin.

Habari hii imeletwa na CNN pamoja na The Jerusalem Post (chombo cha habari cha taifa teule la Israel)

Cc: MK254

======

SmartSelect_20230520-180917_Chrome.jpg
SmartSelect_20230520-181007_Chrome.jpg


SmartSelect_20230520-181128_Chrome.jpg

Screenshot_20230520-181341_Chrome.jpg
 
Dah.
NATO NATO NATO NATO kwa mara nyingine tena
Wameshindwa na Kikundi Cha wapiganaji TU.
Kama vile walivyoshindwa na Kikundi Cha wapiganaji Cha Talaban.
Nauliza kwa dharau kama ambavyo pro NATO wengi huongea kwa dharau dhidi ya jeshi kubwa kabisa hapa Duniani.Red Army.
Kuwa Russia ni Supa pasa wa mchongo.
Sasa NATO tuwaiteje?
Ewe msomaji wa komenti hii kama NATO ni strong je kwa Nini walikimbia na kuwaachia masilaha mengi Watalaban?

Niambie basi,kama NATO ni strong kwa Nini wamezidiwa nguvu na Wagner?

Je si mlikua mnashangilia Kila siku package mpya za vikwazo na michango ya masilaha Kali kutoka nchi wanachama Wa NATO?

Haya ndugu zangu,vita bado ni mbichi kabisa.
Najua vita hii ni vita ya utawala,yaani atakaeshinda ndio mtawala wa Dunia na atakaeshindwa ndio kapoteza utawala wa Dunia.
Je wanaoonekana kua ndio watawala Sasa hivi watakubali kushindwa na kupoteza utawala?

Ni suala la muda.
Muda hua unaongea.
Nadhani Sasa muda ndo unaongea.

Tusubiri teke la mwisho la farasi anaekufa.
 
Siku zote vita za wazungu zinakuwaga vita za dunia yote.tumeona vita zilizoitwa za kwanza na za pili za dunia ilikuwa vita za wazungu lakini mabwege wote tuliobakia tukajumuishwa humo watu wetu wakafa mazingira kuharibiwa nk. Hii ya sasa pia ni wazungu wa mashariki (warusi) wanapambana na wazungu wa magharibi (NATO na washirika wao japan na wengineo) katika ardhi ya ndugu zao ukraine.siku si nyingi wakishindwana wakianza kutumia nyuklia tutaambiwa sasa hii ni vita ya dunia kutetea uhuru na demokrasia sijui na ujinga ujinga gani.mabwege wote tuliobakia vita vyetu ni vyetu (angalia sudan,somalia,colombia,yemen,palestina,venezuela,sahara magharibi nk nk nk)
 
Back
Top Bottom